Kaka Michuzi pole na majukumu na kazi nyingi na tunashukuru kwa kazi nzuri unayoifanya japo nayo inamatunda mengi ya kila aina, nami leo najitokeza naomba unisaidie kuniwekea kwenye blog yako ninaamini wapo wa Tanzania wengi wenye shida kama yangu ila tunaogopa kuwa wa wazi.
Niko serious sana Natafuta mchumba ila awe mtu mzima kuanzia 33-44 mwenye hekima, busara na upendo wa dhati na anaejua definition ya mke nini. Pia kama hajamaliza starehe za dunia za kupenda wanawake asiniandikie - kuna janga la ukmwi sitaki, nataka mtu wa kutulia ili tujenge maisha kwa raha na tabu.
Niko serious sana Natafuta mchumba ila awe mtu mzima kuanzia 33-44 mwenye hekima, busara na upendo wa dhati na anaejua definition ya mke nini. Pia kama hajamaliza starehe za dunia za kupenda wanawake asiniandikie - kuna janga la ukmwi sitaki, nataka mtu wa kutulia ili tujenge maisha kwa raha na tabu.
Napenda awe Mkristo aliye na hofu ya Mungu ndani yake. Awe amesoma walau elimu ya chini awe na diploma angalau awe na kabachela hivi kwa umri huo. Aawe muajiriwa eidha katika shirika au serikalini kama ana mtoto mmoja sio mbaya wasizidi. Awe tayari kupima ukimwi zaidi ya mara 3. Awe muwazi.
Mimi ni muajiriwa katika shirika moja hapa jijini dar sina mtoto niko tayari 32yrs. Ni Mkristo-Lutheran, Mchaga.
Kwa maelezo zaidi atakae kuwa tayari tutafahamishani na naomba email kwa yule tu aliyeko serious na kwa atakayeponda ni sawa tu. Na nitashukuru kwa yule atakayenishauri na pia kuniombea ili niweze kufanikisha maana najua kwenye kila jambo Mungu ndiye muweza wa yote.
email yangu aneth079@live.com
Kwa maelezo zaidi atakae kuwa tayari tutafahamishani na naomba email kwa yule tu aliyeko serious na kwa atakayeponda ni sawa tu. Na nitashukuru kwa yule atakayenishauri na pia kuniombea ili niweze kufanikisha maana najua kwenye kila jambo Mungu ndiye muweza wa yote.
email yangu aneth079@live.com
NI VIZURI UMEWEKA WAZI HITAJIO LAKO KATIKA UBAO HUU WA MATANGAZO NINA IMANI MUNGU ATAKUJALIA UTAPATA UNACHOKITAFUTA. WATU WENGI WANAHOFIA KUFANYA HIVYO WAKIDHANI NI KUJIDHALILISHA LAKINI UKWELI NI KWAMBA HAKUNA KAZI NGUMU KAMA KUTAFUTA MCHUMBA HUSUSANI IKIWA WEWE NI MWANAMKE UNATAFUTA MWENZA. KWA MILA NA DESTURI ZETU TUMEZOEA KUONA KUWA MWANAUME NDIYE ANAFANYA KAZI HIYO, LAKINI KWA KIZAZI CHA SASA AMBACHO KIMEJAA KILA AINA YA HILA, UDANGANIFU, MAGONJWA, UCHUMI DUNI, "HIT AND RUN" NA PIA UKIZINGATIA KUWA KWA TAKWIMU ZA SASA WANAWAKE NI WENGI KULIKO WANAUME, NI VEMA NA DADA ZETU KAMA ULIVYOFANYA WEWE UKATAFUTA KWA STYLE HII. USISUBIRI KUTAFUTWA TU. HONGERA NA NAKUTAKIA KILA LA KHERI, NINGEKUWA SIJAOA NINGEKUFIKIRIA NA MIMI NILIPATA KWA STYLE AMBAYO INAKARIBIANA NA YA KWAKO
ReplyDeleteWewe ujanani kwako ulikula na nani sasa hivi ndio wataka kuwauwa watoto wa wenzako
ReplyDeleteMungu akupe sawa na hitaji lako.
ReplyDeleteaaah! anony wa pili uwe mstarabu basi kwani umesikia huyu anataka kumuua mtu hafu ujana gani unaosema weye si amesema ana miaka 32 mbona ni umri halisi wa ndoa ukizingatia yeye alikuwa shule na sasa yupo kazini na yuko tayari kupima x3 (ngoma) au umesikia mchawi.nadhani usiwakatishe tamaa wanataka kumchukua huyu dada kwa dhati zao.Si mtu mzima sana au ilitaka aseme ana miaka 22.haya dadangu mchakato mwema utapata mwenzio.Mimi nshaoa mwakajana ningekuwa bado weye ningekutafuta tu.Nikumbuke kt sala zako.
