Watoto wa Mitaani wakifanya biashara ya karanga na ubuyu.

Na Joseph Ishengoma - MAELELEZO, DAR ES SALAAM

Leo ni siku ya Mtoto wa Afrika.

Wakati tunaadhimisha siku hii, Serikali imetoa msimamo wake kuhusu vituo vya kulelea watoto wa mitaani na kusema haipendelei watoto kuwekwa katika vituo hivyo.

Badala yake imesema, jamii inatakiwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo la watoto wa mitaani ili kuepusha uwepo wa vituo hivyo.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi Tukae Njiku ametoa msimamo huo kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo leo jijini Dar Es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kilele cha siku ya mtoto wa Afrika kilichoadhimishwa leo.

“Serikali haisisitizi kuweka watoto kwenye vituo. Kufanya hivyo iwe ni hatua ya mwisho wakati unatafutwa ufumbuzi wa tatizo la watoto wa mitaani,” amesema.

Katika mkutano huo ulioudhuriwa na watendaji wengine wa wizara hiyo, Bibi Tukae ameeleza kuwa vituo vya watoto yatima lazima viwesajili na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

“Kama kituo kipo, serikali itataka kujua kama kimesajiliwa, baada ya kujiridhisha kuwa kinafaa kulelea watoto. Lakini kama kituo kinafanyakazi bila kusajiliwa, kituo hicho ni batili na kinatakiwa kufungwa,” amesema.

Takwimu zilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) zinaonyesha kuwa watoto wa mitaani duniani wanakadiliwa kufikia milioni 120, milioni 30 kati ya hao wako barani Afrika.

Aidha utafiti uliofanywa na Shirika lisilo la kiserikali la Consortium for Street Children mwaka 2009 yanayonyesha kuwepo sababu mbalimbali zinazochangia kuongezeka kwa watoto wa mitaani nchini.

Kwa mujibu wa utafiti huo, ukatili dhidi ya watoto unachangia kuwepo kwa asilimia 50 za watoto wanaoishi mitaani, njaa na umaskini 35%, ukosefu wa upendo 11% na kuvunjika kwa familia 4%.

Siku ya Mtoto wa Afrika uadhimishwa na nchi zote wanachama wa Umoja wa Afrika kwa mujibu wa Azimio lililopitishwa na Umoja huo mwaka 1990. hapa nchini kila mkoa utaadhimisha siku hii kwa kushirikisha Halmashauri zake pamoja na tarafa, kata na vitongoji.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Tuungane kwa pamoja kuchukua hatua za haraka kushughulikia tatizo la watoto wanaoishi mitaani.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2011

    Hao watoto wa mitaani au watoto wa familia masikini? Ubuyu umeshakubalika sasa Bongo!

    ReplyDelete
  2. Suala la watoto wa mtaani ni jambo ambalo hupewa umuhimu nyeti katika serikali zenye uchungu wa wananchi wao. Sishangai serikali kutoa tamko kama hilo inaonyesha huruma hamna. Watoto hao sidhani kuwa ni chaguo lao kukaa mitaani. Hatuna budi kama jamii kuangalia suala hili la watoto wa mtaani kwa upeo mpya. Ni jukumu la Serikali kuweka mikakati maalum kuhakikisha watoto wanabaki katika familia zao na kama haiwezekani basi kuwepo na idara za kusaidia watoto hawa ambao huimbwa kama ni taifa la kesho (au hawa hawamo katika wimbo huo). Watoto wanahitaji kulindwa kwa njia yeyote dhidi ya madhila yanayowakuta maana hao ndio viongozi, wafanyakazi, wahudumu wa kesho na wakiachiwa wajitete wenyewe mwisho huwa ndio wezi, wabakaji, majambazi wa kesho.. Inashangaza kuona serikali inabagua msingi muhimu wa maendeleo ya nchi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2011

    haitoshi kukataa! waandae mazingira mazuri kwa wananchi(ktk sekta ya afya hasa, nishati, na maeneo mengine ambayo ni basic kwa maendeleo na maisha bora ya mwananchi); na watoto wa mtaani watapungua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...