Jaji Mkuu Mh. Mohamed Chande Othmani(kulia) akipata maelezo ya ukarabati na ujenzi unaoendelea wakati alipotembelea Mahakama ya Kisutu jijini Dar.
NA MAGRETH KINABO - MAELEZO |
SERIKALI imeamua kufanya ukarabati mkubwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam, ambapo itakuwepo mahabusu ya wanawake, ikiwemo ya watu maalumu wa jinsia hiyo (VIP) unaokadiriwa kugharimu sh. milioni 750.
Hayo kasema Msanifu Mwandamizi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania(TBA),Deogratias Chubwa, ambao ndio wasimamizi wa ukarabati huo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya kibiashara ya kimataifa kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere DaresSalaam.
Hata hivyo ,Chubwa alisema gharama hizo zinaweza kuongezeka kutokana na uamuzi uliofikiwa baada ya kikao cha TBA na Maofisa wa Magereza kufuatia mahakama hiyo kutokuwa na eneo la mahabusu wa jinsia hiyo ambao walikuwa wanawekwa maofisini baada ya kufikishwa mahakamani hapo, ikiwemo kuongeza eneo la kuegesha magari. mengi zaidi ya awali.
Hata hivyo ,Chubwa alisema gharama hizo zinaweza kuongezeka kutokana na uamuzi uliofikiwa baada ya kikao cha TBA na Maofisa wa Magereza kufuatia mahakama hiyo kutokuwa na eneo la mahabusu wa jinsia hiyo ambao walikuwa wanawekwa maofisini baada ya kufikishwa mahakamani hapo, ikiwemo kuongeza eneo la kuegesha magari. mengi zaidi ya awali.
"Tunasimamia ukarabati mkubwa unaohusisha vitu vingi katika mahakama ya Kisutu, ambapo tunafanya ukarabati ya mifumo ya maji taka ambayo ilikuwa haifanyi kazi,kujenga uzio, mgahawa mpya mfumo mzima wa umeme na kuweka Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEKNOHAMA), Hivyo jengo la Mahakama ya KISUTU litakuwa la kisasa," alisemwa Chibwa.
Aidha Chubwa aliongeza kuwa ukarabati huo, unafanyika kufuatia jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kuboresha hadhi za mahakama mbalimbali nchini.
Alisema ukarabati huo ulianza mwaka jana na ulitarajia kukamilika Aprili mwaka huu,lakini umeshindikana kutoka ongezeko la eneo hilo la mahabusu na maegesho ya magari, hivyo unatarajia kukamilika Oktoba Mwaka huu.
Chibwa aliongeza kuwa fedha za ukarabati huo zinatolewa Mahakama kupitia Serikaliuu.
Alisema awali walishasimamia ukarabati wa mahakama za mwanzo katika mkoa wa DaresSalaam, ambazo ni Kigamboni,Mbagala, Kinondoni,Magomeni,Mazense, Temeke na Ukonga, uliokuwa ukifanyika kuanzia mwaka 2006 hadi mwaka 2008.
Michuzi,mbona Mahakama ya kinondoni haionyeshi kama ilishawahi kufanyiwa/kurekebishwa hata siku moja,au watu waliweka fedha mifukoni??????????
ReplyDeletemahabusu ya VIP? Mtu ameshawekwa mahabusu kwa kuwa ana hatia bado anapewa u-VIP? ok! sisemi mengi nikapigwa mawe bure!!!!
ReplyDelete