Jijini Mwanza leo kuanzia majira ya saa 3:10 asubuhi,kumezuka vurugu kubwa sana kati ya wafanyabiashara ndogondogo al-maarufu kama Wamachinga na Jeshi la Polisi jijini humo kwa madai ya kwamba wafanyabiashara hao kufukuzwa eneo lao la biashara tofauti na makubaliano, hali iliyosababisha watu kaadhaa kujeruhiwa na wengine watatu kuhofiwa kupoteza maisha.
Vibanda kadhaa vimevunjwa na Baadhi ya bidhaa zilizopangwa nje zimeibiwa nayo matairi yamechomwa katikati ya njia panda kuingia mtaa wa Makoroboi kuelekea Soko kuu na kiunganishi cha barabara ya Lumumba Mwanza huku baadhi ya wamachinga hao wakirusha maboksi yaliyoshika moto kwenye majengo yaliyo karibu na eneo hilo kwa nia ya kuyachoma moto.


Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza,Afande Simon Sirro akielekea eneo la tukio kutoa amri ambayo kwa kiasi ilirejesha amani.



Kusanyiko la shaka-shaka huku kina Ras Makunja wakiwa wameweka pozi ndani ya Difenda lao.



Matairi pia yamechomwa mbele ya lango kuu la soko kuu la jijini Mwanza hali iliyopelekea kufungwa kwa soko hilo na biashara kusitishwa.



Wafanyabiashara wakichungulia yanayojiri nje kupitia lango kuu la soko kuu.



Kona ya kuingia barabara ya Msikiti wa Ijumaa kutokea barabara ya Nyerere risasi zimelia ile mbaya huku wananchi wakikimbia kujihami na mabomu ya machozi.


Market Street hakuna shughuli inayofanyika kwa sasa kwani hata vibaka wametumia mwanya huu kufanya uporaji.


Mtaa wa makoroboi kulikoanzia vurugu hakuna biashara inayofanyika maduka yote yamefungwa.


Ni moja kati ya hasara zilizojitokeza kwa jengo hili ambalo wamiliki wake ni watanzania wenye asili ya Kiasia lililoungana na msikiti wa Hindu.


Mpaka sasa hivi barabara ya Nyerere haijatulia kwani kuna umati mkubwa wa watu eneo hili mawe yakirushwa nayo mabomu ya machozi yakisikika mitaa ya Makoroboi, Alhamini, Maketi na Msikiti wa Ijumaa kuwatawanya waandamanaji.Picha Zote kwa hisani ya G.Sengo Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2011

    jamani Tanzania, tunaelekea wapi??? kwa kweli hii hali inaendelea kutisha sasa kadri siku hadi siku .
    Mungu IBariki Tanzania

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2011

    Michuzi mambo? huu ni uhuni(wote polisi na Wamachinga ni wahuni)..


    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2011

    kuna vijana kwenye hii bulogu wanachochea vurugu. wanajiona wana mashabiki kibao, wameshakuwa maarufu sana wanaanza kurusha makombora uhamishoni marekani. wewe unayejiita nabii ndo wewe nakusema

    ReplyDelete
  4. tatizo letu kwenye mambo yanayohusu maendeleo tunaleta siasa,haya yasinge tokea endapo huyu mbunge angeacha upambe na upendo wa kinafiki pale walipo waambia hawa machinga waondoke katika ya mji,niupuuzi na ujinga kuwa wapambe kisiasa na vibendera wafuatao upepo na walaani na kuwa laumu hasa hawa wanasiasa wa liochukua hili jiji la mwanza na hiki chama chao ....shame on you

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2011

    Hivi jamani suala la machinga ndiyo kusema halina suluhu kabisa????? Hivi mamlaka husika haiwezi kuja na mpango kazi mzuri ambao utawafanya machinga wawe confortable na kazi zao pasipokuwa na adha kama hizi? Hii inafanya hata wasiohusika waweze kuumia kwa gharama za watu wengine. Mfano hilo jengo la watanzania wenye asili ya India limepigwa mawe wakati wao hawana uhusiano wowote na biashara za machinga. Tunaiomba serikali na wamachinga wakae pamoja na kukubaliana nini kifanyike ili kutatua tatizo la vurugu kama hizi. Tanzania ni nchi ya amani, je kwanini amani hiyo ianze kuchafuliwa na vitu vinavyoweza kuepukika??????
    Mdau

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 06, 2011

    Huu nzigo namtwishA john mashaka kwa kuwa Ty Ndo kaanzisha huko Swali la matabaka ya Wachina na wahindi wakatj bila hawa watu hatuna maendereo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2011

    naona akina Ras makunja wameminya,wanaogopa kusamba magitaa,wasukuma sio mchezo

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 06, 2011

    JOHN MASHAKA umuhimu wa article uliyoileta jana unaonekana na inaonyesha kiasi gani wazawa wa ukweli tunavyonyanyasika,kwa kweli tunanyanyasika sana.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 06, 2011

    Haya Chadema wanafurahia sasa. Hivi kweli jamani tunataka tuwe kama Somalia au Burundi na Rwanda? Likianza timbwi hapo hamna atakaepona,weather you are Indian,arab or mmatumbwi wote tutaumia.Sana sana watoto na kina mama zetu ndio watapata shida zaidi. Jamani tuacheni ujinga wa kufikiria chama fulani kikichukua nchi basi wewe utafaidika,hiyo sahau. Mafanikio ni juhudi zako binafsi. Na viongozi wote wa vyama vyote ni wale wale tu. Wote wana personal interest.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 06, 2011

