Nitashukuru kama nitapata kushiriki na wadau wa blog ya jamii katika suala hili.
Yapata mawiki kadhaa sasa hapa nchini Tanzania pamekuwa na taarifa za uwepo wa samaki wenye mionzi ya Juclear kutoka Japan. Nafurahi kusikia serikali inashuhulikia, wamepeleka sampuli Afika kusini na Kenya (TDFA?????????? TBS??????????? Tume ya mionzi?????????????) Anyway hiyo siyo hoja yangu kwa sasa.
Kwa kuwa mimi ni mfanyabiashara mdogo, hoja yangu ipo katika watengenezaji wa bidhaa nyingi tunazotumia. Utakuta nakwenda kariakoo kununua bidhaa mbali mbali kwa ajili ya wateja wangu. Kinachonitatiza ni hii lugha “….unataka feki au original”? Mimi ambae sina uelewa wa kitaalam, katika masuala ya engineering, kemimali na electronic, nawezaje kulijua hili kama huu sio mtego ambao serikali yetu ndio yenye uwezo wa kudhibiti kuachia hali hii iendelee kutuumiza.
Pia kuna baadhi ya vitu ukinunua, kwenye makasha yake hakuna jina la bidhaa(Brand name) wala address ya mtengenezaji. Hii ni hatari kwani kitu kama hicho kikileta madhara hujui nani wa kumuuliza. Na wahusika wameacha tu viingie nchini. Mbali ya makasha hayo kutokuwa na majina ya watengenezaji/wasambazaji, ukienda kununua vitu vingi wawezakupewa vitu havipo ndani ya makasha, alafu unapewa makasha matupu ili ukaweke mwenyewe ndani ya makasha kwa ajili ya kuwauzia wateja wako. Hii si siri wahusika wapite tu kariakoo madhalani maduka yanayouza vifaa vya electronic au vipuri mbalimbali watabaini hilo. Tunashukuru Mungu vya samaki wa mionzi vimeonekana, na je hivi ambavyo kila leo vinatupa madhara ya kupoteza pesa zetu ovyo nani atashuhulikia? Sisi walipa kodi ni lazima tulindwe na serikali yetu ili tuendelee kuitumia. Sasa mbona hamtulindi tunauziwa vifaa ambavyo haina viwango mitaani, vyakula vyenye sumu kama hawa samaki? Tukifa wote nani atalipa kodi?, nani atapiga kura? Wateja wetu wakidhurika tutauza wapi bidhaa zetu?
Nashauri yafuatayo na pia ushauri mwingine upokelewe toka kwa wadu watakoshiriki kuchangia katika mada hii:
- Tume ya ushindani wa bidhaa nchini, ifanye kazi kwa ufanisi ili kuzuia tangu bandarini/viwanja vya ndege na mipakani uingiaji wa bidhaa ambayo hazijulikani zimetengenezwa na nani?
- Tume ya mionzi ijengewe uwezo ili kuweza kufanyakazi kiufanisi.
- Mamlaka ya chakula na dawa iongeze juhudi na kuzuia vyakula vyote hatarishi kwa maisha yetu walipa kodi
- Mdau Mkere Ketwa
Mdau pole sana hilo ni tatizo kubwa hata ughaibuni. Kwa ufupi njia moja kwa utafiti wangu ni kuwa uangalie bei, duka liuzalo, na "brand". Sony wameruhusu watu maalum kuwauzia bidhaa zao. Hiyo kwa "brand" nyingi tu, Nokia, Toyota na n.k. Usitegee Kariakoo au Darajani kupata bidhaa "Original". Kuna supermarket moja kwa mama ilitaka kuuza jeans za levi's kwa bei poa, wenyewe levi's waliwapeleka mahakamani. kwa lugha nyengine bidhaa original zinauzwa na maduka maalum pengine TZ hakuna hayo maduka, kwa ufupi ukinunua bidhaa hapa nyumbani ni kuwa unatia mkono kizani!!!!!!!
ReplyDeleteMadau Mkereketwa, Hoja zako ni nzuri na zina uzito mkubwa kwa manufaa ya nchi yetu. Swali..Unataka feki au Orijino..ni la kawaida sana huko Kariakoo, hususan kwenye vifaa vya umeme. Hata hivyo, ukweli ni kwamba hamna Orijino, vyote ni feki. Utakuta kifaa kina kasha lenye ramani ya Uingereza halafu unaambiwa eti Made in England! Nani atengeneze ext. cable Uingereza kisha uje uuziwe kariakoo kwa Tsh. 1500?
ReplyDeletePia kuandika tu haitoshi, maandishi nayo feki si yapo? Suluhisho lilikuwa hizo taasisi..Mkemia mkuu, Mionzi, TBS etc ambazo ziko tele, kuweka viwango na kisha kutest kila bidhaa kwamba inakidhi viwango vilivyowekwa. Halafu walaji yaani akina sisi ukikuta kifaa hakikidhi viwango, unawapelekea hao nao watamfilisi huyo muhusika. Lakini si tunajua kuwa TAKUKURU ililetwa kumaliza suala la Rushwa? Je inatusaidia?!