Rais Jakaya Kikwete akiwa na Hillary Clinton katika mkutano na waandishi wa habari, muda mfupi kabla ya mgeni huyo kuondoka
Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton wakiongoza mazungumzo ya kiserikali kati ya Tanzania na Marekani yaliyofanyika huko Ikulu, Dar es Salaam leo
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton na Mama Salma Kikwete mara tu baada ya Clinton alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam Leo.

 President Jakaya Kikwete with the US Secretary of State Mama  Hilary Clinton when they met for talks at the State House in Dar es salaam this morning. Mama Clinton is wrapping up her three-day tour of the country today. Below President Kikwete shakes hands with Mama Hilary Clinton after their talks. Photos by Freddy Maro of State House
MAREKANI YAIPONGEZA TANZANIA KUPAMBANA NA MATUKIO YA UHARAMIA
Na Joseph Ishengoma na Ismail Ngayonga
 MAELEZO
 Dar-Es-Salaam
RAIS Jakaya Kikwete ameiomba Serikali ya Marekani kuipatia Tanzania msaada wa Meli kubwa yenye uwezo wa kupita katika kina kirefu cha maji pamoja na mafunzo ya kijeshi ili kupambana na matukio ya uharamia katika bahari ya Hindi.

Rai hiyo imeitoa leo (jana) wakati wa mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton uliofanyika Ikulu Jijini Dar-Es-Salaam.

Mhe. Rais alisema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita hadi sasa kumekuwepo na jumla ya matukio 27 ya majaribio ya utekekaji wa meli katika pwani ya bahari ya Hindi upande wa Tanzania na katika majaribio hayo meli 4 za maharamia hao zimeshikiliwa na tayari watuhumiwa kadhaa wamefikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazowakabili. 

Alisema mafanikio hayo yametokana na uwezo mkubwa ulionyeshwa na kikosi cha Wanamaji katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania. “Katika mapambano haya bado Tanzania tunatafuta meli kubwa inakayoingia katika maji ya kina kirefu ili kukabiliana na uharamia huu,” Alisema Rais Kikwete.

Kwa upande wake Waziri Hillary Clinton ameeleza kufurahishwa kwake na hatua zilizochuliwa na Tanzania kupambana na vitendo vya uharamia katika bahari ya Hindi na kuhaidi kutoa ushirikiano kwa kadri inavyowezekana.

Akizungumzia kuhusu mgororo unaondelea nchini Sudan, Rais Kikwete ameeleza kuwa ameshafanya mazungumzo na Rais wa Sudan ya Kusini Silva Kiir pamoja na Rais Omar EL- Bashir kuhusu mgogoro huo na anatarajia matokeo ya mkutano wa usuluhishi wa mgogoro huo unaofanyika leo (jana)unaofanyika mjini Addis Ababa Ethiopia utatoa mwelekeo wa kumaliza mgogoro huo.

Aidha katika hatua Mhe. Rais Kikwete amesema hawezi kutabiri Rais atayeionogza Zimbabwe mara baada ya Uchaguzi Mkuu ujao.

“Kuhusu nani atakuwa Kiongozi wa Zimbabwe hilo liko nje ya uwezo wangu. Zimbabwe ni moja ya maeneo yanayojadiliwa na vikao vya Jumuiya ya  Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kinachotakiwa kwa pande zote mbili ni kutimiza makubaliano yao awali ili kuondoa migogoro ya kisiasa nchini humo,” alisema Rais Kikwete.

Viongozi hao awali katika mazungumzo yao Ikulu mjini Dar-Es-Salaam wamezungumzia migogoro mbalimbali ikiwemo ya kisiasa inayozikabili nchi za Bara la Afrika zikiwemo Madagascar, Zimbabwe, Somalia na Sudan.

Bi. Hillary ameipongeza msimamo wa wazi Tanzania katika kutatua migogoro mbalimbali ya kisiasa Barani Afrika.

“Naipongeza Tanzania kwa kuonyesha mwelekeo na msimamo wa wazi katika utatuzi wa migogoro mbalimbali Barani Afrika,” alisema.

Kiongozi huyo wa juu katika Serikali ya Marekani amemaliza ziara yake ya siku tatu ya Kiserikali leo (jana) hapa nchini na ameelekea nchini Eithiopia.
----------------------------------

STATEMENT BY H.E. JAKAYA MRISHO KIKWETE, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA, DURING JOINT PRESS CONFERENCE WITH HON HILARY RODHAM CLINTON UNITED STATES SECRETARY OF STATE, DAR ES SALAAM, TANZANIA, 13 JUNE 2011.

