Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kufungua msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/2012 kati ya Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe Agosti 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa itafanyika Agosti 17 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.

Uamuzi huo umetokana na timu ya Taifa (Taifa Stars) kuwa na mechi ya kirafiki katika kalenda ya FIFA (FIFA dates) ugenini itakayochezwa Agosti 10 mwaka huu dhidi ya Palestina. Stars itarejea nchini Agosti 11 mwaka huu baada ya mechi iyo.

Wachezaji wengi wanaounda kikosi cha Taifa Stars kwa sasa wanatoka katika klabu hizo mbili. Awali Stars ilikuwa icheze mechi nyingine Agosti 13 mwaka huu jijini Amaan wakati aikitokea Palestina. Kocha Mkuu wa Stars, Jan Poulsen ameifuta mechi hiyo kwa vile Jordan haitakuwa na wachezaji wake wa kulipwa kutokana na kuwa nje ya kalenda ya FIFA.

FAINALI LIGI YA TAIFA
Fainali ya Ligi ya Taifa itakayoshirikisha timu 12 zitakazogawanywa katika
makundi matatu ya timu nne nne itafanyika Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga
kuanzia Agosti 6 mwaka huu.

Awali ligi hiyo ilianza katika vituo vinne ambapo timu tatu za juu ndizo
zilizopata tiketi ya kucheza fainali. Kituo cha Pwani kimetoa timu za
Cosmopolitan (Ilala), Sifapolitan (Temeke) na Mgambo Shooting (Tanga) wakati Samaria (Singida), Majengo SC (Dodoma) na Morani (Arusha) zimefuzu kutoka kituo cha
Singida.

Police Central (Ilala), Small Kids (Rukwa) na JKT Mlale (Ruvuma) zimefuzu kutoka kituo cha Rukwa wakati kituo cha
Kigoma kimetoa timu za Kasulu United (Kigoma), Geita Veterans (Mwanza) na Rumanyika SC (Kagera).

Timu zinatakiwa kuwasili Tanga siku mbili kabla ya fainali kuanza ambapo mshindi wa kwanza katika kila kundi pamoja na washindwa bora (best losers) wawili watapanda hadi daraja la kwanza.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2011

    KWA MTAZAMO WANGU MECHI ZA SIMBA VS YANGA ZINGEFUTWA KABSAAAAAAA
    ZINALETA MENGI MABAYA KULIKO MAZURI AMBAYO WAPENDA SOKA TUNGETEGEMEA KUYAONA FIKIRIA MAJUZI TU KWENYE MICHUANO YA TUSKER SIMBA KAFUNGWA IMEKUWA NONGWA SIMBA WAMETIMUA WACHEZAJI WAO KADHAA.WANASAHAU KUWA HIYO NI KAZI YA KUDUMU YA WACHEZAJI NA KUWA WANAISHI NA KULISHA FAMILIA ZAO KWA KAZI HIYO.BILA KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA MTU ANAMTIMUA KAZI MBAYA ZAIDI PASIPO KUZINGATIA UTAALAMU WA FANI HUSIKA.INATIA UCHUNGU WATATIMULIWA WACHEZAJI WANGAPI KILA INAPOTOKEA TIMU MOJA KUIFUNGA NYINGINE.

    TIMU ZIENDESHWA KISAYANSI KWA KUZINGATIA MAONI YA WATAALAM ZIO MTU M1 ANAKURUPUKA TU NA KUSEMA FULANI KAHUJUMU.SOKA HAIENDI HIVYO.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2011

    mchangiaji wa mwaanzo inaonyesha sio mtu wa mpira. watu wanafurahia mpira wewe unasema mechi zifutwe. inabidi upelekwe ukapimwe milembe. kama mechi zingekuwa zimefutwa Watanzania tungepata wapi heshima na furaha katika soka kama tuliyoipata. kama kufutwa ifutwe Simba maana ni dhuluma na hujuma sana. TFF hata kama mkisogeza mbele muda wa mchezo kipigo ni kile kile. lazima mnyama auwawe!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...