Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Mohamed Gharibu Bilal akifungua rasmi maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam leo katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Makamu wa Rais, Dkt Mohamed Gharibu Bilal akizundua rasmi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za ufunguzi wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam.
Msemaji wa Wizara ya Fedha,Ingiahedi Mduma akipokea kikombe cha ushindi wa kwanza leo jijini Dar es salaam kutoka kwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt.Mohamed Gharibu Bilal baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la huduma za uchapishaji / uchapaji , na viandikia vya uelimishaji (Publishing ,Printing, Stationaries Exhibitors) wakati wa maonyesho ya 35 ya kimataifa ya Dar es salaam yaliyofunguliwa leo jijini Dar es salam.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Mohamed Gharibu Bilal akiongoza viongozi wengine kuimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Raslimali watu Issa Nchasi( mweye suti nyeusi) wakifurahi ushindi wa kwanza wa watoaji wa huduma ya uchapishaji na viandikia vya uelimishaji kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es alaam yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere.Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es salam
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Raslimali watu Issa Nchasi( mweye suti nyeusi) wakifurahi ushindi wa kwanza wa watoaji wa huduma ya uchapishaji na viandikia vya uelimishaji kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es alaam yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere.Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es salam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua rasmi maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa , wakati alipotembeleea maonyesho hayo katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Dar es Salaam, leo Julai 01, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikata utepe kuzindua, Redio Sibuka FM.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi ya Mjomba, Mrisho Mpoto, akitoa burudani mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati wa uzinduzizi wa maonyesho hayo leo Julai 01, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimabidhi Tuzo ya ushindi wa jumla Mkurugenzi Mkuu NSSF, Dkt Ramadhan Dau, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Dkt. Ramadha Dau, akifurahia tuzo yake baada ya kukabidhiwa.
Wafanyakazi wa NSSF wakijidai na tuzo walizopata |
Dkt. Ramadhan Dau akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa NSSF, wakifurahia kwa pamoja na tuzo yao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimabidhi Tuzo ya ushindi wa kundi la Engineering Priducts, Mkurugenzi Mkuu wa Sido, Mike Laiser, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimabidhi Tuzo ya ushindi mwakilishi wa Home Shopping Center. wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka baada ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo, uliofanyika leo Julai 01, 2011 kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
Mwakilishi wa SBL, akiwa na tuzo yake baada ya kukabidhiwa kama wadhamini wakuu wa kinywaji cha maonyesho hayo.
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akitoka nje ya banda la Maliasili na Utalii, wakati akikagua mabanda ya maonyesho.
Akiendelea kutembelea mabanda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NMB, Imani Kajula, wakati alipotembelea na kukagua Banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa, baada ya Makamu kuzinduz maonyesho hayo rasmi leo Julai 01, 2011. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Mark Wiessinga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Mark Wiessinga, wakati alipotembelea na kukagua Banda la benki hiyo katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa, baada ya Makamu kuzinduz maonyesho hayo rasmi leo Julai 01, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua bidhaa za Delphine Mlambiti wa Blessing Fashion Centre, wakati akiwa ndani ya Banda la Benki ya NMB, akikagua mabanda ya maonyesho. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Mark Wiessinga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua moja ya Banda la Mjasiliamali wakati alipotembelea Banda la benki ya NMB. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...