Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Member akimpokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mama Hillary Clinton muda mchache uliopita jioni hii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Mama Clinton, ambaye katokea Zambia kabla ya kuja hapa, yuko nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu, ambapo kwa mujibu wa ratiba kesho atakuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na mawaziri, kabla hajaenda Kibaha kuzindua mpango wa chakula. Mchana huo huo kesho atatembelea mtambo wa kuzalisha umeme wa Symbion Power Ubungo kabla ya kuelekea Buguruni kutembelea kituo cha afya, kabla ya kukutana na Rais Kikwete jioni na kufanya naye mkutano na wanahabari Ikulu, Dar.



angekuja raisi wa michezo wa China JK angekwenda kumpokea, sasa kwa nini JK ameshindwa kwenda kumpokea Hillary?
ReplyDeleteJibu la mchangiaji "Kilo" hapo juu. Si lazima kila unachoona uchangie / ukosoe. Kuchangia si lazima. Kama huna point kaa kimya....Mtu huna point unaandika tu tena kwa "bold"...
ReplyDeleteJamani sio lazima rais ampokee clinton.haata hivyo jk ana mambo mengi huyu sio rais amepewa heshima kwa kupokelewa na mwenzake.wa fani moja.jamani tujaribu kuendelea.ulishaona wageni wote wa marekani wanapokelewa na obama.acha hizo wee .kua
ReplyDeleteJk yuko South Afrika
ReplyDeleteJob Title: International Broadcaster (Swahili)
ReplyDeleteAgency: Broadcasting Board of Governors
Job Announcement Number: DEU-11-96
SALARY RANGE:
$74,872.00 - $97,333.00 /year
OPEN PERIOD:
Thursday, June 09, 2011 to Thursday, June 16, 2011
SERIES & GRADE:
GS-1001-12
POSITION INFORMATION:
Full Time Career/Career Conditional
PROMOTION POTENTIAL:
12
DUTY LOCATIONS:
1 vacancy - Washington DC Metro Area, DC
WHO MAY BE CONSIDERED:
United States Citizens
JOB SUMMARY:
This position is located in the Africa Division, Swahili Service of the Voice of America in Washington, DC. The incumbent will serve as an International Broadcaster with responsibility for conceiving, planning, researching, writing and broadcasting original audio/video scripts of a highly complex nature and for providing Internet content for the website.
This position is covered by an union agreement.
The Broadcasting Board of Governors is conveniently located within walking distance to the Blue, Orange, Yellow and Green Metro lines.
Introduction to Agency: The Broadcasting Board of Governors (BBG), an independent federal agency, is an exciting, multicultural organization that encompasses all U.S. civilian international broadcasting. The BBG is comprised of the Voice of America, which delivers high quality, multimedia programming in 44 languages to audiences worldwide; the Office of Cuba Broadcasting (Radio and TV Marti); the International Broadcasting Bureau, which provides transmission, administrative, and other support services; and three grantee organizations - Radio Free Europe/Radio Liberty; the Middle East Broadcasting Networks (Alhurra TV and Radio Sawa), and Radio Free Asia. Our staff of dedicated professionals serves as an example of a free and independent media, reaching a worldwide audience with news, information, and relevant discussions.
This vacancy is being advertised under delegated examining procedures and is open to all U.S. citizens.
The Full Performance Level: 12
KEY REQUIREMENTS:
U.S. Citizenship
Candidates MUST complete the Online Questionnaire.
Relocation expenses WILL NOT be paid.
Selectee will be subject to an investigation for suitability determination.
Position may require candidate to work evenings, weekends and holidays.
Back to top
Duties
Additional Duty Location Info:
1 vacancy - Washington DC Metro Area, DC
ebu tuache mambo ya kunyenyekea watu. kwani kuna ubaya gani kwa hilary kupokewa na membe. hao wote si mawaziri wa mambo ya nje. kwani membe akienda america atapokelewa na obama au mrs clinton. tena mara nyingi president wetu akienda america hapokelewi na obama.
ReplyDeleteKILO....HEBU JIULIZE MWENYEWE KWANINI UMEULIZA HILO SWALI? AU NDIO KTK WALE "ANKLE TOM"NAKUONEA HURUMA NA NINA MAJONZI NA NCHI YETU INALENGA PABAYA.
