Shujaa wa Vita ya Pili ya Dunia Mzee Ernest Paulo Waya akiongea na Globu Dada ya Jamii, Mbeya Yetu, amesema serikali imewatelekeza na kutowajali kwa chochote na kuwazulumu mafao yao mashujaa hao wa zamani ila huwaona wa maana sana siku ya mashujaa tu ambapo amesema huwaita ili washiriki pamoja siku hiyo. Amedai kwamba zoezi hilo likiisha huwa wanatelekezwa mpaka mwaka mwingine tena. Mzee Waya amesema ndiyo maana mwaka huu wenzake wengi hawajaja kwani wapo kujitafutia riziki maana kula yao ni ya shida sanaMzee Ernest Waya akiweka upinde na mshale kuwakumbuka wenzake aliokuanao vitani enzi hizoMzee Ernest Waya akitoa heshima mara baada ya kuweka upinde na mshaleToka kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mbeya John Mwakipesile wapili ni Mstahiki meya wajiji la Mbeya Mh Atanas Kapunga watatu Mzee Ernest Waya wanne ni mwakilishi wa machifu wa MbeyaShughuli imekwisha Mzee Waya huyooo ndiyo wamekwisha msahau hawana mpango nae tena. Hapa anaelekea ofisi ya mkuu wa Mkoa Mbeya apate msaada wa usafiri kumrudisha kwake Mbalizi
Home
Unlabelled
shujaa wa vita ya pili ya dunia apasua jipu mbeya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
HUYU MZEE ANATIA HURUMA SANA. KAMA WAHUSIKA WANA MASIKIO BASI WAMESIKIA. YAANI HATA USAFIRI WA KUMRUDISHA KWAKE HAWAKUMPATIA?
ReplyDeleteBILA SHAKA NAYE MWAKANI ATAINGIA MITINI NA KUSUSIA SHEREHE HIZI.
Lakini walipigania vita muingereza ili azidi kututawala sasa wapeleke malalamiko yao ubalozi wa uingereza. Pia UK Tanzania wafikishe malalamiko kwa mama maana hao ni wenzao isipokuwa tu wamemtumikia wakati tafauti!!
ReplyDeleteSidhani kwamba ni haki kuwalaumu wao kwani kwa kipindi kile ndiyo mfumo uliokuwepo.
ReplyDeletePia mdau ukumbuke vile vita vya pili walivyopigana nchi tofauti ndiyo vilivyowaamsha na kuwaelewesha kwamba kumbe hata Wazungu nao hupigika. Na ndipo harakati za kugombania uhuru zilipoanza.
Niliwahi kusikia kwamba walikuwa wameletewa pensheni zao pamoja na fedha na maangalizi ila kuna kipindi serikali iliwahi kuwadhulumu. Mwenye ukweli atujuze. Hii ni sawasawa na ile ya Afrika Mashariki kwani fedha zilizoletwa zilitumika kwa mambo mengine na mpaka leo wanataseka na kufa pole pole.
kwanza hao waliomuita ni wauwaji sana malipo hapahapa mimi angekuwa mzee wangu nisingemuruhusu anaambulia kula chakula cha siku moja na mkuu wa mkoa alafu anarudi kulala chini anafuatwa na gari kurudi kwa miguu huo ushahidi tosha hapo anatembea anaelekea kwake hiyo njia inaelekea kwa mama john mbeya ndo anaishi kule karibu na mzee mmoja nae alikuwa mkubwa siku hizi analima maparachichi
ReplyDeleteNafikiri huyu ndiye Sikamona niliyemsoma katika kitabu cha ZAWADI YA USHINDI cha Amandina Lihamba
ReplyDeleteKuna pesa zilikuwa zinatolewa na serikali ya Uingereza lakini wajanja wa serikalini wakawa wanazila.Nchi yetu haina huruma kamwe
ReplyDeleteSerikali ingekuwa imemtelekeza angekuwa katakata hivyo? na suti ya nguvu hivyo?
