Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipeana mikono  na Mh. Anne Kilango-Malecela,mke wa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela (wa pili kulia) ambaye pia anaagana na mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, baada ya mazungumzo wakati walipofika nyumbani mstaafu huyo mjini Dodoma, baada ya kurejea kutoka India ambako alifanyiwa upasuaji. Hali yake inaendelea kuimarika
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu John Malecela, alipofika kumjulia hali nyumbani kwake mjini Dodoma.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal (kulia) akifurahia jambo na Mh. Anne Kilango-Malecela, mke wa  Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, Mzee John Malecela,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, John Malecela na mkewe, Anne Kilango, wakati Makamu alipofika nyumbani kwa Malecela mjini Dodoma jana Julai 29, kwa ajili ya kumjulia hali baada ya kufanyiwa upasuaji nchini India hivi karibuni.  
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2011

    Ooh! mzee malecela ugonjwa umemchukua amepungua sana, mwenyezi mungu amrejeshee afya yake haraka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2011

    mzee malecela amefanyiwa upasuaji London sio India,na upasuaji mkubwa wa moyo sio mchezo kilo lazima zipungue sana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2011

    Yes indeed, open heart surgery sio mchezo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2011

    ina maana mzee malecela ni mtakatifu kweli maana duh angalia sofa hizo hapo ingekua zile nyumba za mafisadi mungeshangaaa kweli hapa maana kuko kwa kawaida kabisa nyumbani kwake
    mungu atakusaidia upone haraka hili uweze kuendelea kulitumimikia taifa letu

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 31, 2011

    Wewe mdau wa juu hapo umbeya umekuzidi mdogo wangu. Unaangalia mpaka design ya makochi?

    Muombee apate unafuu na siyo kutoa comments kuhusu sofa sets zake.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 31, 2011

    Si umbea huo ni ukweli ingekuta mafisadi ungefikiri ndo kwa rais na si makamu au waziri. Mafisadi kwao utadhani kwa Queen. Halafu mnadhani nchi itakuwa tajiri,au migomo vyuo vikuu itaisha. Au maandamano ya CHADEMA yataisha huku kuna watu hata mlo mmoja ni shida na eti nchi yetu yenye resource kila kona leo inaomba misaada nje hapo hapo mafisadi wakiendesha magari ya mabilion kwanini hata mafisadi wasiwasaidie maskini, yatima na wajane? nao wakawa na charity? Pole babu tunakupenda na kukuombea Mwenyeenzi Mungu akuponye.

    ReplyDelete
  7. we apo juu mshamba kweli, na ndo aana maendeleo yanakua tabu kwetu...mtu akiwa tajiri anaitwa fisadi...kwani kununua gari zuri na nyumba nzuri lazima uibe hela za watu? hata viongozi wa serikali wanapata mishahara na stahili zao nyingine, wengine wanatumia fedha zao vizuri wanawekeza, wananunua hisa mwishowe wananeemeka...sasa Tanzania ukionekana umejikwamua kiuchumi na ni kiongozi basi unaidhaniwa fisadi..badili mtazamo ndugu yangu!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...