Baraza la Sanaa la Taifa kupitia wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.limepokea taarifa ya wasanii wa Tanzania kutakiwa kushiriki Maonyesho ya 16 ya sanaa ya Kimataifa yatakayofanyika Mjini Rho,Italia.

Maonyesho haya yanalenga bidhaa za asili na za kiutamaduni kutoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Asili (typical products) , Muziki (Musical events), Ngoma (Dances), Mapambo (colours) na vyakula (flavours) ambazo kwa ujumla wake zinaelezea historia ya nchi na watu wake.

Baraza linahimiza vyama na mashirikisho ya sanaa, wasanii, wadau wa sanaa kutumia fursa hii kuonyesha kazi mbalimbali za sanaa katika Tamasha hilo hapo juu.

Kwa maelezo zaidi juu ya maonyesho haya, wasanii na wadau wa sanaa watembelee tovuti ya www.artigianoinfiera.it au kuwasiliana na waandaaji kupitia barua pepe cratfsfair@gestionefiere.com au kwa simu +39 02 31911911 au nukushi +39 02 31911920.

Ghonche Materego
KATIBU MTENDAJI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...