ReplyDeleteAnon, Zawadi ya Ushindi kiliandikwa na Amandina Lihamba au Ben Mtobwa?
ReplyDeleteMiaka ya 80, kuna chama fulani cha Royal Commonwealth, iliyowasafirisha waliopigana WWI kwenda Uingereza kwenye sherehe. Pia pale Faya Dar kulikuwa na Club ya hao WWI na WWII veterans. Hivi bado ipo? Najua kuwa wote waliopigana WWI wamefariki, je, hao wa WWII waliobaki wako wapi? Tunapaswa kuona hao waliobaki mali. Sasa huyo Mzee anatembea na gongo anakwenda kuomba lifti, ni aibu tupu!
ReplyDeleteNa ni kweli serikali ya Uingereza walileta hela ya kuwasaidia hao Veterans lakini pesa zilipita serikalini kwanza na hao wazee walipata kiduchuu!
Why is the Head Chief wearing a Joker's Hat? Looks like a Halloween Costume!
ReplyDeleteHa ha ha wacha mbavu sina, mdau wa halloween umegusa haswa, huyo chifu ni mjukuu wake alimletea hiyo kofia wakati wa likizo na chifu akai-mind sasa kaivaa wakati wa hafya ya kitaifa basi we sisi mbavu hatuna, lakini si haba watu wengi walioudhuria na wanaosoma hii blogu hawakugundua kuwa ile kofia ilikuwa ya Joker!!!!
ReplyDeletealex bura, dar
hiyo ndio bongo ya dasalame ya wadanganyika bana nyingine ni feki kula chako mapema ukimaliza muda wako saga inakusubiri
ReplyDeleteWazee wote nchini wamechoka wa wliopigania WWII, uhuru na wazee kwa ujumla. Malipo yao walilipwa na serikali ya Uingereza ni nani aliyenaudhibitisho kuwa serikali iliwadhulumu? Wazee kama hao wa kenya wanaenda Uingereza kudai kama wanaona wamedhulumiwa. Kwa wasio na uwezo wa kusafiri basi wanaenda kwenye barozi zinazohusika. Ila serikali inapo muita kujumuika kwenye sikukuu yao lazima watakuwa wamepewa suti nyeusi, nauli na malazi na mapochopocho mengine. Mzee huyo baada ya kumaliza shughuli na kwa kuwa kisha pata chake inabidi aanze safari kurudi. sio tena kudai gari kama maelewano ni yalikuwa hivyo. Hivyo wadau tusikuze mambo PESA TAMU
ReplyDeletejuzi walitakiwa waliopigana vita vya dunia wakale pensheni yao kama ana akili huyu akusanye wenzake na ushahidi aende ubalozi wa uk tu huwenda pia akahitimu maisha yake huku huku UK.
ReplyDeleteuMRI WAO NA VIONGOZI SAWA SAWA LAKINI UKIMUANGALIA UTAFIKRI ANA MIAKA 100
Mbona hujasema UMRI WA HUYU MZEE? NI MHIMU SANA TENA SANA.
ReplyDeleteBabu yangu mpaka anakufa alikuwa akiniadithia jinsi walivyozulumiwa pesa zao zilitoka kama sikosei uingereza lakini kuna siku sisi wajukuu zao tuta dig in na kutafuta nini hasa kilitokea na kama ni kweli ni akina nani hasa wanausika na ulaji huu ili sheria ichukue mkondo wake pole sana babu nasikia uchungu kwani wewe ni sawa na babu yangu kabisa pole sana.
ReplyDeletedaa iyo ndio serekari ya tz wajanja wengi sana kila mtu anakula upande wake
ReplyDeletewengine mpaka leo wanandika majina na wengine wameshaandika zaidi ya mara kumi hasa kipindi cha uchaguzi
ReplyDelete