Benjamin Sawe na Beatrice Mlyansi - Maelezo,Dodoma

Imeelezwa kuwa Serikali inakusudia kulipa malimbikizo ya posho za uhamisho wa askari hadi kufikia mwezi Juni 2011.

Akijibu swali la Mbunge wa Manyoni magharibi John Lwanji,Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi Hamisi Kagasheki alisema fedha za posho kwa ajili ya askari hutengwa katika bajeti ya Serikali kwenye fungu la matumizi mengineyo.

Mheshimiwa Kagasheki alisema kuwa kutokana na uhaba wa fedha inakuwa vigumu kuwapatia malipo askari wote waliopewa uhamisho.

Alifafanua kuwa utaratibu wa kutenga fedha za malipo ya posho za askari kwenye bajeti ya Serikali kwenye fungu la matumizi mengineyo si mzuri na unapunguza morali kwa askari ambapo alisema ili kuboresha hali hiyo Jeshi,Jeshi la polisi lipo katika mpango wa kuboresha utendaji wa Jeshi la Polisi.

Aidha Mheshimiwa Kagasheki alisema kuwa sehemu ya maboresho hayo inahusisha umuhimu wa kuzingatia maslahi ya askari na kuweka mifumo ambayo haitaruhusu askari kuhama bila kulipwa fedha za posho

Akitoa ufafanuzi kuhusu malimbikizo ya vyombo vyote vya usalama,Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo alisema malimbikizo yote ya vyombo hivyo yatakuwa yameshalipwa kabla ya tarehe 30,June,2011.

Akijibu swali la Mbunge wa Wete Mheshimiwa Mbarouk Ali la Serikali inampango gani wa kuongeza majengo katika eneo la Limbani Wete ambalo lina nafasi,Naibu Waziri Hamisi Kagasheki alisema Serikali inampango wa kujenga mengine katika eneo hilo na maeneo mengine nchi nzima ili kuzingatia na upatikanaji wa fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...