ReplyDeleteIna maana wewe una bikira au ...Mkuki kwa nguruwe ...
ReplyDeleteWewe unatafuta mchumba mwenye sifa hizo na masharti kibao, Je, wewe mwenyewe sifa hizo unazo?
ReplyDeleteAhhhh mr michuzi hongera kwa kutupatia habari,burudani,kuhabarisha mimi niseme tu huyo dada amefanya uamuzi mzuri sana wa kuweka bayana hisia zake kuliko kuficha basi namtakia utafuataji mwema.Pia bila kusahau wanaume ni wachache wanawake wengi so wasiwe na pozi sana.
ReplyDeleteMimi nimevutiwa na wewe lakini ningeona alau picha mvuto ungezidi. Je upo tayari kuhamia Zanzibar? Pia uko tayari kuwa mke wa pili? Nina shahada ya uzamivu katika fani ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
ReplyDeleteKatika dini/kabila nyingine wanawake ndio hutafuta wachumba na wanaposa sio mambo ya ajabu. Utamaduni wa kizungu wa kungojea kutongozwa na mwanamume mutembeeeeee, na kudokoa visivyodokoleka pengine na kuzaa, mtu anavaa shela, leo kesho anazaa, sio utamaduni wa kiafrika au wa dini zote hata kidogo. Mwanangu hujakosea ni sawasawa ulivyofanya achana nao vijana wetu wa siku hizi ni ignorant kabisa, they have no knowledge of their culture seuze za watu wengine na hawasomi vitabu vihusianavyo na jamii ila hii globu na magazeti ya udaku. BRAVO GIRL.
ReplyDeletemungu akupe sawa na hitaji la moyo wako dada
ReplyDeleteHuyu dada muunge
ReplyDeletewana, muwazi, na anajua wapo akina anonymous wa pili! Nawashauri wanaume wanaotafuta wake wema, waelewa, hapa ndipo pake. Ni bahati mbaya sana tu hajakutana na wake live ktkt pilikapilika za maisha ilia sishangai kwani hata mimi niliyekutana naye nikajiuliza walimwengu walikuwa wapi kumuona huyu! Nikajua Mungu ndiye ajuaye. Mwaka jana tu nimejifunga kwa ahadi. ingekuwa bado, sure ningeapply kwani na qualify kwa mengi na ambayo sio angenielewa na kuwa 100% candidate.
Kila la kheri rafiki
Bora wewe unajitafutie mchumba. Wenzako wa umri huo walishahamua kuwa vimada na kuharibu ndoa za watu
ReplyDeleteusijali dada mingu atakuletea mume mwema na uliyemtarajia kumbuka kusali na kumuomba mungu kwa hilo ili akufanyie wepesi kwenye jambo hilo.Kila la kheri mamii
ReplyDeleteDuh! Watu hao wanapatikana kwa Lusekelo, Kakobe na Rwakatare!
ReplyDeleteusioe usiyemjua ndugu yangu utajalia kilio cha mbwa.yaani huna uliosoma nao,uliokua nao unaosali nao au wasichana majirani,au unaofanya nao kazi au biashara unaowajua kwa muda hadi uparamie kusaka kwenye mtandao?.
ReplyDeleteKama kweli huna basi na wewe una matatizo kuna kitu unakimbia hao wanaokujua ili uoe asiyekujua sababu unajua hao wanaokujua lazima watakukataa kutokana na madhaifu wanayoyajua kwako ambayo wa mitandaoni hawayajui.Unasaka wasiokujua ili waingie mkenge.
kutafuta mke au mume mtandaoni si njia nzuri hata kidogo.
Kwa nia yako njema dada utafanikiwa, ila tu uwe makini kuchuja hasa, usitumie kigezo cha afya tuu, wapo play boy kibaoooooooo. Otherwise, umetumia vema mtandao huu hope you will not regret!
ReplyDeleteDada anaonesha imani yake katika kristo ni hafifu, mkristo gani anatafuta badala ya kumwomba Mungu amwezeshe kwa hilo wala na yeye hana hofu na mungu anayemsema anamwamini, namshauri asitumie ukristo.
ReplyDeleteDUNIA SASA UMEKWISHA NAONA HUYU MWANAMKE ANATOA MASHARTI YEYE KWAKUMTAFUTA MCHUMBA. KWELI ISHARA ZA MWISHO WA DUNIA UTASIKIA NA KUONA MENGI. HUYU DADA KAKATA TAMAA MAPEMA SANA YANI ANAONEKANA IMANI YAKE NI NDOGO SANA WALA SIO MWANAKE WAKUWEKA NDANI .ANGELIKUA WA MAANA ANGELIKUWA AMEOLEWA KITAMBO LAKINI BADO ETI ANATUFUTA MCHUMBA KWENYE LIBENEKE NA MASHARTI KIBAO ANAONEKANA MKOROFI HUYU DADA. mdau toka buja
ReplyDeletemimi nipo tayari na matakwa yako lakini tatizo ni moja mimi ni muislam sasa kama unatafuta wagalatia basi itakuwa umekosa nafasi kwangu maana nipo tayari kuishi nawewe mpaka mwisho wa maisha yetu ila tu utoke huko roma italy uhamie kwenye uislam na uachane na dini za biashara.
