Mjalojia wa mgodi wa madini ya uranium yaliyopo Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Bw Hashim Millongo,akiwafafanulia jambo madiwani wa halmshauri ya wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma juu ya usalama wa wananchi wanaoishi vijiji vya jirani na mgondi huo,madiwani hao walilazimika kwenda katika mgodi huo ili kujiridhisha kutokana na malalamiko mengi ya wananchi wa maeneno hayo.
Mjalojia wa mgodi wa madini ya uranium yaliyopo wilaya ya Namtumbo Ruvuma Bw kassim Millongo akiwaonesha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo mfuko maalum wa kuhifadhia mchanga wa madini hayo,kumekuwa na malalamiko mengi yanayotolewa na wananchi na mashirika ya kutetea haki za binadamu kuwa hakuna usalama wa kutosha kwa wananchi wanaoishi kwenye vijiji vya jirani na mgodi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo Bw Savery Maketta kushoto,akiwaonesha wajumbe wa kamati yake mchanga wenye madini ya uranium katika mgodi wa madini hayo yaliyopo katika kijiji cha Likuyuseka wilayani humo hivi karibuni.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Ruvuma,Bw Kassim Ntara kulia akizungumza jambo na madiwani wa halmashauri hiyo hawapo pichani,walipotembelea mgodi wa madini ya uranium yaliyopo katika kijiji cha likuyuseka wilayani humo, kwa lengo la kuona kama sza uchimbaji zimeanza kufuatia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya kuanza kwa kazi ya uchimbaji jambo ambalo siyo la kweli.Picha na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii,Ruvuma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2011

    Brown cake in Bongo...... Let's make Nuclear power plants to supply energy all over the country.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2011

    maelezo ya mwandishi yanaleta mkanganyiko zaidi kuliko kufanunua; mfano 1)kuhusu malalmamiko yanayotolewa na wananchi na taasisi mbalimbali kuhusu usalama wa wananchi wa maeneo husika.kwa mtazmo wangu hayo ni madini yenye kutoa mionzi hatari sasa kwann wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya usalama wao?na je wanahakikishiwa vipi usalama wao au hadi wadhurike ndo watasaidiwa?

    2)kuhusu kuanza uchimbaji-nani yu karibu na madini hayo zaidi ya hao wananchi ambao ndo kama mnavyowasikia wanalalamika..au mnataka wakae kimya huku watu wanahamisha mzigo?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2011

    Hivi uranuim huwa inashikwashikwa tuu kwa mikono namna hiyo? labda sina taarifa za kutosha kuhusu usalama wa madini hayo!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2011

    Anonymous no.2 hicho unachokiita mionzi haipo kwenye raw uranium ni mpaka iwe enriched, hiyo inaiongezea thamani mara X 100. Ni nchi chache sana zinafanya enrichment ya uranium hata zile tajiri kama Australia hawafanyi kutokana na risks.Hivyo basi hatari zaidi ya uchimbaji huo ni uharibifu na uchafuzi wa mazingira

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2011

    MOJA... NAOMBA KULALAMA KAMA HIVI....JAMANI JAMANI JAMANI X 1000. HII NI HATARI SANA. HAYO MADINI SIFA YAKE NI KURUSHA MIONZI INAYOWEZA KUSABABISHA SARAKANI (CANCER). HAPA NAONA WASOMI NA WASIOSOMA WANAYASHIKA KAMA MAANDAZI AU KARANGA. KUNA HAJA YA KUWAHAMISHA WANANCHI KWENDA ENEO JIPYA MBALI NA MADINI HAYA. NI LAZIMA SERIKALI IWEKE MIPAKA NA KUTANGAZA MARUFUKU KABISA KWA MTU YEYOTE KUWA NDANI YA ENEO HILI KWA FAIDA YAKO BINAFSI. JELA MIAKA 100 KWA MTUHUMIWA.

    MBILI...HAYA MADINI NI MALI GHAFI MUHIMU SANA KWA UZALISHAJI WA UMEME WA NUCLEAR PAMOJA NA MATUMIZI MENGINE KWA NCHI ZILIZOENDELEA. SERIKALI INAWAJIBIKA KUJENGA MTAMBO WA UMEME WA MIONZI KWA KUFUATA UTARATIBU MAALUMU WA KUWAOMBA UMOJA WA MATAIFA AU WAHESHIMIWA WAZUNGU RUKSA YA KUJENGA MTAMBO HUO KAMA ILIVYO KWA NCHI NYINGI ZA AFRICA( WE CANT DO NOTHING UNTIL WHITE MAN SAY GO AHEAD. TANZANIA HATUNA MPANGO WA KUJENGA BOMU LA NUCLEAR. TUNACHOTAKA SISI NI UMEME WA NUCLEAR NA WATAALAMU WAZAWA WAPO WA KUENDESHA MITAMBO HIYO- NA MIMI NI MMOJA WAPO. PIA TUNAO UWEZO WA KUSOMESHA VIJANA WETU ILI TUWE NA WATAALAM WA KUTOSHA KUENDESHA MITAMBO HIYO YA UMEME KWA USALAMA ZAIDI. WOTE TUNAJUA KWAMBA TATIZO LA UMEME NI KUBWA NA WAKATI WA KULITATUA KABISA KABISA UMEFIKA. TUNAO UWEZO KAMA NIA IPO THABITI..ISIPOKUWA HATUTAKI KULIMALIZA TATIZO HILI. NI AIBU KUBWA SANA KUONA TUNA MADINI MUHIMU KAMA HAYA HALAFU TUNASUBIRI MVUA ILI BWAWA LA MTERA LIJAE MAJI. LET US GET SERIOUS...UMEME WA UHAKIKA IS VITAL FOR COUNTRY DEVELOPMENT. TANZANIA TUNAJITAKIA UMASKINI...NA KOSA NI LA WANANCHI KUCHAGUA VIONGOZI WALE WALE MIAKA NENDA MIAKA RUDI HUKU WAKIBEBA BENDERA ZA UFISADI NA NCHI INA TOKOMEA KWENYE DIBWI LA UMASKINI. MA-GENERATOR YA WAHINDI HAYAWEZI KUTUPELEKA KOKOTENA HUU MGAO. NIPO NJE YA NCHI NA SIRUDI NG`O KWA SABABU YA UMEME WA MGAO NA HUDUMA DUNI ZINAZOSABABISHWA NA HILO...IMEFIKA MAHALA HATA MAJI BARIDI HAKUNA MPAKA UMEME URUDI....AIBU AIBU AIBU TUPU. MWEZI HUU NILISOMA MPANGO WA TANESCO KUTATUA TATAZO LA UMEME KWENYE HII BLOG YA MICHUZI... NA HAKUMA SEHEMU YEYOTE ILITAJA MPANGO WA KUZALISHA UMEME WA NYUKLIA...KWA SABABU WANAFURAHI KUONA WANANCHI WANALIA KILA SIKU NA UMEME WA KUBAHATISHA. IKULU INAHITAJI MGAO PIA ILI RAIS ATAMBUE UKUBWA WA TATIZO HILI. kama michuzi unaweza kuichapisha hii kitu hadharani...mpe John Mashaka likizo. I WILL SEE YOU AT THE WASHINGTON DC..DIASPORA GATHERING.

    SOLAR POWER IS ALSO POSSIBLE...TUSISUBIRI MVUA KILA SIKU

    MDAU UGHAIBUNI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...