Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Mustafa Haidi Mkulo akiwasili Bungeni jioni mjini Dodoma jioni hii tayari  kutoa hotuba ya bajeti ya mwaka 2011/2012


Mheshimiwa Spika, 
naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012. Pamoja na hotuba hii, vipo vitabu vinne vinavyoelezea kwa kina takwimu mbalimbali za Bajeti. Kitabu cha Kwanza kinahusu makisio ya mapato. Kitabu cha Pili kinaelezea makisio ya matumizi ya kawaida kwa Wizara na Idara zinazojitegemea ambapo cha Tatu kinahusu makisio ya matumizi ya kawaida kwa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na cha Nne kinaelezea makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2011 ambao ni sehemu ya Bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa tena kuongoza kwa muhula wa pili wa Serikali ya Awamu ya Nne. Aidha, ninamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyonayo kwangu kwa kunichagua kwa mara nyingine tena kuongoza Wizara kubwa na nyeti, ninamuahidi kuwa sitamuangusha.  Pia ninampongeza Dkt. Mohammed Gharib Billal kwa kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  Vile vile, ninampongeza Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge na kuteuliwa tena na hatimaye kupitishwa na Waheshimiwa Wabunge kuwa Waziri Mkuu kwa muhula wa pili wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe binafsi Mhe. Spika Anne Makinda (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Spika na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza Bunge katika Afrika Mashariki. Kuchaguliwa kwako kunatokana na imani kubwa waliyonayo Waheshimiwa Wabunge kwa kuzingatia busara zako, uwezo na uzoefu wako ndani ya Bunge hili. Napenda pia kumpongeza Mhe. Job Ndugai (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika. Nawapongeza pia mawaziri wenzangu wote pamoja na Naibu mawaziri wote, kwa kuteuliwa kwao na Mhe. Rais kushika nyadhifa hizo. Aidha, napenda niwapongeze wabunge wote kwa kuchaguliwa na kuteuliwa kuingia katika Bunge hili.

Mheshimiwa Spika, naomba pia nichukue fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha matayarisho ya Bajeti hii. Maandalizi ya Bajeti ya Serikali yanahusisha wadau na vyombo mbalimbali. Kipekee ninaishukuru Kamati ya Fedha na Uchumi chini ya uenyekiti wa Mhe. Dkt. Abdallah Omari Kigoda, Mbunge wa Handeni, pamoja na kamati nyingine za kisekta kwa ushauri mzuri waliotoa wakati wakichambua mapendekezo ya Bajeti hii. 

Kwa hotuba kamili 
kwa Kiswahili na Kiingereza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2011

    Michuzi samahani naomba uniwekee swali langu hapa najua WACHUMI watakuja Kusoma:Mimi nafanya kazi nje ya nchi,mshahara wangu unatumwa Tanzania kupitia benki(akaunti yangu iko TZ) lakini kodi(PAYE) nalipia hapa kwenye nchi ninakofanya kazi.Nataka kujua kama na mimi nachangia kwenye uchumi wa nchi yetu au la?Kama jibu ni ndiyo..ni kwa vipi.Tafadhali

    David V.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2011

    swali zuri sana David ni kweli unachangia uchumi wa nchi kwa kuwa huo mshahara wako unaoingizwa ktk akaunti yako ya TZ the moment unapotumwa tu benki ya Tanzania inakata "remitance" ambayo mwisho wa siku benki hiyo inakuja kuilipa serikali kiasi fulani kama kodi ya benki. hii inaaply pia hata kama ungekuwa unamatumia mtu yeyote hela bongo kuingiza ktk akaunti yake. anakatwa remitance kama kawaida. nakosa neno la kiswahili la "remitance" wadau watasaidia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2011

    Jamani tuwaombe wabunge warudishe magari ya serikali na yauzwe yote,na pesa tupate pesa za madawati,vitanda vya hospitali ,vitabu,maji na umeme.
    wao wanao uwezo wa kujinunulia au kuagizia magari yao,now iwe na wao wanalipa fadhila maana wengi wao wamesomeshwa na serikali mpaka hapo walipo ila leo wamesahau kuwa still kuna watoto wanataka kusoma ila hawana uwezo na shule za serikali hazina madawati na vitabu.
    Nchi za wenzetu elimu ya chini ni bure na ni lazima kwa watoto wote,na mzazi unashitakiwa kama hujampeleka mtoto shule.
    Bajeti iwe na priority na goals zenye maana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2011

    Na pia hata hiyo pesa unayotuma kuweka kwenye account yako, ndio Benki nayo inaizungusha kwa wateja na kupata faida, na kuilipia kodi hiyo faida pia. Kwa hiyo unachangia uchumi wa TZ pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...