Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(kulia) akikaribishwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Neema Mbuja (kushoto) wakati alipotembelea banda la Shirika hilo  kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere ili kujionea shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akiwasili katika Banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa ajili ya kuangalia na kujifunza shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na shirika hilo katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi kuhusu mradi wa uzalishaji wa chuma ghafi eneo la Maganga Matiti , Ludewa mkoani Njombe jijini Dar es salaam kutoka kwa Meneja wa Mradi huo Abdallah Mandwanga(kulia) wakati Balozi  huyo alipotembelea Banda la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Meneja Mawasiliano Neema Mbuja. Mradi huo unasimamiwa na Maganga Matitu Resources Development Limited.
Balozi wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mtaalamu wa Miamba(Geologist) wa Kampuni ya TANCOAL Alex Sosteness(kulia) kuhusu mradi wa machimbo ya makaa ya mawe wa Mbalawala wilayani Mbinga unaotarajiwa kuanza uchimbaji hivi karibuni.Mtaalamu huyo alitoa maelezo hayo wakati Balozi huyo alipotembelea NDC kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa Neema Mbuja.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2011

    ijumaa kareem uncle mithupu!uncle nna dukuduku nataka kushare na wana jamii pls uciichunie hii issue!ni kwa nn hapa tanzania hasa international airport ya dar wanachukua alama ya vidole kwa wananchi wa tanzania?kwa ninavyojua nchi za wenzetu wanaochukuliwa alama za vidole ni wageni ili kuepuka na magaidi wa nchi nyengine kuingia nchi iliyokuwa si yake.je hii inamaanisha kwamba watanzania wote ni magaidi?samahani wakubwa ni kwa kumwaga utamu na naomba kujibiwa kama itawezekana.ndimi mdau wa blog baaab k ya jamii.ahsanteni.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2011

    Anony wa mwanza ... Mbona dukuduku lako umeliweka ndipo sipo????????? (unrelated thread)....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...