Vikombe vya ushindi wa michezo ya Umitashumta  kwa kanda ya mashariki vikiwa vimewekwa mezani mara baada ya kukabidhiwa kwa Mkuu wa Morogoro, Issa Machibya ( kushoto),wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa timu hizo.
Mwalimu wa kitengo maalumu kwa Viziwi wa Shule ya Msingi Kilakala, Haji Mvungi (kulia) akiongea kwa lugha ya alama na wanafunzi wake ambao walishiriki katika mashindano hayo.

baadhi ya wachezaji wanafunzi wa shule za msingi wa Mkoa wa Morogoro, wakiwawakilisha wenzao wa Mkoa wa Pwani, wanaounda Kanda ya Mashariki ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingi Tanzania ( UMITASHUMTA) mara baada ya kutwaa vikombe vinne vya michezo mbalimbali pamoja na medali 16 kati ya hizo 13 za dhahabu, mbili za fedha na moja ya shaba, baaada ya kumalizika kwa mashindanio ngazi ya taifa , Julai 7, mwaka huu mjini Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Kanda zilizoshiriki ni Kanda maalumu ya Dar es Salaam, inayoundwa na Mikoa ya kimichezo, Ilala, Kinondoni na Temeke.,Kanda ya magharibi mikoa ya Tabora na shinyanga, kanda ya ziwa, Mwanza na Mara, kanda ya kati, Dodoma na Singida, Kanda ya kusini , Mtwara na Lindi,Kanda ya nyanda za kusini, Iringa na Ruvuma,Nyanda za juu , Rukwa na Mbeya, Kanda ya Kaskazini Mashariki , Kilimanjaro na Tanga na Kaskazini Magharibi ni Arusha na Manyara.Na John Nditi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2011

    Unatubania mapicha ya Yanga at Jaydee....lol Ankal wewe ni Simba au?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...