Mdau wa Seattle, Marekani, MC Catunda yupo kijijini kwao Mwange Mshindo, Songea, Tanzania, akishughulikia ujenzi wa kisima cha kisasa chenye urefu wa mita 120 ambacho kitakuwa kikitumia Solar power kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto yatima cha SWACCO chini ya ufadhili wa Mwangaza Jitegemee USA na JAPAN eneo ambapo itajengwa shule kubwa ya watoto hao yatima ambao wanaonekana pichani wakiangalia uchimbaji wa kisima hicho
MC Catunda akirejea nyumbani na mavuno ya alizeti shambani kwao
MC Catunda akisaidia kuvuna alizeti
MC katunda akisaidiana na watoto yatima kuchambua alizeti
MC Catunda akiwa karibu na panapochimbwa kisima hicho
Wanachama wa Mwangaza Jitegemee USA na Japan Catunda na Kobayashi ambao wote ni wataalamu wa mambo ya Tv wakiwa kazini kijijini Mwange Mshindo, Songea








Dah!!! ama kweli box si mchezo, si unaona mwenyewe mkono huo?!!!!!!
ReplyDeletehongera mc katunda kwa kukumbuka kwenu, hicho kisima kitahudumia wengi sana hapo kijijini. wengine igeni mfano sio kazi kushindana kushusha suruali chini ya matako.
ReplyDeleteAsante sana shemeji yetu Kobayashi kwa shughuli zako za kujitolea kuleta maendeleo nchini kwetu,tusalimie sana dada yetu(mkeo)Fidea.
ReplyDeleteMdau Tokyo,Japan.
Mkono wa mbeba box unaonekana hii ni kudhihirisha kuwa anajituma na kufanya kazi kwa bidii,na siyo mabishoo huko bongo kila siku bonanza, Mango garden,Leaders club,Billicans nk.watu kazi hawafanyi kila siku ni starehe tu,na kwa mtaji huu bongo umaskini hautakwisha inabidi watu wabadilike na kupunguza starehe.
ReplyDeletemdau London.
AL HARAMAIN ALUMNI mnazidi kufanya vitu vyenu
ReplyDeletesafi sana hiii
bado akina Dau, Khalfani Mrisho, Mrisho Mzese na wengineo
msikae sana huko nje mpaka mnajisahau
tumeona mambo yako shem wetu keep it up tunakutegemea huu ndo mwanzo tu, mwangaza mzuri kwa otman wetu,
ReplyDeleteMAMA MASI AND AISHA FROM KEKO MAFLATE CORNER...WISH U AL THE BEST
mwenyezi mungu akupe kila la kheri kwa kazi yako nzuri. watanzania tulio nje ni lazima tusaidie wenzetu nyumani.
ReplyDelete