Kama kumbukumbu za harakati za marehemu Sekou Toure Mndeme (akiongea pichani) katika kujishughulisha na Mtandao wa Wanataaluma Tanzania, zifuatazo ni baadhi ya kumbukumbu zilizopo TPN. Bila shaka wengi mtaweza kuzitambua picha zifuatazo na matukio yaliyoambatana na picha hizo. Katika pila picha wapo pia wana TPN wengine ambao pia wanaweza kutambuliwa. Mnakaribishwa kutoa maoni  kuhusu picha hizi na hata kuzungumza machache kuhusu marehemu Mzalendo Mndeme: BOFYA HAPA

Wasalaam
                                                                  Mz. Sanctus Mtsimbe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2011

    Marehemu Sekou Toure nilimfahamu mara ya kwanza mwanzoni mwa miaka ya tisini pale chuo kikuu cha Dar-es-salaam, tulipokuwa wote tunachukua shahada ya kwanza. Alikuwa ni rafiki wa wote,mcheshi na mpenda watu.Tabia ya ucheshi na kupenda watu aliendelea nayo hata alipoanza kazi CRDB alipohitimu masomo yake, kila tukikutana alikuwa mwingi wa tabasamu na furaha, kwakweli sijawahi kumwona akiwa na uso wa huzuni na masikitiko, hata akiwa amegubikwa na tatizo lolote. Marafiki wa Toure, CRDB na taifa kwa ujumla limepoteza mmoja wa watu wema, lakini tunaamini huko alikokwenda atapumzika mahali pema peponi. Mungu awabariki wafiwa wote. Amin.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2011

    Vijana wenzio wa zamani pale Usagara Sekondari ( 1980 - 1983 )tutakukumbuka daima kwa ucheshi wako na ushirikiano wako mzuri katika kila fani. Hatutasahau vichekesho na utani wa kila mara usiokera kwa wanafunzi wenzio na hata walimu.
    Eee MOLA WETU ILAZE ROHO YA MAREHEMU TOURE KATIKA BUSTANI YENYE UPEPO MWANANA.

    Juju, Father, Kindoroko, Shortman na mwalimu wetu Kichwa cha nyoka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...