Asili ya Saluti ya askari

Kamanda wa polisi Dar es salaam mstaafu
Afande alfred Tibaigana akipiga saluti
Hadi sasa hakuna ajuaye kwa uhakika chanzo cha kupiga saluti. Maandiko yanasema, toka zama za kale kwenye historia za majeshi ya ulinzi, mkono wa kulia (ama mkoni wa silaha) ulikuwa unanyooshwa juu kama alama la kuamkia kirafiki, ikimaanisha huna silaha mkononi na mambo ni mswano, pita zako. Utaratibu ulikuwa kwamba mwenye cheo cha chini ndiye aanze kunyoosha mkono. Bila shaka hii imechangia kuhalalisha saluti yetu hii ya sasa.

Maandiko ya awali yanatanabahisha kwamba saluti ya askari wa leo imetokana na askari wa zamani enzi hizo, kunyanyua mfuniko wa kofia yake ya deraya ya chuma  kama alama ya kujitambulisha mbele ya afande wake.

Inaelezwa pia kwamba aina ya saluti zilitofautiana kwa njia tofauti kwa kadri miongo ilivyopita. Inasemekana kuna wakati saluti ilipigwa kwa mikono yote miwili! Katika mapicha ya zama hizo kumeonekana hata kupigwa saluti kwa mkono wa kushoto.
Kuna maandiko yanayoeleza kile kinachosadikiwa nin dhana ya karibu kuliko zote ya asili ya saluti. Nayo imetokea katika majeshi ya Uingereza ambao inasemekana askari wa cheo cha chini alilazimika kuvua kofia anapomsalimia afande. Ila kutokana na mabadiliko ya muundo wa kofia katika karne za 18 na 19, mtindo wa kuvua kofia mbele ya afande ukabadilishwa na kugusa sehemu ya mbele ya kofia (visor) na kunyenyekea. Baada ya hapo ikabadilika taratibu na kuzuka saluti hii ya leo. 


Kwa askari wanamaji, taratibu ni kwamba saluti hupigwa kwa kuwika mkono kifuani huku kiganja kikiangalia chini, bila shaka kwa kuwa mara nyingi wanamaji mikono yao huwa michafu kila mara kwa kazi za melini. Vile vile  kiongozi wa Ujerumani Adolf Hitler alibuni aina yake ya saluti ambapo askari wake walikuwa wakinyoosha mkono mbele kwa ukakamavu huku wakitamka 'Heir Hitler' saluti ambayo kwa sasa haipo tena

Tangia awali ya 1745 amri katika kitabu cha kanuni katika jeshi la Uingereza iliweka bayana kuwa ‘Askari anaamrishwa asivue kofia wanapopishana na afande, ama wanapoongea naye, ila kuinua mkono hadi karibu na kofia na kuinama wakati husika”. Pia kukauka huku mikono imebanwa ubavuni kwa asiyevaa kofia ama sare.
Hata hivyo maelezo yoyote yatayopatikana jawabu lake la mwisho ni kwamba saluti ni aina ya kitendo cha kuonesha HESHIMA mbele ya afande aliyekuzidi cheo, na kwamba kwa askari yeyote hiyo ni jukumu na haki yake.

PS: Globu ya Jamii inakukaribisha mdau ulie na data ama stori aina hizi ili kuendeleza libeneke hili la JE WAJUA? Zitume kwetu kupitia issamichuzi.blogspot.com nasi baada ya kuzihakiki tutazichapisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...