Na Nurdin Ndimbe,Mwanza.

Warsha ya kujadili maendeleo ya mradi wa Hifadhi ya Mazingira katika Ziwa Victoria imeanza Jijini Mwanza kwa Wadau kujadili maendeleo ya Mradi Mkubwa wa Kuhifadhi mazingira katika Ziwa Victoria (LVEMP).

 Akizungumza katika ufunguzi wa Warsha hiyo, Mkurugenzi msadidizi Idara ya Rasilimali ya Maji katika Wizara ya Maji Bwana Sylvester Matemu allsema kuwa lengo la warsha ni kupitia malengo ya mradi na kujua mafanikio yaliyopatika katika kipindi cha miaka miwili ya utekelezaji wa mradi huo katka awau ya pili.

 “Kama mnavyofahamu Mradi huu mkubwa sasa unafikia miaka miwili hivyo lazima tufanye taathimini ya maafanikio na changamoto tulizozipata katika kutekeleza malengo yaliyokubaliwa “ alisema Mkurugenzi huyo .’’

 Ni matumaini yangu kuwa, warsha hii itatufungulia njia ya kujipangia malengo mapya na kujiwekea mikakati ya kuyatekeleza ili kufanya mardi huu wa hifandhi ya Mazingira katika Ziwa Victoria kuwa endelevu kwa wanchi wetu’’ alisisitiza Bwana Matemu.

Mradi wa Hifadhi ya Mazingira katika Ziwa Victoria (LVEMP II) ulianza kutekelezwa rasmi na Nchi za Uganda,Tanzania na Kenya ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na matumizi endelevu ya rasilimali ya maji,utunzaji wa mazingira na rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria inakuwa endelevu kwa Wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Mraunfadhiliwa na Nchi wanacha pamoja na Mashirika ya Fedha ya Kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...