Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  akiongozwa kukagua meli ya Ocean Rig Poseidon baada ya kuizindua  kwenye bandari ya Mji maarufu kwa ujenzi wa Meli kubwa wa Geoje nchini Korea ya Kusini Julai  8, 2011. Meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Petrobas ya Brazil inatarajiwa kufanya utafiti wa mafuta na gesi kwenye pwani ya mtwara na Mafia miezi michache ijayo.
  Mama Tunu Pinda  akiongozwa akikagua meli ya Ocean Rig 
 Mama Tunu Pinda akizindua meli ya Ocean Rig Poseidon kwenye bandari ya Geoje nchini Korea ya Kusini  leo. Meli hiyo  mali ya kampuni ya Petrobas ya Brazil inatarajiwa kuwasili nchini miezi michache  ijayo ili kufanya utafiti wa mafuta katika Pwani ya Mtwara na Mafia
 Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  akikagua meli ya Ocean Rig Poseidon baada ya meli hiyo kuzinduliwa na Mama Tunu Pinda kwenye Bandari maarufu  kwa ujenzi wa meli kubwa ya Mji wa Geoje nchini Korea Kusini  Julai 8, 2011. Meli hiyo mali ya Kampuni ya Petrobas ya Brazil inatarajiwa kufanya utafiti wa mafuta na gesi kwenye pwani ya Mtwara na Mafia miezi michache ijayo
Mama Tunu Pinda akihutubia baada ya  kuzindua meli ya Ocean Rig Poseidon kwenye bandari ya Geoje nchini Korea ya Kusini Julai 8, 2011. Meli hiyo  mali ya kampuni ya Petrobas ya Brazil inatrajiwa kuwasili nchini miezi michache  ijayo ili kufanya utafiti wa mafuta katika Pwani ya Mtwara na Mafia
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa katika mzungumzo na viongozi  waandamizi walioshiriki katika uzinduzi wa malei ya kukufanyia utafiti wa mafuta na gesi katika  pwani ya Mtwara na Mafia kabla ya uzinduzi uliofanywa na Mama Tunu Pinda katika mji maarufu wa uundaji meli wa  Geoje nchini Korea Kusini leo. 
Picha na mdau Hilary Bujiku wa Ofisi ya Waziri Mkuu


=============================

Pinda aalika wawekezaji katika gesi asilia


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema umefika wakati kwa wawekezaji wa kimataifa kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika miundombinu ya kusafirisha gesi asilia kama njia mojawapo ya kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania.

Amesema kupatikana kwa gesi nyingi katika ukanda wa pwani ya kusini mwa Tanzania kunatoa fursa ya wawekezaji kuanza kufikiria ujenzi wa mabomba ya gesi ili bidhaa hiyo iweze kutumika viwandani, kuendesha mitambo pamoja na viwanda.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Julai 8, 2011) kwenye hoteli ya Samsung mjini Geoje, wakati akiwahutubia wageni maalumu kutoka makampuni mbalimbali ya wawekezaji walioalikwa kuhudhuria uzinduzi wa meli ya uchimbaji mafuta iitwayo Poisedonkatika bandari ya Geoje, iliyoko kusini mashariki mwa Seoul, mji mkuu wa Korea Kusini.

“Tangu mwaka 1974 ilipogunduliwa gesi asilia katika kisiwa cha Songosongo katika pwani ya kusini mwa Tanzania, kumekuwa na ugunduzi mbalimbali kutokana na tafiti zilizofanywa na makampuni ya nje kwa kushirikiana na TPDC.”

“Miaka kadhaa baadaye, iligungulika akiba kubwa ya gesi asilia huko Mkuranga karibu na Dar es Salaam; ikafuatia Mnazi Bay mwaka 2007; Kiliwani mwaka 2008; na sasa kampuni ya Ophir kwa kushirikiana na kampuni ya British Gas wamegundua visima vitatu maeneo ya Mtwara… hii ni dalili njema kuwa Tanzania ina hazina (reservoir) kubwa ya gesi na mafuta,” alisema.

“Chini ya sera yetu ya mwaka 2010 ya Ushirikiano baina ya Umma na Sekta Binafsi, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na sekta binafsi, makampuni ya uchimbaji mafuta na gesi itabidi tutafute njia za kuleta ufanisi ili ugunduzi huu uweze kuimarisha sekta ya mafuta na gesi kuendeleza uchumi wa nchi yetu,” alisema.

“Kutokana na mipango ya baadaye tuliyonayo, sekta binafsi haina budi kujitokeza na kuangalia ni maeneo gani wanaweza kuwekeza katika uchimbaji mafuta na gesi na kwa kuanzia wanaweza kungalia usafirishaji wa gei na usambazaji wake, viwanda vya mbolea, kuleta magari yanayotumia gesi au kutengeneza injini za gesi zinazoweza kuzalisha umeme,” alisema.

