| Katibu wa Itikaddi na Uendezi CCM, Nape Nnauye |
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
KATIBU wa Itikaddi na Uendezi CCM, Nape Nnauye amesema madai ya viongozi wa Chadema kutaka posho za watumishi wa serika na wabunge zifutwe ni unafiki na ajenda ya kusaka umaarufu wa kisiasa lakini siyo hoja inayotoka katika dhati ya mioyo yao.
Akizungumza kwaa njia ya simu, jana, Nape alisema, viongozi hao wa Chadema wangekuwa na dhamira za dhati kutaka posho hizo zifutwe wangefuata taratibu zinazojulikana ambazo ni za uhakika badala ya kumwandikia spika barua na kuzungumzia swala hilo barabarani.
Nape alisema, kwa kuwa utaratibu huo wa posho uliwekwa kisheria baada ya kupitishwa na bunge, viongozi hao wa Chadema kama wangekuwa wa kweli kutaka posho hizo zifutwe wangepeleka hoja hiyo bungeni kwa kuwa inazungumzika.
"Badala ya kuzungumzia barabarani kuhusu jambo hili ambalo linazungumzika, kama kweli wana nia hiyo na si vinginevyo wapeleke hoja binafsi bungeni ambako ndiko sheria hutungwa" alisema Nape.
"Kimsingi sina tatizo na hoja kwa sababu wana haki kuitoa, lakini nina mashaka na dhamira yao hasa njia wanayotumia kuijadili hoja hii" alisema
Alionyesha kumshangaa, Mwenyekiti wa Chadema , Freean Mbowe kuweweseka na utaratibu huo wa posho ili hali ulipitishwa kisheria kwa kujadiliwa na wabunge katika bunge ambalo na wabunge hao wa upinzani walikuwemo.
Kuhusu hoja ya Mbowe kwamba posho za watumishi wa serikali zingefutwa zingeweza kupatikana sh. bilioni 900 kwa mwaka, Nape alisema,watumishi wa serikali kama polisi, walimu, na wataalam mbalimbali wanapoajiriwa kwa ajira mpya hupewa nauli na posho za kujikimu kuwawezesha kufika vituo vya kazi. "je, ikiwa utaratibu huo wa posho utafutwa kabisa kama wanavyodai, wafanyakazi hawa watakuwa wanafika vipi kwenye vituo vyao vya kazi ?" alihoji Nape.
Nape alisema, suala la msingi ni kwamba serikali ifute posho zisizo za lazima kwa kuwa haiwezekani kufuta hata zile za muhimu, na kutaka suala hilo lijadiliwe kwa kuzingatia uhalisia wake siyo kwa mlengo wa kisiasa.
"Hata hivyo waziri wa fedha ameshasema serikali itafuta posho zisizokuwa za lazima, lakini huwezi futa posho zote" alisisitiza Nape na kuwataka wananchi kuwa makini na ghiliba za kisiasa zenye lengo la kutafuta umaarufu kisiasa badala yake wapime kila hoja.
"Na kwa Chadema hii ni kama kawaida yao, wanapoona hawana hoja za msingi, hukimbilia kuzusha mambo ambayo hata wao huwa hawayaamini,mfano ni wakati Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa alipokuwa mbunge alizusha hoja kwamba anaumizwa na mshahara wa wabunge wa sh. milioni 6, kwamba ni mkubwa mno kulingana na hali za vipato vya Watanzania walio wengi.
Baada ya kutamba na hoja hiyo kiasi cha baadhi ya wananchi kudhanianakerwa na hali hiyo,sasa yeye mwenyewe amedai na kupata malipo ya Sh. milioni 7 kila mwezi kutoka Chaadema huku wafanyakazi wengine wa chama hicho wakipata malipo yasiyofikia hata robo ya kiasi hicho.
" Mheshimiwa Mbowe akatoka hadharani kumtetea Dr. Slaa kuwa eti malipo ya 7.5 milioni kwa mwezi ni posho tu isiyostahili kulipiwa kodi,leo wanadai kuona uchungu kwa posho za wengine!! Narudia sina tatizo na hoja ila ninatatizo na dhamira yao" alimalizia Nape.


