Je wajua kwamba stelingi mkali wa sinema huko Hollywood Angelina Jolie (kulia) ni binti wa nyota wa sinema mkongwe Jon Voights (kushoto)? Basi habari ndiyo hiyo, ila Angelina na baba yake haziivi baada ya mzee mzima kumjia juu kuhusiana na mahusiano yake na wanaume tofauti. Kabla ya kuanza libeneke na mista wake wa sasa Brad Pitt, Angelina alishawahi kuolewa mara mbili katika ndoa ambazo hazikudumu.
Mengi zaidi kuhusu Angelina BOFYA HAPA
Mengi zaidi kuhusu Angelina BOFYA HAPA
-------------------------------
Huu ndio mwanzo wa mlolongo wa makali fupi za 'JE WAJUA?' ambazo Globu ya Jamii itakuwa inakuletea mara kwa mara katika mstakabali wa kuendeleza libeneke. Mawazo na maoni yanakaribishwa ili mambo yawe mswano - Masharti na vigezo kuzingatiwa....
-Michuzi
-Michuzi
nashukuru Globu ya jamii ila kuna mambo mengi hapa Tanzania sijui...naomba tuanzie nyumbani.
ReplyDeleteNawasilisha.
Sasa wewe michuzi....Brad Pitt alimuoa lini Angelina??!! au Uliwapiga ya mkeka bila jamii kujua?!!
ReplyDeleteKama nakumbuka vizuri walisema hawataoana mpaka....mpaka wa mlango wa pili nao wawe huru kuoana......angalia vyanzo vyako urekebishe na ututake radhi ...kama nikosea mimi natanguliza samahani...chonde kaka ila sidhani kukosea mie!!!
Mzawa
hawajaoana na brad pitt zaidi ya kuzaa watoto na wengine wakuadopt uwe unachunguz kwanza mabo kabla ya kuleta ishu humu, na kisa cha kutoongea na babake ni kwa vile alimuacha mamake akaapa kutomsamehe mdingi na kwa hasira hatumii jina la dingi wake akajiwekea jolie
ReplyDeleteNeno stelingi limepitiwa na wakati!!
ReplyDeleteso what? kuna mambo mengi mno ambayo ni muhimu kwa mtanzania na ambayo yatamsaidia kwa maisha yake ya mbeleni hukuyaona ila umeona uanze na ya ughaibuni? Watanzania tutaacha lini kuona kila kilicho cha mzungu ndio bora?
ReplyDeleteMie nakubaliana na Wa Kwanza tufanye ya nyumbani na viongozi wetu wa zamani kuhusu je wajuwa? hizi za kina Angelina hazitotusaidia saaana wengi na uhakika wanalijuwa kuhusu Angelina na mzee wa Anaconda. tuwe tuna ongelea Tanzania na Bara la Africa kidogo alafu ndio tutoke nje. MZ
ReplyDeletehuyu binti ni homewrecker, tena ndoa zake zote yeye anajua, kama mnataka kujua fatilien.
ReplyDeletenawe michuzi tukuulize jee unajua unachokiandika?
ReplyDeletejamani michuzi hakukosea kwani kujuwa habari tofauti si mbaya jamani namuombea kwa ilo hii ni blog ya jamii kuna watu wengine wapo nje ya nchi na wanaangalia hii blog na hata mambo ya tanzania wanaangalia
ReplyDeletemi naona si vibaya hii ni blog ya wote ndani na nje ya nchi kujuwa kulikoni
ni maoni yangu tu
JAMANI MSIMSHAMBULIE MZEE WA LIBENEKE MAMBO YENYEWE YANAKUJA HII NI ONTEST HALO HALO HALO TUNAJARIBU KWAHIYO KWENYE KUJARIBU HATA MTU AKICHAPIA HAKUNA KOSA .....JE WAJUA? HALO HALO TUNAJARIBU HAYA NGOJA TUKULETEENI ZA NYUMBANI.
ReplyDeleteJE WAJUA?
yule mshiriki mwingine wa big brother kutoka Tanzania wa kuitwa BHOKE alikula CHAKULA CHA USIKU NA ERNEST WA UGANDA usiku wa kuamkia jumapili siku ambayo jioni yake aliaga mashindano.
HALO HALO TUNAJARIBU FANYENI SUBRA WADAU HALO HALO TUNAJARIBU JE WAJUA?
JE WAJUA?
TUNAJARIBU
JE WAJUA?
Wewe acha porojo, Angelina hajawai kuolewa zaidi ya mara moja. Baada kuachana na mumewe Bob Thornton mcheza movies aliyemla Halle Berry kwenye movie Monster Ball ndio akazoana na Brad Pitt.
ReplyDeleteNa uhasama na baba yake zamani hakuwa juu ya Angelina kuwa na wanaume, kwani Angelina hana sifa ya kuwa alitembea na wanaume wengi. Chanzo anasimulia Angelina kuwa Baba yake alikuwa hamjali marehemu mama yake ambaye alimuacha, Angelina na kaka yake walilewa na mama yao, wakati mdingi akila maisha na vimada wake. Kwahiyo Angelina hakusahau na kuamua kumlia ngumu mdingi kwani nafikiri hata mama yake alipougua na kufa mdingi hakujari hivyo licha ya kuwa walikwisha achana.
Kama uko hapa Marekani tuliona huyo mdingi ndiye alikuwa akimuomba radhi Angelina kwenye ma-TV amsamehe, wawe na uhusiano ili aweze kuwa karibu na wajukuu zake. Angelina akamsamehe sasa wako poa kama familia na anacheza na wajukuu zake.
Acheni kuandika habari za kupotosha kabla hamja check ukweli wa habari.
Mdau, US.