![]() |
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh. Juma Duni Haji |
NA NAFISA MADAI MAELEZO ZANZIBAR
SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa umoja wa kitaifa imesema haina nia ya kujivua gamba katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wake na kuwaachia watu wa sekta binafsi kwani bado malengo yake juu ya utoaji huduma ya afya yapo pale pale.
Hayo yamelezwa na Waziri wa Afya, Juma Duni Haji alipokua akifungua hospitali ya Dkt. Mehta iliyopo Vuga Mjini Zanzibar ambapo alisema nia ya Dkt. Metha kufungua hospital hiyo ambayo itatoa huduma zote za matibabu na uchunguzi ni jambo la msingi sana kwani itaweza kuwaokoa wanzanzibar wengi.
Aidha alisema katika kipindi kilichopo hivi sasa ni cha kuimarisha huduma za afya imekua ni kapaumbele cha serikali ya umoja wa kitaifa lakin kuongezeka kwa hospital binafsi nako pia kutawafanya wanzazibar wawe na chaguo walipendalo katika kutafuta huduma.
Hata hivyo alisema licha ya kutoa fursa kwa wananchi kuwa na chaguo la kutafuta huduma wanapopenda,lakini pia kuimarika kwa sekta ya afya kutafanya hata watalii wanapokuja kutembelea visiwa vya zanzibar watakuwa na uhakika wa kupata huduma za afya zilizo katika kiwango kilicho bora.
Akitoa wasifu wa Dkt. Mehta waziri huyo amesema Dkt. Mehta ni mmoja kati ya wazanzibar wenye uzalendo wa hali ya juu kwani kutokana na utaalamu aliokuwa nao angeweza kufungua hospital yenye daraja la juu nje ya zanzibar na akaweza kupata faida zaidi.
Waziri duni amesema kuwa vitu ambavyo vimekuwa vikiumiza kichwa Serikali ni kutafuta mbinu mabalimbali za kuhakikisha wale kina mama wanaokwenda kujifungua hawalipishwi senti nyekundu kwa vile hali ya maisha ya wazazi na jamii yenyewe ni ya kimaskini sana na kuzaa ugumu wa kuweza kulipia huduma hiyo.
kwa upande wake Dkt. Mehta amesema lengo la kufungua hospitali hiyo ni kuwarahisishia wanzanzibar kupata huduma za afya ambao wengi wao walikuwa wakifuata huduma hiyo Nairobi,Tanzania Bara na kwenginenoko ambako harama huwa kubwa zaidi.
Aidha alisema kurudi kwake zanzibar ni kuja kuwasaidia wanzanzibar wenzake na sio kibiashara zaid kama livyo katika hospital nyengine kwani yeye ni mzanzibar halisi ambae anafahamu hali ya maisha ya watu wa zanzibar.
Hata hivyo alisema hospital yake itahakikisha inatoa huduma zote muhimu katika maisha ya mwanadamu kama vile huduma ya X ray, Ultra sound, in pantient, huduma za meno na viungo na pia huduma za magonjwa ya kike katika kipindi kifupi kijacho
Dkt. Mehta alisema pia katika siku sitini ataweza kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje kufuata huduma hizo kwani atakuwa tayari amepata wataalamu ambao wataweza kutibu maradhi sugu kama moyo, figo pamja na upasuaji.
akitaja harama za ujenzi, ukarabati katika baadhi ya jengo la hospita hiyo pamoja na vifaa amesema mpaka kukamilika kwake ametumia dola za kimarikani milioni mia moja na hamsini.
Nae naibu katibu mkuu katika ofisi ya raisi ikulu inayoratibu shughuli za watu wanaoishi nchi za nje Said Natepe, amesema kuwa rais wa zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein lengo la kuanzisha ofisi hiyo ni wanzaznibar wanaoishi nje wanakuja kuwekeza zanzibar na sio kwengine kwa lengo la kusaidia kimaisha.
Amesema kuwa mfano alionesha dr mehta unafaa kuigwa na kila mzanzibar mwenye uwezo anaeisha nje kwani umekua ukionesha faraja kubwa kwa wanzanzibar ambao wana hali ya nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...