Na Dina Ismail

WAREMBO 15 wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Inter college mwaka 2011 wataanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo jumapili hii kwenye ukumbi wa Break Point ulipo katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo Vicky Kimaro alisema warembo hao watakaotoka katika vyuo vya Cbe, IFM, Ustawi wa Jamii na DSj watakuwa chini ya ukufunzi wa Beatrice Lukindo na mrembo anayeshikilia taji hilo, Rose John.

Alisema maandalizui mengfine kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea ikiwamo kusaka wadhamini watakaiosaidia kufanikisha shindano hilo linalohusisha wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu vya jiji la Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa mwaka huu wamejipanga kuhakikisha wanapata washiriki bomba ambao wataiwakilisha vema kitongoji hicho katika ngazi inayofuata na hatimaye fainali za Miss Tanzania, huku tarehe ya shindano hilo itatangazwa baadaaye.

"Ndio maandalizi yameanza, nafasi zipo wazi kwahiriki wenye sifa kujitokjeza katika shindano letu, pia tunaomba makamopuni mbalimbali yajitokeze kushiriki shindano kletu", Alisema Vicky.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...