Hapana shaka umeshawahi kujiuliza neno ‘Kata’ limeibukia wapi hata kukawa na Katibu Kata ama Kata ya sehemu fulani, mfano Kata ya Kijitonyama, ikimaanisha mojawapo ya ngazi ya chini katika serikali za mitaa.
Utafiti wetu umebaini kwamba jina hilo linatokana na aliyekuwa Jaji Mkuu wa kwanza wa Tanganyika, Sir William Carter, aliyeshika wadhifa huo toka mwaka 1920 hadi 1924, akifanyia kazi zake jijini Dar es salaam. Hivyo, akiwa ndiye Jaji Mkuu wa kwanza, jina lake likavuma kila pembe ya nchi ambapo wenyeji walilitamka Kimatumbi, yaani Jaji Kata.
Hivyo umaarufu wa Jaji Kata ukapelekea hata wale viongozi wa ngazi za serikali za mitaa, ukitoka kwa mjumbe wa nyumba kumi kumi, unafuata ngazi ya Bwana Kata, yaani jina la Jaji Carter likawa kama kiashirio cha cheo cha kutoa maamuzi katika ngazi za chini za utawala. Baadaye himaya ya Bwana Kata ikaja kujulikana kama ‘Kata’ ambapo baadaye zaidi kiongozi akawa Katibu Kata pamoja na Mwenyekiti wa Kata.
| Jaji Mkuu Mstaafu Mh. Augustino Ramadhani akiwa na wapiganaji siku aliyoapishwa rasmi kuwa Jaji Mkuu mwaka 2007 |
Historia ya cheo hicho cha Jaji Mkuu nchini Tanzania, ambayo imeweza kutoa jina la uongozi katika ngazi ya serikali za mitaa, inaanzia baada ya Vita Kuu ya kwanza, wakati Tanganyika iliyokuwa koloni la Ujerumani, ilipochukuliwa na kuwekwa chini ya hiamaya ya Uingereza mwaka 1919. Mwaka mmoja baadaye nafasi ya Jaji Mkuu ikaundwa.
Tanganyika ilipata Uhuru wake mwaka 1961 na baada ya mwaka ikawa Jamhuri. Mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nchi ikabadili jina na kuitwa Tanzania. Pamoja na kuungana huko, Bara na Visiwani zilikuwa na mfumo wake wa Mahakama, yaani kila upande una Jaji Mkuu wake hadi leo. Mahakama ya Rufani, ambayo ina mamlaka ya juu katika sheria nchini kote, ilizinduliwa mwaka 1979.
![]() |
| Jaji Mkuu Mh. Mohamed Chande Othman |
Majaji wakuu wa Tanganyika
1920–1924: Sir William Morris Carter
1924–1929: William Alison Russell
1929–1936: Joseph Alfred Sheridan
1934–1936: Sidney Solomon Abrahams
1936–1939: Llewelyn Chisholm Dalton
1939–1945: Ambrose Henry Webb
1945–1951: Sir George Graham Paul
1951–1955: Sir Herbert Charles Fahie Cox
1955–1960: Edward John Davies
1960–1964: Ralph Windham
Majaji wakuu wa Tanzania
1964–1965: Ralph Windham [17]
1965–1971: Philip Telford Georges
1971–1977: Augustine Saidi
1977–2000: Francis Lucas Nyalali
2000–2007: Barnabas A. Samatta
2007–2011: Augustino Ramadhani
2011 – Hadi sasa: Mohamed Chande Othman



Salaam ndugu Michuzi na ndugu mtoa mada wa Jee Wajua. Mimi kwa utafiti wangu neno "kata" halina asili ya jina la mtu anayeitwa Carter.Nakubaliana na huo mchango wa huyo jamaa lakini neno hili "kata" lina asili ya Kiarabu kama yalivyo maneno mengi ya Kiswahili. Katika Kiarabu kuna neno "qataa" likiwa na maana ya 'cut up, divide au cut to pieces". Pia kuna neno jengine la kiarabu "muqataa" au nadhani kuna waswahili wanalisikia neno makataa. Neno "muqataa" au "mukataa" kwa kiarabu lina maana ya region, district , province na sisi waswahili tunalitumia kama "ward". Kwahiyo nafikiri hii ndio asili ya neno "kata". Mtu anaetaka zaidi basi aangalie Kamusi aliyoitoa Ustadh Ibrahim Bosha "The Influence of Arabic Language on Kiswahili with a Triliangual Dictionary (Swahili-Arabic-English.
ReplyDeleteNasubiri wachangiaji zaidi.
A. Mazrui
Naam,
ReplyDeleteMtoa habari hii ametupunja kidogo kwa kukosa kutueleza chanzo cha habari yake. Namuomba arudi atupe chanzo cha habari yake kama vile alivyofanya Ndugu A. Mazrui.
Shime wanaisimu na wanahistoria tunawasubiri mtupe uhondo wa chanzo cha KATA.
Salaam ndugu michuzi, hivi ss Tanzania ndio tuko nyuma au inakuaje maana mpka naandika comment hii ni kua wikipedia wameandika kua Jaji AUgustine Ramadhan ndie jaji mkuu imekaaje hii...
ReplyDeletePorojo zimeanza, mmeshiba sana. tumuombe mh. kikwete apunguze shibe hilo waswahili bwana!!!!
ReplyDeleteHAYA NDIO TUNAYATAKA KWENYE JE WAJUA? INGEKUWA WAMEWEKWA MA STAR WA NJE UNGEONA COMMENT KIBAO... JE WAJUWA MELI(JAHAZI) IMETOKANA NA NENO GANI? WASWHAILI TUNAITA MELI ZAMANI ENZI ZA UKOLONI WATUMWA WALIKUWA WAKIFANYA KAZI KWENYE MFUKWE WA PWANI SASA WAZUNGU WAKILETEWA MAIL(BARUA) KUTOKA NJE KWA NJIA YA JAHAZI SASA WAZUNGU WAKIZIONA WANAJUWA BARUA ZAO ZINAKUJA WANAANZA KELELE MAIL<MAIL,MAIL KWAKUMAANISHA BARUA ZAO. BASI NDUGU ZANGU PIA WAKAWA KELELE MELI MELI MELI TOKA SIKU HIYO TUKAIITA MELI.
ReplyDelete