Kaimu Ofisa Tarafa ,Joseph Ogare ( kulia) wa Tarafa ya Malinyi, Wilaya ya Ulanga, akielezea mfumo wa kuhifadhi mahindi shambani unaojulikana kwa jina la Mabiwi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya( katikati) na (kwanza kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Francis Miti.
Mkulima wa mpunga ,Bakari Mwambungu ( kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya , wakati akipotembelea bonde la mashamba ya mpunga kwa wakazi wa Kijiji cha Misegese, Tarafa ya Malinyi, Wilaya ya Ulanga
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhandisi Evarist Ndikilo, ( aliyesimama) akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Namawala, kabla ya kumbaribisha Mkuu wa Mkoa , Issa Machibya ( suti nyeusi aliyekaa) kuzungumza na wakazi hao kuhusu masuala la ulinzi wa miundombinu ya taifa ikiwemo ya Tanesco na Reli ya Tazara na mingineyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, ( kulia) akiangalia mahindi yaliyovunwa na baadhi ya wakulima wa Kijiji cha Usangule, Wilaya ya Ulanga, Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya kilimo mara baada ya kumalizika msimu wa Kilimo .
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, akisaidia kupalilia shamba la maharage la mkulima Maula Sangusangu ( kushoto) wa Kata ya Nawenge, Wilayani Ulanga.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Namawala, Wilaya ya Kilombero, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, baada ya kupewa fursa na Mkuu wa Mkoa , Issa Machibya (hayupo pichani) kuzungumza na wananchi hao kuhusiana na masuala la ulinzi shirikishi na polisi jamii.
Baadhi ya sehemu ya Mji wa Mahenge makao makuu ya Wilaya ya Ulanga, ukiendelea kuendelezwa na wakazi wa Wilaya hiyo, kama unavyoonekana.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii- Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...