ReplyDeletemujahidina.
Kumbe kichwa kinasema unatafuta mchumba mimi nilifikiri unatafuta mume kumbe unatafuta mchumba.Wachumba mbona wako kibao kupata waume ndio kazi.
ReplyDeleteKama lengo lako ni kupata wachumba utawapata wengi hadi ukinai.wako mabarabarani,mitandaoni kila kona wamejaa.Nafikiri hata email yako itakuwa imejaa.
Ukitowa mashati na wewe ukubali masuruali. Jee na wewe ukotayari kupima vvux12 kwa mwaka katika kipindi cha uchumba?
ReplyDelete1 si vibaya njia uliyo tumia ila kwa masharti yko unaonyesha ww unakasolo ahuko sahihi kwa na mna yyte ile wtu cku izi awahangalii tena helimu wanahangalia ana pesa wenye helimu wanatumwa na wasio na helimu au unamtaka mwenye helimu mubonge ung`eng`e ndani hallo baby ...hello honey nakupa pole kwa masharti ayo utachuna sna kwa ushauri wa bule nenda kwa kakobe peter apa italy
ReplyDeleteKuna tatizo hapa. Huyu dada ni dictator. Alishakuwa nao wengi wamemshindwa. Kuwa flexible utafanikiwa
ReplyDeletewatanzania bwana, mtu anatafuta mchumba nyie sababu nyingi mara mtandaoni sio vizuri inamaana wote tunatumia mtandao hatufai kuwa waume? wangapit mlipata watu sehemu tu nzuri kama kanisani, shuleni ila kwa sasa wanawatenda. mtandao ni sehemu tu ya maisha kwa sasa inayotakiwa itumiwe vyema.
ReplyDeletekila la kheri ila uwe makini maana bongo uchumba una mambo siku hizi.
Kuna wadada mashujaa....
ReplyDeleteI got be honest nimesoma almost comments zote so far naona sio mbaya wala nini. Kwahiyo watz naona tunastaarabika....
ReplyDeleteMi kwa jinsi fulani nakubaliana na yule aliyeuliza kwamba huna marafiki kutoka shule, majirani, kanisani, kazini, biashara. C'mon I am sure umeshaonana na watu ambao unaona wanafaa...
The other thing if you meet someone and you feel he is a good man, not married of course usiogope kuonyesha interest. Give them compliments, ask to go lunch or dinner together, usiogope,narudia tena usiogope kama umempenda mtu kumwambia umempenda..
my two cents
KIla la heri dada.Njia haiko moja tu kila mtu anapitia njia yake katika kusaka kile anachokitafuta.Hayo masharti ni ya kawaida na ndiyo chaguo lako. KUPANGA NI KUCHAGUA. muombe sana Mungu akuwezeshe kumuona unayemhitaji.Usikatishwe tamaa na wanaokuponda kwani na wao hawana lolote ni walewale wanaosepa huko mitaani tu.
ReplyDeleteMungu Akupe hitaji la moyo wako dadangu wala usikatishwe tamaa.asante kwa kuwa mwazi ni wachache kama wewe wengi ni waongo sana.Pia uwe unaongea na Mungu usiku saa tisa atajibu maombi na kukuletea mtu wa jinsi utakavyo.all is possible wen u believe.all the best dear one.
ReplyDeleteZidi kuomba Mungu atakusaidia, usiwajali hao wanaokucrush, ndo kawaida ya waswahili.
ReplyDeleteMmmh, ungeweka na picha yako ingekuwa poa kweli ili mtu uweze kujudge upeleke application au la, vinginevyo ni mbuzi kwenye gunia!!!!!
ReplyDeletehi. ninatafuta mwanaume mwenye mapenz ya kweli nimpe moyo wangu. in short nina miaka ishirin na tano. ninakadegree kamoja na nimuajiriwa. i hav seen people find their soulmates through this media. naomba awe mkristu. umri kwangu doent matter as miaka ni numbers..my email is jullunjr@g mail.com
ReplyDeleteNatafuta mke umri kuanzia miaka 23 had 30...Mim Nina miaka 28..ni mwalimu WA shule ya msingi...tuwasiliane 0744903557..nipo ruvuma
ReplyDeleteKwa Hiyo Nyie mnaosema hana watu wa kanisani au nyumbani. Kwani Nyie mmefanana ao mahitaji zenu
ReplyDelete