Bwana michuzi,
Cheki mambo hayo! Niko hapa Jakarta, Indonesia na nimefurahi kuona huu mradi wao wa mabasi yaendayo kasi. Sijui kwa muundo wa barabara za Dar es salaam hii itawezekana maana ufinyu wa barabara zetu hauwezi kuruhusu barabara spesho ya mabasi hayo kama unavyoona hapa kwa wenzetu. Sijui lakini... labda inawezekana...
Mdau Jakarta


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2011

    Mzee mwenyewe hilo linawezekana....ni kuongeza tu upana wa barabara, sema tu wanaojenga wanatumia Wachina ambao kwao hakuna barabara za namna hiyo!...Halafu kwa nini mainjinia wetu wasitembelee nchi km UK au huko uliko mzee na kwingineko, ili wapate uzoefu wa namna mambo ya usafiri yanavyoenda!!...sema hela yote iko kwa mafisadi, hiyo nayo noma!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2011

    Tatizo nadhani siyo ufinyu wa barabara kwani zitapanuliwa na kuwa kama hivyo. Tatizo kubwa zaidi ni nidhamu mbovu ya madereva wetu kuwa hawataingilia barabara hiyo baada ya kuona foleni zao haziendi. Tatizo lingingine ni watembea kwa miguu wengi wanaweza kupoteza maisha kwa uzembe wao wa kuvuka katika hali kama hiyo (mengine yako kwenye foleni mengine yanaenda kasi). Elimu ya kutosha inatakiwa kuepusha maafa..

    Mzozaji.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 29, 2011

    hahaa hiyo ni barabara kwa ajili ya public transpot, na emergency kama ambulance, zima moto, na police, sioo speacial kwa mabasi yaendayo kasi acha kupotosha watu mdau, umefika nje juzi nini? na kama hujuwi ungeuliza kwanza... unafika tu nje na unaanza kupotosha watu kuwa mstaarabu..

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2011

    Je mabasi yaendayo kasi ndio yepi? Hapo wadau wengi hawakufahamu. Hiyo habari iliandikwa kwenye Nipashe na wenziwe kuwa maandalizi ya ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi umeanza. Hata Mithupu naye aliweka hiyo habari. Hiyo inayoonekana hapo pichani ni "lane" ambayo imetengwa kwa kazi maalum. Kuweka kwa "lane" kama hizo kutaneemesha trafiki maana wabongo wakiona barabara iko tupu watawahi, sasa trafiki watakaa kukamata wale wanaovunja sheria na wakitoa kitu kidogo wanaachiwa. Ili kuondoa tatizo la foleni Dar ni kujenga barabara mpya mbili tu zinatosha za kilomita 20. Isipokuwa itabidi nyumba zivunjwe kupisha hizo barabara mpya. Moja ipite katikati ya eneo kati ya barabara ya morogoro na ya kuendea Oysterbay, nyengine ipite Bandarini izinguke mpaka uwanja wa ndege, indelee mpaka mwenge.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2011

    Anony wa Wed Jun 29 02:52:00 AM 2011, wewe ndo unapotosha umma, mdau yupo sahihi kabisa. Hiyo ni njia ya mabasi yaendayo kasi. Hata huu wanaotaka kuuanzisha Bongo upo katika mfumo huo. Usichonge bila Evidence nenda Ubungo Plaza Gorofa ya kwanza katika ofisi za DART watakuonyesha michoro. Yote yanawezekana cha msingi ni commitment tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 29, 2011

