Moja ya Style ya wanenguaji wa Khanga moja na kitu Tigo wakati wa kuwapagawisha mashabiki.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KIKUNDI cha wanenguaji mahiri wanaojulikana kama Khanga Moja Ndembe ndembe na Kitu Tigo wanatarajia kufanya onyesho la aina yake katika Ukumbi wa Arusha City Park Jumamosi ya Julai 30, kuanzia saa tatu za usiku hadi majogoo.

Khanga Moja na Kitu Tigo wanazidi kujipatia umaarufu mkubwa hapa nchini hasa maeneo ya jiji la Dar es Salaam kutokana na aina yao ya uchezaji inayowaacha hoi wadau na mashabiki wa muziki wanaokwenda kuwaona mabinti hao.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa onyesho hilo, Karen , akiwa chini ya Kampuni ya ONE2B Entertainment , alisema shoo hiyo itakuwa ya aina yake kutokana na mikakati yao kabambe, wakiwa na maana ya kuwaonyesha wadau wa jijini Arusha, umakini na vipaji vya wakina dada hao wa Khanga Moja na Kitu Tigo.

Alisema kufanya vema kwa mabinti hao sehemu mbalimbali za Tanzania kumewafanya na wao watamani kuwapatia burudani hiyo mashabiki wa jijini humo, ukizingatia kwamba watakua wakichuana vikali na kuwaona mabinti hao ni burudani tosha.

“Nadhani mashabiki wa muziki wa jijini Arusha hasa kupitia unenguaji wa wakina dada hao wa Khanga Moja na Kitu Tigo wanaotamba nchini wakifanya makubwa katika kulishambulia jukwaa wakivalia vazi la khanga linalotoa macho wadau wengi.

“Nawaomba mashabiki wote bila kujali itikadi zao kuja kwa wingi katika onyesho hilo maalumu kwa ajili yao, likiwa la mwisho kabisa katika kuelekea mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, hivyo nadhani mashabiki watafurahia burudani hiyo,” alisema Karen.

Khanga Moja wanaofahamika pia kwa jina la Laki si pesa wameibuka katika siku za hivi karibuni na kuchengua wengi wanapokuwa jukwaani wakicheza kwa ubinifu wa hali ya juu, bila kusahau aina yao ya kucheza wakiwa wamevaa khanga. Wakati Kitu Tigo wao wanafahamika zaidi kwa jina wakali wa kuchezesha nyonga .

Kufanyika kwa onyesho hilo la watoto wa khanga moja ndembendembe na Kitu Tigo wakali wa nyonga jijini humo ni nafasi ya kuonyesha makali yao kwa watu wa huko, ikiwa ni baada ya kutokea mkoani Tanga kwa Wagosi wa Kaya, wakifanya shoo pia mjini Korogwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2011

    sawa wamepata umaarufu, ila wajiweke sawa sasa hasa ki mwili,show yao watu wengi wamegundua hao wadada ni wachafu kimwili hasa miguu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2011

    Hawa watakuwa na lao jambo. Kwanza hizo kauli mbiu zao; "KITU TIGO" na "LAKI SI PESA" ukichanganya na huo uvaaji kanga moja, zina maana kubwa kwa mtu mwenye akili.

    Picha ninayoipata hapo ni kwamba kuvaa kanga moja kunakuhamasisha uamshe miwashasha, kitu tigo maanake tigo inatolewa na laki si pesa manake ukitaka hiyo tigo usije na laki ukafikiri utapata uje na zaidi ya laki. Hawa wanajiuza.

    Sijui kama tutapona kwa mtindo huo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2011

    Arusha Kutawaka Moto..Hao Madada ni soo...sipati picha hii show ya Tarehe 30

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2011

    Nahama kutoka tigo, nahisi nadhalilishwa siku baada ya siku.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2011

    huyu dada kwa mtindo huu,kuzaa hadi akamwazime punda hapo ndo ile bakora ya mzee punda inaweza kumfaa huyu mdada!!hafu, hivi mdada kufanya michezo kama hii ya kudhalilisha ina maana ni umasikini wa akili au umasikini wa pesa au ndo mtasema vipaji mungu kawapa???

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2011

    Arusha kwetu mnapoteza muda tu, wenyewe mna rangi mbili ya mwili wenu na uchafu juu. Mtatuambie nini na inaelimishaje jamii aliyebuni nampa o
    tena mko kama mpo sokoni mkimaliza show mnasikilizia mwanaume gani yupo free. Acheni hii tunaanza mwezi mtukufu tunataka kuwa swafiiiiii

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2011

    Tuendelee katika kuhamasisha ngono na kuendelea kulipa gonjwa nafasi ni kweli tutakufa sio masihara

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...