Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Tatu Mapando, ambaye ni mmoja kati ya vijana waliotoa ushuhuda mbele ya Makamu wa Rais kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya, baada ya kuacha kutumia madawa hayo. Tatu aliwahi kuwa mnenguaji wa muziki wa dansi katika bendi za Fm, Academia, Diamond Sound, Betta Musica na bendi kadhaa za jijini kabla ya kuanza kutumia madawa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkemia Mkuu wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Bertha Mamuya (katikati) wakati alipotembelea na kukagua mabanda katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam leo, wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kupiga vita Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam leo.
Vijana waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya, Rajab Huseein na Tatu Mapando, wakitoa ushuhuda kuhusu utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kuacha kutumia madawa hayo.
Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyokuwa katika moja ya mabanda hayo kwa ajili ya maonyesho.


KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2011

    Je lile kabila linalokula bangi kama mboga ya ugali mbona hawajaadhirika?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2011

    hizo kuber mbona ni poa tu kwa handas, tangu zimekuwa mihadarati??

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2011

    watanzania uchwari wanapewa hela ya kuamua nini ni bora na nini si bora.kudadadeki mbona mfano wamarekani wanawatesa watu wao kwa kuwapa dawa adictive?nani anayeamua kiwango cha kimataifa WTO?jiulize ni nini haswa kiwango cha ubora wa embe kufikia international standard.im tired of been da only knowlegeable one.i knw many r there,pliz nipe tano.masikini kuber london west ham zimejaa kibao,ni 60 pence,mbona mnatuchanganya.kwangu dawa ya kulevya kwanza ni amerika,kisha vinginevyo pmj na ngoism.

    ReplyDelete
  4. sijamuelewa mchangiaji wa tatu kutoka mwanzo, labda mniambie naye ni muathirika wa hayo madude ya kulevywa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2011

    hicho kibakuli chenye sausage rangi nyekundu na nyeupe nayo mada ya kulevya pia au?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 28, 2011

    naona mr john anaswali tu,hana oni na akiwa nalo litakuwa na msingi wa swali tu.fuatilia kinachotokea mpaka kitukinawekwa kwenye sheria za anti narcotic drugs.jana hakikuwemo leo kimo.tofautisha cocaine from da moment inaonekana ni tayari haramu.fananisha mchango wa marekani kuchochea nchi kusign anti terrorism mpaka sasa mlipopigwa bomu embassy 1997,anti Drug Abuse and Illicit Trafficking etc.sasa kuber inafanya nini haswa mpaka ikafikia kiwango cha narcotic drug? uk full mpeto,nawaamini hawa watu wa huku,kwa tayarifa sio wote wa uk ni wazungu(nazungumzia waingereza sio wazungu panua hapo)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...