ReplyDeletemtoa mada wa kwanza hapo juu inaonekana nyie ndio wale wanaopenda utumwa uendelee kwenye nchi zetu
ReplyDeletewewe unataka kila kiongozi wa kimarekani akija hapa nchini apokelewe na rais ungejuwa kama viongozi wetu wakifika huko marekani wakati mwengine hupokelewa mpaka na mjumbe wa kijiji na baadae ndio wanakutana na uongozi wa juu
safi sana tena itapendeza zaidi ikiwa wageni wengi kama hao watapokelewa na waziri au viongozi wa ngazi za chini na baadae ndio wakutane na raisi wetu
lazima rais wetu apewe heshima yake na kuwa boss mkuu atakutanishwa na huyo kibaraka wa kimarekani baadae
Ankali wakati mwingine hata wewe unafaa kupokea viongozi kama hao huku ukiwa umevaa ile ze fulanaz iliyoombewa na babu kwa ze loliondoz.
Mchangiaji KILO hata hilo ulilochangia pia linaonesha kilo ulizo nazo kimawazo. Huku hata Mh kikwete akija huwa hapokelewi na mwenyeji wake ambaye ni rais, huwa anapokelewa na raisi mwenyeji nje ya lango la nyumba ya serikali ( ikulu) hivyo hata bwana membe haja kosea ni utaratibu tuu usimuelewe vibaya. Ni matumizi mazuri ya muda
ReplyDeleteNi kweli mdau hapo juu, nchi yetu inalenga pabaya, tena pabaya sana. Tangu lini USA INAKUA NA RAFIKI WAKUDUMU? Watawatumia viongozi wetu kutunyonya wakishiba wanawatupa kama "kondomu". Mobutu alikua mtu wako kalibia miaka 30 walipomchoka wakamwacha na kujifia ugenini kifukara kabisa. Viongozi wetu wanatakiwa wajifunze kwa hili.
ReplyDeleteNi sahihi kwa waziri wa mambo ya nje kumpokea waziri mwenzie wa mambo ya nje na ni kweli kwamba JK anapoenda Marekani huwa hapokelewi na Obama (sijui hata kama huwa anapokelewa na mtu yeyote zaidi ya wafanyakazi wa ubalozini).
ReplyDeleteUrafiki na Wamarekani unamaanisha kwamba wameshtukia kuna nafasi ya kutunyonya ambayo hawaitumii vema. Tumejiandaa angalau na sisi tupate kitu humo au ndio tutaendelea kunyonywa tuuuu?
unajua kuna watoa maoni hapa barazani wanakua hawana la kuandika,mfano huyo jamaa KILO ! anaandika Pumba..yaani unampangia kazi rais au serekali nani? wa kwenda kumpokea Mama Clinton?.Si bora ungechangia labda Mama Clinton asitushawishi kuunga mkono harakati za marekani katika kumuondoa madarakani rais Gaddaf wa Libya
ReplyDeleteYaani wewe Anonymous wa Sun. June 12,06:04:00 PM 2011 Umeona bora kumwambia mweznio anongea "Pumba" lakini unaona Gaddaf kubaki madarakani ni sawa?! Naona na wewe unachangia pumba kama huo ndio mchango wako, kwani Gaddaf amekaa madarakani miaka mingapi? Demokrasia iko wapi? Na Michuzi naomba usiniweke kapuni, kwani wabongo wanaongea pumba kweli humu.
ReplyDeleteSijawahi kuona maoni yote 14 ni pumba tupu duh, kweli watu balaa!!...Issue ya Bi Clinton ni ya kiuchumi ila hakuna hata mmoja aliyegusia issue hiyo. Ninachojua uhusiano wa Tanzania na Marekani hudhihirishwa kila muhula wa Rais anapoingia madarakani. Clinton mwenyewe sikumbuki alikuja na nini Tz, Bush akaja na net za mbu, ila watu bado wanakufa na malaria kila siku. Huyu mama naye sijui kaja na nini, labda umeme walahi, angalau tupone na giza hili. Huwezi jua bwana pengine naye ana maslahi kwenye hiyo Symbion Power...hebu mtuhabarishe. Ninachojua Marekani hawaji nchini bila maslahi fulani, sasa hebu muwaangushe kwenye maslahi yao muone watakavyokuwa wakali...hata hivyo bora waje tu kuangalia mitambo ubungo ili taa ziwake maana Watz wamechoka na vibatari na gharama juu. Akifanya hivi huyu mama iko siku atampigia JK amwulize km umeme unawaka Tanzania, maana ni aibu!!! Na leo sidhani km umeme haujakatika kweli na huyu mama akiwemo ndani ya Tz...hahahahaaa....aluuuu!!
ReplyDelete