Na Hamad Hija,Maelezo-Zanzibar
Mkutano wa nne wa baraza la nane la wawakilishi Zanzibar unatarajiwa kuanza jumatano tarehe 15 mwezi huu huko mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Mkutano huo utakaa, kujadili,kuchambua na kupitisha bajeti ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2011-2012.
Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Mbweni, Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar , Ibrahim Mzee Ibrahim amewaambia waandishi wa habari kuwa kati ya mambo ambayo yatafanywa katika kikao hicho ni pamoja na kuuulizwa na kujibiwa masuala 237.
Katibu huyo amesema kuwa , mbali ya majadiliano ya Bajeti Baraza hilo litajadili miswada ya Serikali ikiwamo mswaada wa sheria ya kuidhinisha matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011-2012
Akizungumzia suala la kuvuja kwa Jengo la Baraza la Wawakilishi Ibrahim Mzee Ibrahim amekiri kuwa jengo hilo linavuja pamoja na kutoa mrejesho wa sauti,na kusema kuwa, wahusika hivi sasa wamo mbioni kurekebisha matatizo hayo.
Akizungumzia matatizo ya umeme katibu huyo amesema kuwa, Baraza la Wawakilishi Zanzibar tayari limeagiza Jenereta lenye uwezo wa KVA 725 ambalo limegharimu jumla ya shilingi milioni 335.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...