Baadhi ya Wasikilizaji wa Radio Ebony Fm walioshiriki promotion hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa Ebony FM radio nje ya ukumbi wa VETA mjini Iringa

Mshindi wa Promotion ya Radio Ebony Fm Axzavery Mlawa na mgeni rasmi wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa radio Ebony FM

Mgeni Rasmi Daniel Kadine ambaye ni afisa utamaduni Manispaa ya Irina (wa pili kulia) na viongozi wa  Ebony Fm wakipata chakula

Mtangazaji Edwin Bashir (kulia) akiwa na DJ Muba
 Wana Ebony FM wakitoa misaada hospitali
Wana Ebony wakifanya usafi soko kuu la Iringa


Picha na habari na Francis Godwin
Afisa utamaduni wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Daniel Kadindi amesifu jitihada mbali mbali zinazofanywa na kituo cha Radio Ebony Fm katika kutimiza nguzo kuu tatu za tasnia ya habari.
Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho mkoa wa Iringa umeendelea kujulikana zaidi na wananchi wake kuendelea kupata mambo mapya ambayo yamekuwa yakitolewa na timu ya wanahabari wa kituo hicho kwa kuzingatia misingi na maadili ya taaluma ya habari nchini na kutaka kituo hicho kuendelea kukaza buti zaidi kwani hadi sasa kwa nyanda za juu kusini ni kituo pekee kinachoongoza kwa kuwafikia vema wananchi wake .
Kadinde alisema kuwa moja kati ya mambo ambayo yamekuwa yakifanywa na Radio Ebony Fm ni changamoto kubwa kwa vituo vingine vya radio ndani ya mkoa wa Iringakuiga na kufanya mambo hayo vinginevyo vitaendelea kubaki nyuma.
“Nataka kuwahakikishieni bado wasikilizaji na viongozi wa mkoa wa Iringa wanatambua kuwa radio pekee ndani ya Iringa ni Radio Ebony Fm …..japo zipo nyingi ambazo sipendi kuzitaja majina ila nasema baba ni baba hawezi kuwa mama Ebony Fm mnachapa kazi lazima tuseme ukweli”
Pamoja na sifa hizo bado aliwataka watangazaji kutobweteka na kusema sasa ndani ya mkoa wa Iringa radio inayokuja kwa kasi zaidi na kufuata nyayo za Ebony ni Overcomes Fm pekee japo pia bado haijaweza kuufikia umaarufu wa Radio Ebony FM .
Aidha Kadinde aliwataka wanahabari wa kituo hicho ambao wamekuwa wakifanyavema kuwa ni pamoja na George Ndamagoyo,Bahati Alex, Athumani Mwalubadu, Raymond Francis , Edwini Bashir,Hatya Omary,Bony Zachalia, Mareges Gilshon,Grolia, Agnes Andason,Alen Philipo,Imanuel a.k.a Mtoto wa Mungu bilakuwasahau ma DJ wawili wa kituo hicho DJ Muba na DJ Kwasa ambao wamekuwa ni moto mkali kwa Ma DJ mkoani Iringa na mikoa ya nyanda za juu kusini kama si Tanzania kwa ujumla.
Pia alipongeza safu ya uongozi wa Radio hiyo chini ya mkurugenzi wake mzawa wa mkoa wa Iringa Evaristo Mfugali ambaye amekuwa mmoja kati ya waajiri wakubwa wa vyombo vya habari mkoa wa Iringa kwa kutoa ajira kwa wafanyakazi zaidi ya 40 .
Katika hatua nyingine Kadinde amepongeza jitihada nzuri za meneja wa kituo hicho ambaye ni mganda pamoja na wasaidizi wake akwemo Cosmasi , Hostine na wengine kwa kujipanga vema.
Kuhusu baadhi ya vipindi kama zile vya kijamii ,habari na burudani mbali mbali yakiwemo matamasha ya Mitikisiko alisema matamasha hayo yamekuwa ni tishio katika mkoa na kuwa umati ambao huwa unajazwa uwanja wa Samora hakuna kiongozi aliyepata kufikia idadi hiyo zaidi ya hayati baba wa Taifa alipofanya ziara yake miaka ya 70 katika mji wa Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2011

    Picha mbaya kuliko maelezo. Hiyo kamera ya mchina nini??????? Au mpiga picha ni wale waandishi wa mitaani????

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2011

    Kaka nilivyoona hizi picha nikajua ni za miaka ya 90!! Ndugu yako kama Camera imechoka fanya harammbee ununue nyingine.
    Asante kwa taarifa na Hongera Ebony FM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...