Kwa nini wazazi wakambo wanawekwa benchi

 katika shughuli muhimu za watoto wakambo?

Jana nilihudhuria mazishi ya binamu yangu wa karibu.Binamu yangu huyu alilelewa na mama wakambo karibu maisha yake yote.Kilichonishangaza na kunisikitisha ni kuona kuwa mama yake wakambo alivyowekwa kando wakati wa mazishi. 


Ninachomaanisha ni kuwa, wakati wa kumwaga udongo na kuweka mashada kaburini, waliitwa mume wa marehemu, baba mzazi na mama mzazi, wadogo wa marehemu, na mpaka shangazi na wajomba zake. Lakini mama wakambo akarukwa!!Hivi ni katika hatua gani mchango wa wazazi wakambo katika malezi ya watoto huanza kuthaminiwa? Binamu yangu amelelewa na mama wakambo toka akiwa mdogo. 


Lakini leo hii amefariki, ndugu hawaoni umuhimu wa kumhusisha mama huyu kwenye matukio muhimu ya kumwaga udongo na kuweka mashada. Kulikuwa kuna ugumu gani kuwashirikisha wote mama mzazi na wakambo?Au ni mpaka pale mama mzazi anapokuwa hayupo (amefariki, nk), ndipo mama wakambo anapopewa heshima yake?Na kwenye shughul za harusi mambo yanakuwa hivi hivi....kama mama mzazi yu hai, basi mama wakambo hakai kwenye meza ya wazazi, hatambulishwi, halishwi keki, hanyweshwi shampeni????




Inasikitisha kuona kuwa mpaka leo hii bado 
tunaendelea kuwabeza wazazi wakambo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2011

    Mama wa kambo ni mlezi tu kam housegirl kwani house girl aliweka maua? As long as mama mzazi yupo itakuwa si haki awe replaced wakati mtoto kazaa mwenyewe. Yeye mama kambo hana watoto wake. Asubiri wafe au waolewe kwa nini amind na atake pewa cheo kisicho chake. Kwanza ungejiuliza kwa nini haitwi mama anaitwa "mama kambo" ndio ujue mama kambo "si mama"

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2011

    Unajua haya mambo ni ya aibu somehow. Yaani wewe unataka MC kwenye harusi aseme mama yake bwana harusi na mama yake wa kambo wasimame? Ebo, huoni kuwa utafanya ukumbi uone kuwa bwana harusi ametoka kwenye familia isiyoheshimu ndoa. There is nothing to be proud of when you have been raised with someone who is not your mum while your mum is still alive.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2011

    Inategemea na mume. Tamaduni za TZ zimemzalilisha mama wa kambo kiasa na yeye hapendi watoto wa kambo, na watoto wa kambo na wanachukia wazazi wa kambo. Tamaduni zibadilike.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2011

    Pole sana ndugu yangu kwa uliyoyaona. Kwanza si halali kumtenga mama wa kambo aliyeshiriki kumlea mtoto wa kambo.

    Lakini kwenye jambo kama hilo huwa kunakuwa na vijimambo vingi vilivyojificha ambavyo hakuna aliye tayari kuviweka wazi. Nikianza na upande wa wanawake wanaokubali kumlea mtoto wa kambo, ni vizuri ukafahamu kwamba si wote wanaokubali kwa dhati jukumu hilo. Unakuta mwanamke anakubali tu kwa unafiki kuwa atamlea huyo mtoto kwa vile tu hana namna nyingine ya kukwepa naye anamuhitaji huyo mwanamume. Sababu kubwa ya kuchukia jukumu hilo ni kutokanana mambo mawili:
    1. Mwanamke anajiuliza ni kwa nini nilee mtoto mwenye mama yake na ambaye mamake yuko hai?
    2. Maswala ya urithi wa mali yatakuwaje? Hili linatokea hasa kama mwanamume amechuma vijimali kidogo. Wanawake wengi wanaweka mbele sana mambo ya urithi wa mali kwa watoto waliowazaa wao na hivyo kujikuta wakiwa na wivu kwa watoto wa kambo. Kwa sababu ya hili, wenye roho ngumu hudiriki hata kuwauwa watoto wa kambo kwa sumu hasa anapohisi mzee anaweza kukatika siku yoyote. Utafikiri wao hawafi. Chuki hizi zinakuwa kubwa zaidi kama mwanamume ulificha kuwa una mtoto wakati mnachumbiana.