Wamezungumzia Posho za allowance anazolipwa Mbunge anapohudhuria kazini wakati ni wajibu wake, Kama mkitaka ziendelee basi na walimu walipwe wanapohudhuria darasani. Tatizo viongozi wetu wamekuwa wabinafsi sana. Sasa na sisi tumeanza kuamka na punde tutafika kwenye hiyo mishahara yenu.. Na nashukuru sana Kwa Zitto kuandika barua nyingine akikataa Posho zao hata kuziweka kwa Organization ya Kigoma
ReplyDeleteNape inabidi utumie kichwa na akili kufikiri. Unaropoka mno. wenzako wameongelea posho zote sio wabunge tu. Na hapa ni swala la mfumo sio eti CDM wakizikataa inatasaidia. Tunataka wote wenye kupokea posho na mkishahara ikome au wote tupewe posho kuanzia wafagizi mpaka Raisi.
ReplyDeletesikunalianne na wewe nape.......posho ya kuwapeleka waalimu sehemu walzipongiwa huziwezi kuziita POSHO
ReplyDeleteNape unadandia hoja ambayo huielewi. Kinachozungumzwa na wabunge wa Chadema sio posho za kujikimu (perdiems) na nauli, bali ni posho za vikao wakati mbunge au mtumishi anapokuwa anatekeleza majukumu yake. Wewe nenda kaendelee na kujivua gamba, haya huyawezi.
ReplyDeleteNina mashaka makubwa na dhamira za wachangia hoja wote hapo juu kama ambavyo Nape ana mashaka na dhamira za Chadema. Chadema, endeleeni kushabikia hiyo hoja mkione cha moto, mwulizeni mwenzenu JK kuhusu hoja ya wafanyakazi mwaka jana. Nape yuko sahihi 100%. Hakika nimeanza kukosa 'Love at first sight' kwa CHADEMA ikilinganisha na nilivyokuwa naiona mwaka jana, nahisi nyota nyenu inafubaa kwa hoja zizizotoka moyoni na zisizo na mshiko.
ReplyDeleteNape mtayavua magamba mpaka mchoke.tumeuchoka uccm ccm mnaojali matumbo tu bila kujali wananchi wenu wanaokufa kwa njaa huku neema ikichotwa na wachache.
ReplyDeletetatizo la wanasiasa ni siasa. na tatizo la tanzania ni chama cha siasa, tena ccm. hata watu waliokuwa wanaonekana wana busara wakiingia kwenye ccm busara zao huwaruka pia. nape alikuwa akionekana mwenye busara, lkn tangu aingie kwenye madaraka ya ccm, busara zote zimemruka. hivi kuna tatizo gani kwa chama tawala kukubaliana na hoja nzuri inayotoka upinzani?
ReplyDeletesuala la posho linalozungumziwa na chadema halihusiani na posho za kujikimu (subsistence allowances) ambazo ni stahili ya mfanyakazi yeyote yule anapokuwa nje ya kituo chake cha kazi. chadema wanazungumzia posho wanazolipana wakubwa wakiwa wamekaa kwenye viti vyao maofisini. tena pesa zenyewe ni nyingi. umezuka mchezo serikalini na kwenye mashirika ambapo watumishi wanaandaa vikao kisha wanaandaa posho wakiwajumuisha wakubwa wao ambao wala hawahudhurii vikao hivyo.
waziri mkullo anatamba kuwa wamefuta kodi kwenye posho za wafanyakazi, hivi mwalimu, nesi, askari polisi anapata posho zipi hadi atarajie ahueni inayotokana na ufutaji wa kodi hiyo? hizi ni ghiliba za ccm. watu walikuwa wakilalamikia kodi kubwa zinazotozwa kwenye mishahara na si posho. wapunguze kodi kwenye mishahara (paye) ili watumishi wanufaike na mihashahara tofauti na leo ambapo serikali natoa kwa mkono wa kulia na kuchukua kwa mkono wa kushoto. wizi mtupu!
aisee Nape!! kumbe ndo hali halisi ya serikali. mimi ni askari. nilipoanza kazi sikupewa hizo posho. sikujua ilipokwenda na hiyo ndo hali halisi ya serikali yetu ya ccm. jamani kweli bado mnatetea hii mada. posho ya kikao wakati ni kazi yako. yaani hatuwezi kuwaelewa. Nape acha kabisa mambo ya siasa siasa, naona ulichotaka kusema ni posho ya Slaaa. kwa nini bado mnatuona wananchi kama watoto wa kudanganywa dangaywa tu. just be a bit serious.
ReplyDeleteAFADHALI UBAKI HUKO HUKO CCM MAANA SIASA ZAKO ZISINGETUSAIDIA CCJ. SARATANI YA MASLAHI.
