Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Mtwara waliojitokeza kumsikiliza mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana jioni.
Rais Dr.Jakaya Mrisho kikwete akiwahutubia wananchi wa Mtwara katika uwanja wa Mashujaa jana jioni
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Bwana Ashvin Ganatra ambaye ni mwakilishi wa mfanyabiashara maarufu Mustafa Sabodo wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi sekondari ya Mustafa Sabodo mjini Mtwara jana jioni.Bwana Sabodo amechangia zaidi ya Shilingi bilioni moja katika ujenzi wa shule hiyo na pia ametoa  vifaa mbalimbali vya kufundishia na kuahidi kuleta waalimu kutoka India kwa gharama zake. Shule hiyo inachukua wanafunzi kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara ikiwa ni juhudi za kukuza kiwango cha elimu katika mikoa hiyo miwili. Picha na mdau  Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2011

    Eh Mnyezi Mungu mzidishie baraka huyu mzee,mpe pepo yako baada ya dunia hii. How lovely to see this wonderful news,haya mambo yalitakiwa kufanywa na wazawa pia sio kuwacheka tu ati watu wa kusini hawataki soma and so on hapa umeonyesha mfano hopeful Adam Malima unaona haya nawe utafanya kwa watu wako, wa pwani,na pesa hiyo unayo ila roho tu ya kufanya hivo je ipo??

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2011

    Mh Raisi nadhani unapata picha ni kwa nini tuna pigia kelele gap linalozidi kutanua kati ya walio nacho na wasio nacho.fikiria huo umati ulivyochoka na ndani ya serikali yako mtu mmoja tu anaingiza hasara ya kuwapa tiba nzuri angalau huo umati tu kwa takribani mwaka mzima.Tafadhari tafakarini mnapotembelea watu waliochoka kama hao na bado wanawapendeni na kuwatukuza bila kujua kama wanadhurumiwa haki yao.Na ole wako michuzi usitoe maoni yangu kwani siku hizi unabagua CCM mkubwa wee.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2011

    Safi sana! nataka niwakumbusha wadau kwamba Mbunge wa zamani wa Mtwara Mjini Mh. Mohamed Sinani alichangia sana kufaniskisha ujenzi wa shule hii. Asnen Murji upo hapo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2011

    Hongera nyingi kwa Mzee Sabodo. Ingefaa wazawa wengine nao waige mfano huu mzuri toka Baba huyu. Hebu angalia jinsi wengine tulivyo wabinafsi kupita kiasi. Utadhani Tanzania hii haina kitu wala utajiri wowote. Tujisahihishe kupitia uongozi huu wa sasa na Chama hiki hiki Tawala. Angalia shule zilizopo kijijini mwako. Ona utajiri wa kutupa walio nao akina ... Kwani hawakuupata hapa hapa Tanzania? TUFANYE KWELI KATIKA ELIMU TANZANIA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 26, 2011

    Hayo ndio maneno we Anony Te Jul 26, 03:45:00 PM! Ni kweli kabisa, huyo mh. tulikua nae bega kwa bega kuleta maendeleo ya mkoa wetu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...