-

Madam Secretary of State,
Let me begin by once again, saying how happy we are to welcome you to Tanzania.  We are gratified and feel deeply honoured that you included Tanzania in your itinerary in Africa. Your visit speaks volumes about the state of our bilateral relations.   In many ways the exchange of visits by officials of our two countries has contributed immensely to the development and consolidation of our relations.   Tanzania and I have fond memories of the visit to Tanzania by former President George W. Bush and my three visits to the White House: two during President Bush’s time and one during President Barrack Obama’s administration.   Tanzanians are now anxiously awaiting visit by President Obama.  If he chooses to visit us, I promise that it will be the visit of  a lifetime.

Tanzania Benefits:
Our countries have benefitted from our bilateral cooperation.  Tanzania has received a lot of invaluable support from the US which has complemented our development efforts and continues to make a difference in improving the lives of Tanzanians.  The list is long but let me mention few things.

In the health sector, through the support of the US Government thousands of Tanzanians, including women and children who would have died of diseases such as malaria, HIV/AIDS and TB are alive today.  Thanks to the President’s Malaria Initiative, PEPFAR and other programmes.  Through US support, deaths from malaria have been reduced by half from 120,000 deaths per annum to between 60,000 and 80,000 and malaria has almost been eliminated in Zanzibar.  In the past, 40 per cent of outpatients in our hospitals used to be those suffering from malaria, today its only 20 percent.  The gains made in reduction of under-five mortality rate mortality is very much a function of malaria and HIV/AIDS.

HIV/AIDS:
With the support of the US government through PEPFAR over 13 million Tanzanians have been counseled and voluntarily tested for HIV.   Infection rate has declined from 18 per cent in the mid 1990s to 5.4 per cent to date.  Those infected can now get the requisite care and treatment.  Pregnant mothers who are HIV positive can now deliver children who are HIV free.

Education:
In education, let me thank President Barak Obama and you, Madame Secretary of State for delivering on two of my request I made when we met in Washington in May, 2009. I am pleased that we are getting science and mathematics teachers among the Peace Corps coming to Tanzania.

I am also grateful for the support in printing of science and mathematics text books for our secondary schools.  We have already received 800,000 textbooks which have been distributed and 923 schools have benefited.  Another1,425,000 books are on the wayThe availability of these textbooks plus support for teacher training will significantly reduce the shortage of books and go a long way towards improving the quality of education in Tanzania.

Millennium Challenge Account:
Through the Millennium Challenge Account a number of important roads are being built, water and electricity supply is being improved in Tanzania. When completed, these projects will benefit close to 8 million Tanzanians.

Counter Terrorism,  Counter Narcotics and Piracy
Our two countries have been working together closely in the fight against terrorism, narcotics and piracy.  We thank the US government for assisting our security organs in building capacity in this fight.  There are tangible results.  Tanzania has become a difficult place for perpetrators of these crimes to operate.  We have apprehended a number of them and brought them to justice.  I am pleased that you have agreed to continue cooperating in this area.

Money Well Spent:
Let me assure you Madam Secretary, United States tax payers money is well spent and is bearing the desired results of improving the living conditions of the people of Tanzania.

Future Cooperation:
We thank the US government for including Tanzania in two recent development initiatives of the Obama Administration: the US Partnership for Growth and Feed the Future Programme.  This will enhance Tanzania’s capacity for comprehensive growth and ensure food security and nutrition for our people as well as the neighboring countries that depend on Tanzania as their source of food.

Cooperation on Regional and International issues
Tanzania and the US see eye to eye on a number of regional and international issues.  We appreciate US leadership on global issues and promise to continue to work together for peace and development in Africa and the world.  Once again let me welcome you and the members of your delegation to Dar-es-Salaam!

Now, I am passing the floor to you with pleasure.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2011

    mheshimiwa umeomba meli ya kivita. ungeomba na mabehewa yatreni pia.na flaiovers.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2011

    Ungesema tu Rais ajae wa Zimbabwe ni fulani..ungekoma kwa Mugabe, si hajabu kesho tu angetua Dar umeeleze vizuri.

    Mwambie mama akupe pesa ushughulikie umeme wa STIEGLER'S GEORGE wa 2100MW. Muachane na huu mazagazaga ya Dowans.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2011

    natamani angekuja condoleezza rice,the former us sec. of state namzimia sana yule mazeri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...