Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati walipokuwa wakitangaza michezo mbali mbali itakayowashirikisha warembo wa Kanda ya Dar es Salaam na waandishi wa habari wanawake.kulia ni Mwakilishi wa Waandishi wa habari wanawake,Vicky Kimaro.
Mwakilishi wa Waandishi wa habari wanawake,Vicky Kimaro akiongea na vyombo vya habari namna walivyojipanga kupambana na Warembo wa kanda ya Dar es Salaa (Ilala,Temeke na Kinondoni) katika michezo mbali mbali itakayofanyika Julai 9,kwenye ufukwe wa Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.Wengine pichani ni,Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah (pili kulia),Mratibu wa Miss Kinondoni,Boy George (pili kushoto) na Mratibu wa Miss Ilala,Jackson Kalikumtima.
Na Francis Dande wa Globu ya Jamii.
WAREMBO wa Redds Wilaya za Kinondoni, Ilala na Temeke watapambana kwenye mechi za kirafiki kati ya warembo wa kanda hizo tatu za Dar es Salaam pamoja na wanahabari wa kike kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redds Original ni wafadhili wakuu wa mashindano ya urembo ya Kanda za Dar es Salaam yajulikanayo kama Redds Miss Temeke, Ilala na Kinondoni. Kwa kuzingatia matakwa ya wananchi TBL imejikita sambamba na mashindano hayo na
imefadhili zaidi ya vitongoji na kanda 35.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah amesema kuwa 'Redd's inashiriki ipasavyo kwenye mashindano hayo Urembo.
Aidha Bw. Butallah aliongeza kuwa siku hiyo itajumuisha michezo kama, Kandanda, mpira wa mikono, mashindano ya kukimbia na kadhalika.
"Tasnia ya urembo ina mchango mkubwa kwenye jamii yetu sio tu kwa upande wa burudani bali inawapatia nafasi warembo mbalimbali Tanzania kukuza vipaji vyao na kuweka msingi ambao wakijipanga vizuri utawajenga na kuwaletea mafanikio kwenye maisha yao."
Naye Mwanadada Vicky Kimaro kutoka Mwananchi Communication akiongea kwa niaba ya wanahabari wanawake watakaochuana na warembo katika mchezo wa soka aliwataka watu wengi kujitokeza siku ya julai 9 kwenye ufukwe wa Mbalamwezi kuangalia jinsi watakavyowatoa nishai warembo wa kanda za Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...