ReplyDeleteNape punguza kuropoka jipange sababu unajidhalilisha. Kiukweli mi nimeona mantiki ya Zitto kwenye hoja yake kwani kihalisia kazi ya Mbunge ni nini? Bila kuingia ndani zaidi Mbunge ni mwakilishi wa wananchi ambapo inampasa kuwasikiliza na kujua shida za wananchi wa jimbo lake,ili ziweze kurekebishwa.Uwakilishi huu hufanyika pia kwa yeye kuhudhuria vikao vya Bunge sasa hii ni sehemu ya kazi yao ambapo mwisho wa mwezi hulipwa mshahara. Hapa Zitto alijaribu kutofautisha vikao vya bodi na vikao vya Bunge. Wanabodi hawalipwi mishahara bali posho ya vikao,sasa wabunge posho ya vikao ya nini wakati analipwa mshahara we Nape hilo hujaliona badala yake unaleta unafiki wa kisiasa. Huoni kwamba nchi yako inaupungufu wa zaidi ya trilioni 6 kwenye bajeti yake sasa watu wanasaidia serikali namna ya kupunguza gharama kwa faida ya nchi wewe unakurupuka na kujibu hoja wa faida ya chama. Huu ni unafiki kwa Taifa
ReplyDeleteWote mliotoa maoni hapo juu, hamgusii issue mbona??? Issue ni POSHO ZA VIKAO ZA WAH. WABUNGE NA WAFANYAKAZI WA SERIKALI: Posho za vikao zipo kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.Pili Hakuna cha Zitto mwenyewe wala Mbowe wataweza kuzikataa hizo posho kwa kuwa ni stahili zao kwa mujibu wa sheria, na wengine huwa wanataka hata kulia wasiposaini hizo posho. Mtu ambaye amewahi kusainishwa posho na aseme hapa kama kweli hizi posho sio tamu. Kama Zitto amechoka kusaini, ni vema asaini halafu zielekezwe jimboni kwake kama alivyoshauriwa, hakuna atakayepinga. Ila issue ni kwamba hakuna asiyependa posho ya vikao hata mmoja...Zitto anataka tu kufanya siasa ili Chadema waonekane safi kwa ajili ya kushinda urais 2015, wananchi msidanganyike na siasa za kihuni, basi kama tunaweza kupata kiongozi safi na mwenye moyo wa kujitolea basi hiyo ni HEKO Tanzania, ila mimi naona huu ni wizi mtupu. Kuhusu kufutwa posho,mnaelewa wafanyakazi wa serikali wanalipwa viwango vidogo vya mishahara pamoja na kukatwa kodi, mtu analipwa laki tatu akitoa makato yote anajikuta anapata laki 2, hapo ana bonge la familia ukizingatia na familia zetu za extended Tanzania (ujamaa) yaani aibu hata kusimulia kuwa eti wewe ni mfanyakazi wa serikali..maana wiki moja tu mshahara umeshaondoka. Nadhani hapo point hao wabunge ambao wana mishahara mikubwa kuliko kawaida ndio wapunguziwe posho za vikao wanazosaini, na mmesikia kuwa kila vikao wanaohudhuiria lazima wasaini, na ni vikao hata 3 au 4 kwa siku, can you imagine?, ila watumishi wa serikali, vikao vyenyewe hutokea kwa nadra labda mara moja kwa miezi 4, na posho yenyewe ni kiduchu ukilinganisha na ya mhe. mbunge. Naona bora ngazi za watendaji ziachwe zisiguswe kabisa maana watendaji ndio wanaowezesha shughuli za serikali kufanikiwa. Hao wahe.wabunge kazi yao ni vikao tu na safari...Huyo Nape ndo hakuelewa kabisa kilichoongelewa, na sidhani kama anafuatilia magazeti na mijadala vizuri, tumsamehe tu maana hajui aongealo.
ReplyDeleteIts complex kwa kweli Rugaibamu
ReplyDeletemmmmmhh zito anatafuta umaarufu tu..chademmma wanafiki ...nahisi nimeanza kutokuwa na imani nao tena...maana hoja zao hazina maana
ReplyDeleteposho iliyo zungumziwa hapo ni ile ya vikao Sitting allowance na si vinginevyo..hoja hii kama itajadiliwa kwa kimya kimya wengi wata ikataaa maana si waadilifu wa kweli but ikiwekwa wazi kama hivi ilivyo kila mmoja anakuwa anaona aibu na dhamira yake kumsuta
ReplyDelete