Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka  (wa pili kushoto) akiwa na wafanyakazi wa  Mamlaka wakiwa na zawadi walizopata baada ya banda lao kushika nafasi ya kwanza katika kutoa huduma bora wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyomalizika hivi karibuni.
 Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Siylvia Lupembe Gunze akipongezana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Rosemary Lulabuka  (kulia) baada ya kumkabidhi zawadi walizoshinda kwenye Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Afrika yaliyomalizika hivi karibuni katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Habari na Picha na Francis Dande wa Blogu ya Jamii
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo wamekabidhi zawadi mbalimbali walizopata wakati wa Maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma iliyomalizika hivi karibuni katikaViwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea zawadi hizo na kufanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Mikocheni jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi huyo aliwapongeza wafanyakazi hao kwa nidhamu ya hali ya juu waliyoionyesha wakati wote wa Maonyesho hadi kuibuka washindi wa kwanza katika kipengele cha kutoa huduma bora pamoja na banda lao kushika nafasi ya pili kwa ubora.

‘Napenda kuwapongeza sana kwa kazi nzuri na heshima na sifa nzuri mliyoipatia Mamlaka yetu tunatambua juhudi zenu na muongeze jitiada katika kazi zenu za kila siku’ alisema Mkurugenzi huyo. Naye Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Siylvia Lupembe Gunze alisema kuwa kujituma na kufanya kazi kwa pamoja ndio kulikowafanya kuibuka washindi katikaMaonyesho hayo yaliyozishirikisha nchi mbalimbali kutoka katika Ukanda wa Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2011

    Tatizo hizo huduma bora mnatoa wakati wa maonyesho tu, tena mkiwa hapo hapo kwenye banda lenu. Tukija ofisini kwenu baada ya maonyesho ili mtuhudumie mnaanza miyeyusho ya kibongo, mara ohoo file alionekani,boss hayupo, hili haliwezekani hadi utoe chochote, sijui nini. Acheni huo ubabaishaji jamani, pigeni kazi nchi ipige hatua!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...