Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia ushindi walioupata leo wa magoli 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati.Yanga imetinga fainali ya mashindano ya Kagame-Castle Cup kwa kuitungua timu ya St. George ya Ethiopia kwa idadi hiyo ya magoli.hivyo Yanga itakutana na Simba katika fainali hiyo itakayochezwa siku ya jumapili ya julai 10 katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
 Mashabiki wa timu ya Yanga wakiwa ni wenye furaha sana kwa timu yao kupata ushindi huo na kufanikiwa kutinga fainali ambapo timu yao itakutana na watani wao wa jadi Simba hapo jumapili ya julai 10.
Beki wa timu ya St. George ya Ethiopia,Alula Girma akijaribu kuondosha hatari iliyokuwa ikielekea langoni mwake na Mshambuliaji wa Yanga Jerryson Tegete.
Nurdin Bakari akichuana na beki wa St. Georges.
Wachezaji wa timu ya St. George wakizuiliwa na kina Ras Makunja wakati walipokuwa wakitaka kupiga sebene na  waamuzi wa mchezo kwa madai ya upendeleo.
Baadhi ya Mashabiki wa timu ya Simba wakiwabeza Mashabiki wa timu ya Yanga kwa ujumbe huu.
Dakika tisini za mchezo zimemalizika na haya ndio matokea yalivyo,na hivi sasa dakika thelathini zimeongezwa na mchezo bado unaendelea.
Ndani ya dakika 45 za kipindi cha pili lilitokea zengwe mara baada ya shuti kali lililopigwa na Shadrack Nsajigwa wa Yanga kuingia wavuni lakini kwa mpira uliokuwa umeishatika.hivyo mtafaruku kidogo ulitokea na hatimae muamuzi akasawazisha na mpira ukaendelea kama kawaida.
Sehemu ya Nyavu ilitoboka kutokana na shuti la Nsajigwa ikiwekwa sawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2011

    Nurdin Bakari ni tunu ya Yanga, jamaa namkubali saaaanaaaaa! Na huyu jamaa ndio atawatungua Simba J2, trust me, wa ukweli mnooooo!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2011

    najua hawa jamaa akina Ras Makunja hawanaga mchezo ktk mziki wao,na wachezaji wangeleta za kuleta ,mara moja muziki ungeanza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...