    Kwa sababu hizo, inapotokea mtoto wa kambo amefariki, watu wengi huanza kuhisi labda ameuawa na mama wa kambo. Kuna tukio moja lilitokea Dodoma ambapo baba mmoja alikuwa amezaa mtoto kabla ya ndoa na mwanamke mwingine halafu akafunga ndoa na mwanamke mwingine. Walikubaliana tangu mwanzo kuwa kuna mtoto wa nje na atakuja kuishi na watoto wengine. Wakati yule mtoto anaishi na mamake wa kambo na wadogo zake wengine maisha yalikuwa yanaenda vizuri na hakuna mahali huyo mama alipoonesha chuki yake. Katika kuhangaika na maisha yule baba akapata vijihela vyake akajenga restaurant pale dodoma kisha akaiita jina la yule mtoto wake wa kwanza. Mama wa kambo aliposikia jina la hiyo restaurant ni la mtoto wa kambo, akaamua kuwatuma watoto wake dukani halafu akamwambia yule wa kambo abaki wakati huo mzee yupo kwenye mihangaiko. Baada ya watoto wake kuondoka aliamua kumnyonga yule kijana kwa khanga hadi kufa na kutaka kumtupa nje. Bahati nzuri wakati anaenda kumtupa majirani wakamuona wakamkamata.

    Kwa upande wa wanaume sijawa na ushahidi wa mambo mengi kama hayo kwani wanaume wengi wanakuwa na uhuru wa kumkataa mwanamke mapema kama wakigundua amezaa. Na kwa wale wanaokuwa wamefichwa siku wakigundua wanachofanya ni kumchukia huyo mwanamke na kuanza kuchachapa nje. Zaidi wanakuwa "frustrated" lakini sijasikia wakifanya jambo la kutoa uhai wa mtoto.

    Ushauri wangu kwa wanaume wenzangu. Unapoona umezaa mtoto na mwanamke mwingine ni vema ukamuacha yule mtoto kwa mama yake na kama kuna ulazima wa kumchukua, basi mpeleke kwa ndugu zako ila uwe unapeleke pesa ya matunzo na kumsomesha. Najua wanawake wengi hupenda kutumia mtoto kama sbabu ya kudai pesa kwa wanaume waliozaa nao ndio maana wanaume wengi huamua kuchukua watoto wao ili kuepukana na usumbufu wa namna hii. Lakini ni kheri ukagharamika kupeleka pesa kwa mwanamke mwingine kuliko kumuacha mtoto wako katika maisha ya wasiwasi.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2011

    nakubaliana na mc wa shughuli alivyofanya mama wa kambo wengi wameingia kwenye hizo nyumba kinguvu na inawezekana ndiye aliyemfanya huyo mama aachane na mume wake. hata angejifanya mwema mama wa kambo ni mama wa kambo tu. asubiri wa kwake afe atafanyiwa anavyotaka.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2011

    Mchangiaji wa kwanza hahahahaha

    Mama wa kambo ni mama lakni kwenye mambo kama ulio andika
    kama mama mzazi yupo kwa nini aitwe yeye?au kwa vile alikuwa dada yako
    ndio maana ukandika hivi.....
    Je kama mama wa kambo alimpindua mama mzazi asichukiwe?
    Pole sana lakni ujue Mama ni mama haitobadilika hiyo.....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2011

