Mdau wa Seattle, Marekani, MC Catunda yupo kijijini kwao Mwange Mshindo, Songea, Tanzania, akishughulikia  ujenzi wa kisima cha kisasa chenye urefu wa mita 120 ambacho kitakuwa kikitumia Solar power  kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto yatima cha SWACCO  chini ya ufadhili wa Mwangaza Jitegemee USA na JAPAN  eneo ambapo itajengwa shule  kubwa ya watoto hao yatima ambao wanaonekana pichani wakiangalia uchimbaji wa kisima hicho
 
 MC Catunda akirejea nyumbani na mavuno ya alizeti shambani kwao
 MC Catunda akisaidia kuvuna alizeti
 MC katunda akisaidiana na watoto yatima kuchambua alizeti
 MC Catunda akiwa karibu na panapochimbwa kisima hicho
Wanachama wa Mwangaza Jitegemee USA na Japan Catunda na Kobayashi ambao wote ni wataalamu wa mambo ya Tv wakiwa kazini kijijini Mwange Mshindo, Songea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2011

    Dah!!! ama kweli box si mchezo, si unaona mwenyewe mkono huo?!!!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2011

    hongera mc katunda kwa kukumbuka kwenu, hicho kisima kitahudumia wengi sana hapo kijijini. wengine igeni mfano sio kazi kushindana kushusha suruali chini ya matako.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 10, 2011

    Asante sana shemeji yetu Kobayashi kwa shughuli zako za kujitolea kuleta maendeleo nchini kwetu,tusalimie sana dada yetu(mkeo)Fidea.
    Mdau Tokyo,Japan.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2011

    Mkono wa mbeba box unaonekana hii ni kudhihirisha kuwa anajituma na kufanya kazi kwa bidii,na siyo mabishoo huko bongo kila siku bonanza, Mango garden,Leaders club,Billicans nk.watu kazi hawafanyi kila siku ni starehe tu,na kwa mtaji huu bongo umaskini hautakwisha inabidi watu wabadilike na kupunguza starehe.
    mdau London.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2011

    AL HARAMAIN ALUMNI mnazidi kufanya vitu vyenu

    safi sana hiii

    bado akina Dau, Khalfani Mrisho, Mrisho Mzese na wengineo

    msikae sana huko nje mpaka mnajisahau

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2011

    tumeona mambo yako shem wetu keep it up tunakutegemea huu ndo mwanzo tu, mwangaza mzuri kwa otman wetu,
    MAMA MASI AND AISHA FROM KEKO MAFLATE CORNER...WISH U AL THE BEST

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 11, 2011

    mwenyezi mungu akupe kila la kheri kwa kazi yako nzuri. watanzania tulio nje ni lazima tusaidie wenzetu nyumani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...