    Nyie watu nyanbaf kweli. John mashaka anahusjka vipi wakati hapa . Haya yaliyotokea ni kama unabii wake kwa maanake aliandika kwamba wananchi hasa wataamua kuchukua nchi yao toka kwa hawa wakoloni mambo leo

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2011

    Suluhisho ni rahisi sana kama linavyofanyika katika nchi nyingi ulimwenguni. Wamachinga au wafanya biashara ndogo ndogo (upendavyo kuwaita) hupatiwa mahali katika mji na helo eneo huwa linagawanywa pande nyingi ambapo wamachinga huleta bidhaa zaoa na kuuza bila maudhi yeyote. Maafisa wa manispaa inayohusika (na sio akina makunja na mgambo) ndio husimamia malipo ya matumizi ya hapo mahali. Inategemea na manispaa husika, kama kuchukua malipo kwa kila siku mmachinga anapochukua sehemu ya kuuza au kwa wiki. Askari huwepo pembeni kuhakikisha usalama wa wananchi, wamachinga na wakusanya malipo wa manispaa. Endapo mmachinga akikataa kulipa ada ya matumizi ya sehemu anayouza bidhaa zake hapo ndipo polisi huitwa na kumuamuru mmachinga afunge virago vyake na kuondoka, sio kumharibia au kuchukua mali yake, kiustaarabu kabisa anatakiwa kuondoka. Anapobisha na baada ya kuonya bila kusikiliza hapo ndio askari hutumia uwezo wake kumkamata na kumpeleka kituoni . Hilo pia hutendeka bila ya kuharibu mali za mmachinga.

    Tanzania hili kwa nini lisiwezekane?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2011

    Hali inayoendelea mwanza so nzuri hata kidogo. Watu wamechoka na hii serikali ya wanamagamba, na kusema kweli namuunga mkono beans JOHN MASHAKA 100% kwa maana aliandika ni kweli na ndiyo imeanza kutokea hapa nchini. Mwanza ni mwanzo tu, bado kariakoo. Dr. Endelea kumwaga nondozo mkuu tunakuaminia

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 06, 2011

    jamani hapa suala si siasa wala chama,, Hasa wewe Siegfried. Issue ni je wamachinga wafanye biashara zao vizuri na waendeshe maisha yao.. Swali kwanini vurugu zisitokee miaka yote mpaka leo hii baada ya watu kutaka kuwahamisha??

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 06, 2011

    Tanzania ya Sasa inahitaji tindu lissu, zitto kabwe na john mashaka 10 tu. Huu ni mwanzo tu. Hata sisi ndani ya CCM tumechoka kabisa

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 06, 2011

    Nadhani hatujanyanyasika vya kutosha, huu ni mwanzo tu, hatujafika hata robo ya kunyanyasika. Hao wanosema ni uchochezi au ni Johna mashaka nadhani hawajui viongozi wetu ni wa namna gani, hatuna viongozi, hatuna msaada, hatuna chakula , hatuna elimu, hatuna chochote, wachina na wale wote waliotoka nchi nyingine ndiyo wanoongoza nnchi. Mbona hatujasikia watu wengine wamerushiwa mabomu yani ni wazawa tu ambao ni walala hoi. Mkombozi wa walal hoi ni mlala hoi mwenyewe kama hatajikombowa hakuna lelemama, ubaguzi upo na umeshaingi Tanzania, kama wewe ni maskini ni maskini huna chako utakufa maskini na mtoto wako hataona mlango wa chuo. Hataona faida za mali za nchi zinakokwenda hata kama amelala kwenye kijiji amabcho kinatowa alimasi usiku na mchana, kama wewe ni masikini hutaona hata chembe ya alimasi inakopita.

    ReplyDelete
  16. Tanzania yetu sio nchi ya AMANI.Wananchi ni wabaya wanashambulia hata kutaka kuchoma moto vituo vya polisi ipo siku hao polisi wataanza kuchomewa nyumba

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 07, 2011

    @anonymous , hebu hacheni kumpaisha mashaka kwenye level la rais eti. Hata sisi tumekula buku sana ila tumetulia kitaa. Mtuu kufaamu kiingerrza sana siyo kuwa na akili ya kuwa rais wa nchi. Mashaka Ikiwa rais wa Tanzania haki ya mbingu naama hii nchi. Ila namtumia mshure baba rizone jumbo kwamba nchi inachafuka abadilishe uongozi

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 07, 2011

    Nduguzanguni umaskini, au ulala hoi hauondolewe na vurugu au kuchoma moto matairi, au kuwavunjia watu nyumba zao kisa eti serekali inawaondoa majinga kwenye maeneo yaliyo katazwa na serekali, huo ni ukosefu wa imani na upendo,kwann kusikuwepo tuu na maongezi ya amani tuu,au hao viongozi wa vyama vinavyo penda maandamano na uchochezi wasikae kwa amani na viongozi wa chama tawala mkayamaliza tuu kibinaadamu bila mtu kuumia au kupoteza maisha na hasara za ajabu, mjue pakiwaka moto hapo ndo maisha yatakua magumu maradufu ya hapo. Tujitume kwanguvu zetu binafsi ili tuongeze vipato sio vurugu. Mungu tuendelezee amani Tanzania na ibariki amin

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...