    Ukweli ni kwamba kama mama wa kambo ndie aliyesababisha mama mzazi akimbie nyumbani basi hana haki ya kupewa heshima mahala popote. Lakini wa mama wengi huondoka ndani ya nyumba kwa tamaa zao na kumwachia baba watoto pekee sasa yeye atahitaji msaada ndipo mama wa kambo huingia basi kama heshima apewe la kwa kuwa ni mtu wa msaada ktk tuta basi ajinyamazie tuu kwani Mungu ndiye atakaemlipia mema na si mwanaadamu. Kwa kuwa wewe umeumia sana unajua undani zaidi...uzuri jema hata dogo namna gani kwa Mungu halipiti bure halikadhalika baya... litalipwa tuuu hapa hapa duniani ahera ni mahesabu. Mama wa kambo si housegirl pls anonymous wa kwanza...just put yourself in her shoes...wanawake tupendane na tusishutumiane...housegirl ni mtu muhimu ktk nyumba ndio maana unafanyakazi au biashahara wakati watoto wako na mume wako wakiwa salama...Mungu wabariki waanawake wa Kitanzania ameni!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2011

    Huo ni uelewa wa mtu binafsi. Kama mtu aliitelekeza nyumba yake na akapatikana mbadala wake ni muhimu yule mbadala wake akapewa heshima yake. Kulea mtoto siyo kazi nyepesi hivyo kama mzazi mwenyewe alichemka akaachika au akatelekeza familia sioni haki ya kuheshimiwa hapo baadaye kisa alimzaa binti au kijana, aliyelea mpaka mtoto akakua ndiye anastahili heshima yake.....

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2011

    Jamani mimi nina mtazamo tofauti, kuna watu nawafahamu wamelelewa na mama wa kambo na hawana ulalamishi. Yaani mama wa kambo wamekuwa wakijitolea zaidi kuliko mama zao katika makuzi. Kuna mdada namfahamu hadi analipiwa ada ya kusoma university nje ya nchi na mama wa kambo. Baba mtu hana muda. Wakati mwingine binadamu hatuna shukrani. Wewe mama au nyie ndugu wakati mtoto analelewa na mama wa kambo nyie mlikuwa mmekufa? Iweje leo mshindwe kusema ahsante?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 01, 2011

    Haki ya nani? Yaani hivi kweli tanzania kuna watu wenye akili finyu kama mdau wa mwanzo? Hili ndio moja ya sababu tanzania hatuendelei. Fikira za wengi ni mbovu sana na ni chuki kupita kiasi.

    Mdau wa mwanzo alipoona neno mama wa kambo basi ni kujumlisha wote kuwa ni mbaya. Kuna mama wa kambo tele wanalea watoto wa waume zao kama watoto wao waliowazaa, sio tanzania tu bali nchi tele duniani wanaonekana sana hasa katika karne hii tuliyonayo. Ni kosa kuwapiga fimbo moja mama wa kambo wote.

    Na kwa nini mdau wa mwanzo hakuuliza ni kwa nini mama wa mzazi aliachana na baba wa mtoto, kwa nini hawako pamoja, jee alikuwa akimuangalia mwanawe? mwandishi amesema kuwa mama wa kambo ndie aliemlea mtoto maisha yake yote, jee mama mzazi alishindwaje kumchukuwa mwanawe na kumlea mwenyewe.

    Siandiki mengi maana kila nikisoma alichoandika mdau wa mwanzo hamaki zinazidi na nashindwa hata kuandika ninachotaka kusema hapa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 01, 2011

    HIYO ULITAKIWA UIOTOE HAPO HAPO MAKABURINI BILAKIJALI LOLOTE

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 01, 2011

    Muuliza swali umeleta hoja ya msingi sana. Jamani si kweli kuwa mama wa kambo wote ni balaa na kwamba mama wazazi wote ni wema. Kuna mama wazazi ambao waliwatupa watoto wao chooni, mtoto akaokotwa na akalelewa na mama wa kambo. Siku ya harusi au mtoto huyu anapofanikiwa mama mzazi anaona kuwa ana haki zote! Nakumbuka miaka ya 80 au 90 Vijana Jazz waliimba wimbo MAMA WA KAMBO (http://www.youtube.com/watch?v=K5xokwWaBqE). Tafadhali sikiliza wimbo huu!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 01, 2011