Alisema hayo ni maeneo machache ambayo wanaweza kufikiria kuanza nayo katika uwekezaji wao wenyewe kama sekta binafsi au kwa kushirikiana na Serikali.
Kwa upande wa Petrobras, kampuni ya Brazil ambayo itaendesha utafiti nchini Tanzania, Waziri Mkuu alisema ana matumaini na kampuni hiyo kama mbia makini kutokana na historia ambayo imejiwekea duniani tangu mwaka 1952 ilipoanzishwa.

“Nimeambiwa kwamba mwaka jana, kampuni ya Petrobras ilikuwa na uwezo wa kuzalisha mapipa zaidi ya milioni mbili ya mafuta kwa siku… vilevile ni kampuni inayojulikana kwa kutumia teknolojia za kisasa kuzalisha mafuta kwenye maji ya kina kirefu,” aliongeza.

Mapema leo asubuhi, mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda na Bibi Anne Tollefsen walipewa kazi ya kubatiza meli mbili (kuwa mama wa ubatizo) zilizozinduliwa leo na kukata kamba kwa shoka kuashiria kutoa nanga kwa meli hizo. Meli hizo ni Poseidoninayokuja Tanzania na Mykonos inayoenda Brazili.

Mama wa ubatizo huteuliwa na kampuni inayomiliki meli, kwa hiyo walimteua Mama Tunu Pinda awe mama wa ubatizo wa meli ya Poseidon, na Bibi Anne Tollefsen awe mama wa ubatizo wa meli ya Mykonos. Bibi Tollefsen ni mke wa Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Ocean Rig, Bw. Frank Tollefsen kampuni ambayo inasimamia ujenzi wa meli hiyo.

Leo mchana, (Ijumaa, Julai 8, 2011) Waziri Mkuu atatembelea eneo la Georim lenye viwanda vya kusindika mazao ya kilimo katika mji huu wa Geoje.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amefuatana na mkewe Mama Tunu Pinda, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Bibi Salome Sijaona, Balozi wa Brazili nchini Tanzania, Bw. Francisco Carlos Luz, Mwenyekiti wa TPDC, Jenerali Mstaafu, Robert Mboma na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Bw. Yona Kilagane.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, JULAI 08, 2011.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2011

    MIMI BADO SIJAELEWA NI MILA AU NI KWANINI MELI MPYA LAZIMA IZINDULIWE NA MWANAMKE,1979 NILISHUDIA KWENYE NCHI YA KIKOMUNIST WAKATI HUO PORT COSTANSA RUMANIA,1984 TULIFUTA MELI MPYA SINGSPORE KUTOKA UMANGANI(UGIRIKI)MV TRITON COSTAMAREIY COMPANY BONGE LA DUDE ALIEVUNJA SHAMPENI NA KUKATA UTEPE NI MWANAMKE NIKAMUULZA CAPTAIN AKASEMA LAZIMA MWANAMKE AFUNGUE MELI HAKUNIPA SABABU,KUNA ANAEJUA NI KWANINI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2011

    Hii imekaaje! kwa nini mama WM na pia akatoa hotuba.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2011

    Kama ndiyo utaratibu kwamba lazima meli ifunguliwe na mwanamke, hivi hatukuwa na waziri mwanamke (Mf. Mary Nagu, Anna Tibaijuka, Gaudencea Kbaka, n.k) ambaye angeenda kufungua rasmi hiyo meli kwa niaba ya serikali? Nafasi ya mke wa waziri mkuu kwenye serikali ni ipi????? Bongo bwana hata wake za wakuu wa wilaya na makatibu kata wataanza kwenda kufungua miradi ya serikali!! Bongo tambarare!!

    Mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2011

    Mimi mambo ya kwa nini meli kufunguliwa na mwanamke siyajui.

    Ila ninachoomba mnisaidie ni kuhusu utata uliopo juu ya mafuta tanzania bara. Nashindwa kuelewa kuwa mafuta yameshapatikana kinachosubiriwa ni uchimbaji tu au bado makampuni yapo kwenye utafiti? Sasa hilo limeli ni la uchimbaji au ni la utafiti? Na hiyo meli ni mali ya Tanzania au ni mali ya makampuni ya kutafuta mafuta?

    Na kama mafuta yamepatikana, kwa nini serikali ya Tanzania haiweki wazi? Mbona masuala ya gesi yamewekwa wazi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2011

    misupu mtumie hii picha joh mashaka. hata mie hawa watu wa asia siwapendi kabisa, wanatuharibia nchi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...