Kamishna wa Jeshi la Polisi,Afande Paul Chagonja akipokea msaada wa simu za Mkononi na Modem za intaneti kutoka kwa Afisa Biashara Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania, Chiruyi Walingo kwa ajili ya kusaidia kurahisisha mawasiliano ya ndani ya jeshi la polisi na pia baina ya jamii na Jeshi hilo
Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya (kulia) akiongea katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini.Kushoto ni Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini,Paul Chagonja na katikati ni Afisa Biashara Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Airtel Tanzania,Chiruyi Walingo.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Wanahabari waliohudhulia hafla hiyo.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, inayotoa huduma za gharama nafuu na zilizosambaa chini nzima, leo imeendeleza wigo wake wakusaidia wadau mbalimbali nchini ambapo safari hii imetoa msaada wa simu za Mkononi sitini, Modem sitini za intaneti, vyote vikitolewa ili kusaidia kurahisisha mawasiliano ya ndani ya jeshi la polisi na pia baina ya jamii na Jeshi hilo.
Msaada huu utaliwezesha Jeshi la Polisi, kupitia kitengo cha Maadili makao makuu ya Polisi kuimarisha mifumo na taratibu za udhibiti wa uadilifu kwa watendaji wake; kuwa wa kielekroniki na haraka zaidi kwa kuwawezesha wananchi kuwasilisha malalamiko au kutoa taarifa mbalimbali kupitia kwa waratibu wa kamati za maadili waliopo katika mikoa na vikosi vyote.
Kadhalika msaada huu umelenga kuimarisha jitahada za jeshi la polisi kufikia moja ya Malengo makuu ya programu ya maboresho ya Jeshi ambalo ni kuwa na Jeshi linalofanya kazi kwa kushirikiana karibu zaidi na Jamii ‘Polisi Jamii’
Akiongelea juu ya msaada huo, Afisa Biashara Mkuu, Chiruyi Walingo, alisema Airtel, ikiwa ni kampuni yenye kujali na iliyojidhatiti katika kuhudumia wananchi kwa gharama nafuu na mawasiliano ya uhakika, uwepo wa mawasiliano bora na nafuu ndio njia pekee inayoweza kuimarisha upashanaji wa habari hapa nchini, hususani kwa jeshi la Polisi .
“Katika kudhihirisha dhamira yetu ya kutoa huduma zenye gharama nafuu hapa nchini, tumeziwezesha simu zote sitini kuweza kuwasiliana baina ya zenyewe kwa zenyewe bila gharama yoyote katika muda wote wa matumizi, kila siku, wiki, mwezi na hata mwaka”, alisisitiza Walingo.
Aidha, Afisa Biashara Mkuu alisisitiza ya kwamba Airtel imedhamiria kuhakikisha kuwa inaendelea kutoa huduma za mawasiliano kwa kuzingatia gharama nafuu katika mawasiliano, sio tu kwa Jeshi la Polisi nchini, bali pia kwa jamii nzima ya watanzania, huku akiamini ya kwamba makubaliano haya na jeshi la polisi yatawezesha kuliongezea jeshi hilo ufanisi mkubwa wa kazi zake za kila siku.
Akitoa maoni yake kwa niaba ya jeshi la polisi nchini, Mkuu wa Jeshi laPolisi, Inspekta Jenerali wa Jeshi hilo Said Ally Mwema alisema kuwa uwezeshwaji huo kutoka Airtel utaimarisha kwa kiwango kikubwa ufanisi wa kazi ndani ya jeshi hilo, hususani katika utekelezaji wa majukumu ya waratibu wa kamati za maadili za Jeshi hasa kwakuwawezesha wananchi na watendaji wa jeshi hilo kushirikiana kudhibiti uadilifu napia kupata huduma ya haraka dhidi ya kero mbalimbali walizozo dhidi ya Jeshi lao.
“Tumefarijika sana na msaada huu kutoka Airtel, na kwa hakika, utawapa nguvu na ufanisi mkubwa wa kazi maofisa wetu, na hata kuwawezesha kufanya kazi kwa kujituma zaidi na kwa kusaidiana zaidi katika uratibu wa malalamiko ya wananchi kuhusiana na masuala mbalimbali yenye kuleta madhara katika jamii” Alisema.
Msaada uliotolewa na kampuni ya Airtel kwa jeshi la polisi una gharama ya zaidi ya shilingi milioni nane, ukiwa umelenga katika kusaidia uimarishaji wa mawasiliano ndani ya Jeshi hilo na wadau wake wote hasa baada ya kufanya uelimishaji na uhamasishaji wa kutosha utakapokamilika kupitia njia mbalimbali ikiwemo kutumia vyombo vya habari .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...