    Mama wa kambo sio mama.
    Huyo ni kibarua tu wa baba kumburudisha.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 01, 2011

    waswahili wanasema tenda wema usingoje shukrani. MUNGU ndiye atoaye hukumu na kulipa. wakati mwingine nadhani utamaduni au watu ndio wenye matatizo maana kama kweli mama wa kambo amemlea vizuri na hakupwa heshima eti kisa si mama yake mzazi lakini wakati wa kulea anabeba majukumu yote kama vile mama mzazi nadhani hapo anakuwa kama vile hakutendewa haki. Ila napenda kumtia moyo kuwa thawabu yake ipo kwa MUNGU kama alimtendea mema marehemu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 01, 2011

    Tatizo hili sio kwa mama au baba wa kambo tu, ni kwa walezi wote wanaolea watoto wa wenzao. Utakuta mtu kalelewa na shangazi, mjomba, mama mdogo/mkubwa au ndugu yoyote yule lakini ikitokea kitu chohote cha kumhusu huyo mtu hao walezi hawashirikishwi kabisa. Na hii si mila wala desturi bali ni tabia mbaya za dharau na ubinafsi tulizojijengea siku hizi. Tangu enzi watoto walikuwa wa wote na ikitokea anataka kuoa au kuolewa basi mzazi anakaa kando na kutoa madaraka yote kwa mlezi tena wanasema wazi huyu bwana ni mtoto wako si umemlea mwenyewe na watu baki kamwe hawatajua kuwa huyo si mtoto wako wa kumzaa. Lakini siku hizi choya na ubinafsi zimetawala utalea mtoto wa mwenzio akikua kila kitu kwa wazazi wake wewe wala hakuthamini kabisa.

    Mfano mdogo tu mimi nililea mtoto wa marehemu shemeji yangu, yaani msichana nililetea darasa la nne nikamkazania shule mpaka akafaulu, angekuwa kwao asingefaulu darasa la saba, na alipofaulu ile form one tu akaanza uhuni na kuzurura akaondoka kwenda kwao, akipeleka keki wanafurahia akirudi na chips wanachekelea akileta mkate sikukuu, alipofika form two akafeli. Wakaja kuniomba aje akae tena kwangu, nikamkubalia na kumbana mpaka hiyo form two akafaulu kuingia form three, akatoroka bila kuaga. Akaenda huko kwao form four akafeli akasoma shule private za form five na six nako akapata angalau grade. Na huyo kwao ni msomi kweli kweli ukilinganisha na wengine. Siku alipopata mume anataka kuolewa nilifanya kusimulia siku ya harusi kuwa leo ndio anaolewa nikawaambia akakae salama kwa mume. Kisa malezi, ukimweka mtoto kwenye mstari unaonekana mbaya unamtesa, wao wanataka mtoto akuletee mpaka mabwana ndani, aje na chips na kuka na mikate na kake ndio usasa huo ukikataa hayo na kuwa strict wewe ni mbaya na una roho mbaya.

    Kwa hiyo kwanza hata sishangai hao waliomtenga mama wa kambo wa huyo marehemu inawezekana kwa ushirikina wao washaenda kupigiwa ramli kuwa karogwa na mama yake wa kambo! Cha msingi wewe ni kutenda wema wende zako usingoje shukurani kwani mwanadamu habebeki hata umpe au umfanyie nini haishi lawama.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 01, 2011

    Ni busara mamo yenu ya kifamilia mkayamaliza kifamilia. Kila familia ina matatizo yao, kwa hiyo blog ya jamii isihusishwe na mambo binafsi ya kifamilia.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 01, 2011