    we mdau wa wed jun29.02:5200 am 2011 ndio wale wale. sasa hapo ni kitu gani kimekufanya urukie conclusion eti hapo ni emergence, sasa public transpost ni nini kama sio hayo mabasi yaendayo kasi? au wewe ndi mmoja wa wale wanaodhani mabasi yaendayo kasi ni maana yake yana mwendo wa kasi? JITAHIDI kusoma zaidi kuhusu BRT, WEWE HAPO NDIO CHANZO CHA KUPOTOSHA JAMII, NA KEJELI ZA AJABUAJABU ETI KWA SABABU KAFIKA NJE JUZI JUZI, WE ULIYEFIKA NJE ZAMANI UMECHANGIA NINI KATIKA KUTOPOTOSHA WATU, HIYO HAPO NI (BRT LANE) NA HAYARUHUSIWI MAGARI MENGINE KUPITA, BRT ONLY, MDAU KAONA VILE SHERIA ZINAFUATWA KATIKA ENEO ALIPO NDIO MAANA KUTUWEKEA HAPA NASI TUJIFUNZE NA KUONA KAMA KWETU INAWEZEKANA, DART, AMBAYO NI DAR ES SALAAM RAPID TRANSIT WAMESHAANZA KUJENGA KITUO PALE FERRY, NA UPIMAJI UMESHAANZA PALE AIZKIWE STREET, NA UKIANGALIA UFINYU WA BARABARA ILE NA HII NI SAWASAWA KABISA, NA HILO LINAWEZEKANA, KUNAWEZA KUWA NA LANE MBILI, MOJA YA BRT KAMA HAPO KWENYE PICHA NA NYINGINE KWA MAGARI MENGI, PS MABASI YAENDAYO KASI HUWA HAYAMAANISHI SPEED 120 AU ZAIDI, HAPANA NI YA KASI KWA MAANA BARABARA ZAO HAZITUMIWI NA MAGARI MENGINE NA HVYO KUYAFANYA YA HARAKA KWA KUTOKUA NA FOLENI LABDA TUU KUSIMAMA KENYE MATAA.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2011

    Hapa inaonesha jinsi gani mtu ataacha gari lake nyumbani na kupanda basi ili awahi mahali. Na hii itapunguza idadi ya magari mjini. Kwa sababu ukichukua gari lako binafsi utakaa kwenye Jam zaidi kuliko ukipanda daladala.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 29, 2011

    ujinga wenu utawapotosha.. kaeni na hayo mawazo yenu ya mabasi ya kasi. umasikini mbaya sana

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 29, 2011

    Wadau,

    In principle wote mpo sawa. BRT (Bus Rapid Transit) inatekelezwa tofauti katika masoko tofauti. Kuna wanaotumia "mabasi ya kawaida" yaliyotengewa lane maalum(kama mdau wa Indonesia alivyoona), kuna yanayopita kwenye njia zilizotengwa kwa watumiaji walio na zaidi ya mtu mmoja ndani ya chombo, zinaitwa *HOV (High Occupancy Vehicle)...hii ni kusema kuna wanaoruhusu magari ya kawaida kutumia njia hizi maalum kama kuna zaidi ya abiria mmoja ndani ya chombo (kama ni HOV lane, na kuna ambao yanaruhusiwa mabasi pekee.

    Kuna masoko ambayo wanaotumia "mabasi maalum" yenye kutumia njia zilizojengwa maalum kwa mabasi haya. Unaweza ukayata treni za mwendo kasi na bado ukawa sawa (japo wenyewe wanayaita "mabasi"). Njia zake zimejengwa na mataruma laini/mepesi ya reli. Haya wanakwenda kasi kuliko mabasi ya kawaida, na yana vituo vikubwa (terminal) ambazo yanasimama. Kwa kawaida yanapita kwenye njia kuu pekee i.e. kama ni Bongo, itakuwa Morogoro Rd, Kilwa Rd, Ali Hassan Mwinyi (aka Old Bagamoyo Rd), Kawawa Rd nk.

    Kujielimisha zaidi gonga
    http://www.gobrt.org/whatis.html na pia unaweza gonga http://en.wikipedia.org/wiki/Bus_rapid_transit

    Kaka Yenu

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 30, 2011

    kweli watu wazima na akili zao wanafikiria kuwa mabasi yaendayo kasi.. yataenda kasi vipi hapo? ni kuwa tu hiyo njia haina foleni magari ya kawaida hayaruhusiwi kupita njia hiyo, zaidi ya public transport, police, firefighter, na amburance... basi wao kwa ujinga wa watanzania tulionao wameona ni barabara ya mabasi yaendayo kasi.. hivi je nyie wote hapo mlioweka comment mmelifikiria jambo jingine zaidi ya mabasi yaendayo kasi? na ndio maana tanazania hatuendelei watu fikira ziko finyu sana.. poleni sana ni umasikini na ushamba unatasumbua tena bila ya aibu unaweka comment kushabikia hilo.. hahahaaha

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...