Akina mama wanaojishughulisha na uuzaji wa biashara ya dagaa pembeni mwa soko kuu la songea wakiwa na biashara zao wakisubiri wateja kama walivyokutwa na mpiga picha wetu.
Kijana ambaye hakufahamika jina lake mara moja akiwauzia bisi (popcorne) abiria wa daladala inayofanya safari zake kati ya soko kuu na mkuzo manispaa ya songea ambapo alikuwa akiuza kwa shilingi 100 kila mfuko,uuzaji wa vyakula aina hii unaweza kusababisha madhara makubwa kwa wateja.
Mkazi wa manispaa ya Songea ambaye ni mlemavu wa miguu aliyefahamika kwa jina moja la Milanzi,akisoma gazeti lenye picha za wachezaji wa timu ya Yanga katika moja ya meza za kuuzia magazeti kandokando ya barabara ya sokoine manispaa ya songea.Picha na Muhidin Amri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2011

    Dah BONGO kichefu chefu sana yaani nikiona picha kama hizi inanipa huzuni sana.cheki huyo jamaa DISABLED yaani angalau angekuwa na wheelchair lakini wapi yaani shida tu Ehee Mungu tuhurumie.MBELE MBELE watu kama hao wanaangaliwa sana Full huduma zote wanapata lakini kwa hapo Nyumbani Mhhh mimi sijui!!!

    ReplyDelete
  2. Brother michu
    Now you are talking. Taswira za mikoani zinavuta hisia sana, zinatufunulia vitu amabavyo havipewi nafasi kuonekana.
    Issue za temeke , Kinondoni na Ilala zimezidi. Ntakutumia picha kama hutozi pesa za maisha ya kila siku majumbani au mitaaani kama Rorya vijijini au Magu vijijini. Huwa nina access na huko sana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2011

    BMW nyeusi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2011

    "Taifa litajengwa na sisi vijana" Hebutujaribu kuangalia kauli hii kama iliweza kuwa na manufaa enzi zile, itaweza kuwa na manufaaa enzi hizi au imepitwa na wakati? Katika maeneo mbalimbali mikoa ya wenzetu kwa vijana waliokamata mpini wamekuwa ni chachu ya maendeleo huko walikotoka!Hata ukiangalia mataifa ya wenzetu mambo ni hivyo kiasi kwamba wameweza kufikia hatua ya kuunda urafiki na baadhi ya majimbo, viji, na hata miji ya hapa Tanzania. Sisi je?
    Inatupasa kuwasaidia watu kujenga maarifa ya namna pesa inavyoweza kupatikana, huo ndio msaada endelevu. Kumsaidia mtu kwa kumpatia fedha ni sawa na kumuangamiza....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...