    Huo nimtazamo duni kwa mama wakambo mi huwa nawaita mama mlezi nasio kinamama wote walezi wana matatizo au wanakuwa namtizamo hasi dhidi ya watoto wawaleao kwahiyo basi kama mama mzazi yupo atatambulishwa kama mama mzazi na vivyo hivyo mama wa mlezi (WAKAMBO) atatambulishwa kama mama mlezi ni hayo tu msibaguane wandugu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 01, 2011

    ah mama wa kambo wanawa abuse watoto wa wenzao kwahiyo sioni haja ya wao kupewa attention yoyote,iwe harusi au mazishi. huyo binamu yako hakukupa stori yoyote ya unyanyasaji,unless huyo mama wake wa kambo alikua wa kipekee.
    Acha TZ waendelee na utamaduni huo huo,mama wa kambo hana sauti au thamani kama mama mzazi yupo. habari ndo hiyo.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 01, 2011

    Tamaduni zetu kwa zaidi zinanyanyasa wanawake

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 01, 2011

    Mchangiaji wa pili,kama mama mzazi yupo hai,lakini mama wa kambo ndo amemkuza mtoto,mama mzazi hamjui mwanae nje ndani kama mama wa kambo anavyomjua,nani awe recognized mama wa kambo au mama mzazi?...There is something to be proud of when you have been raised by a woman who isn't your biological mother, she took care of you and raised you as her own, she's the one who gave you all the affection and not your biological mother...all in all she also deserves recognition, your biological mother might as well, but not as the woman who has really been there for you.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 01, 2011

    Hizo ni tabia za "USWAHILI" tu,sioni sababu ya kumbeza mama wa kambo ambapo huwa anakuwa amesumbuka kumlea mtoto hadi akakua,Mimi binafsi nimelelewa na mama wa kambo na nikafanikiwa kusoma vizuri hadi nchi za nje,hii yote ni bidii ya mama huyu na kunitilia mkazo nijali masomo pia niwe na tabia au maadili mema wakati wote.Inabidi tuute kabisa hii mentality ya kuwaona mama wa kambo siyo muhimu,hata kama kuna sherehe au msiba siyo lazima itajwe kuwa huyu ni mama wa kambo,kuna weza kuwa na njia nzuri ya kistaarabu ya kumuhusisha naye aweze kujisikia kama binadamu,hata akiitwa mama mdogo si vibaya,Watanzania tuache tabia za kizamani ambazo zimepitwa na wakati,matatizo mengi katika familia zetu husababishwa na sisi wenyewe,kutokana na mtazamo finyu wa mambo mengi yanayo tuzunguka na pia tabia za uswahili,Tumthamini na kumheshimu mama wa kambo kwani yeye pia ni mama ingawa hakumzaa mtoto muhusika.
    mdau Washington Dc,Usa.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 01, 2011

    ikiwa watanzania wengi wana akili kama za mdau wa mwanzo basi hali haitobadilika, sio juu ya suali hili tu bali mengi ambayo kijamii yanahitaji marekebisho.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 02, 2011

    Kwa kweli mara nyingi mama wa kambo huwa ameingilia ndoa ya mwenzake (yaani mwizi wa mapenzi) ndio maana hawathaminiwi! Pia ni aibu kuonyesha kuwa kuna mama wawili. Ni kitu ambacho huwezi ukakilazimisha. Wanaume hujifanya ni halali kuwa na wake zaidi ya mmoja lakini machoni kwa watu hulionea aibu jambo hili. Hata huyo mzazai ungemwambia tumtambulishe mama wa kambo nina uhakika angekataa. Kwahiyo wanawake tufumbue macho, tuache wizi wa mapenzi. Mwisho wa siku huna unaloambulia ni aibu tupu.
    Nawe uliyeandika hapa, leta hoja za kuchangia maendeleo. Hizi zinarudisha nyuma maendeleo, mama wa kambo ndio chanzo kikubwa cha watoto wa mitaani.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 02, 2011

    Mchangiaji wa kwanza na wa pili big up. I like your reasoning.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...