Mgeni Rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Uratibu Mhe. Stephen Wassira akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bwana Daniel Ole Njoolay pamoja na viongozi wengine kabla ya kuanza zoezi la utoaji wa zawadi.
Mgeni Rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Uratibu Mhe. Stephen Wassira akimpa zawadi ya Cheti Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega bwana Kyuza Kitundu baada ya kushika nafasi ya pili kwa halmashauri zilizofanya vizuri katika kipengele cha manunuzi.
Wadau wa habari, Mathew Kwembe, Afisa Habari Mwandamizi TAMISEMI (kushoto), Emanuel Minja Afisa Masoko Mwandamizi wa TBC (katikati) na Joshua Joel Mwakilishi wa ITV Mkoa wa Rukwa wakiwa uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga jana wakati wa kilele cha Siku ya Serikali za Mitaa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bwana Daniel Ole Njoolay akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga bwana John Mzurikwao wakiwa katika banda la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Mgeni Rasmi Mhe. Stephen Wassira akitembelea banda la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwenye maonyesho hayo katika uwanja wa Nelson Mandela.
Kikosi kazi cha Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kikiwa tayari kumsubiri Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uratibu Mhe.Stephen Wasira kutembelea banda lao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...