Marehemu Danny Mwakiteleko (kulia) alikuwamo katika msafara wa Jukwaa la Wahariri walioenda Arusha wiki iliyopita kwa semina iliyoandaliwa na Serengeti Breweries.
Hapa wahariri wakifurahia jambo walipopumzika kwa muda wakiwa njiani kurejea Dar. Danny yuko nyuma kabisa kule

Marehemu Danny Mwakiteleko enzi za uhai wake
Rais Jakaya Kikwete, akimpa pole Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Coperation, inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba na Bingwa, Danny Mwakiteleko alipomtembelea jana jioni katika chumba cha wagonjwa mahututi Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), baada ya kupata ajali Dar es Salaam juzi. Lakini usiku wa kuamkia leo amefariki Dunia, Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina
JAMII YA WANAHABARI NCHINI INA MAJONZI YA KUPOTELEWA NA DANNY MWAKITELEKO, MPIGANAJI MWENZAO NA NAIBU MHARIRI MTENDAJI WA MAGAZETI  YA HABARI CORPORATION YA  MTANZANIA, RAI, DIMBA NA BINGWA AMBAYE USIKU WA KUAMKIA LEO ALIFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI KITENGO CHA MIFUPA (MOI) ALIKOKUWA AMELAZWA KUUGUZA MAJERAHA MAKUBWA ALIYOYAPATA KATIKA AJALI YA GARI SIKU NNE ZILIZOPITA JIJINI DAR ES SALAAM.

MSIBA UKO NYUMBANI KWA MAREHEMU TABATA  CHANG'OMBE  JIJINI DAR (UKITOKEA MJINI UNAPINDA KULIA UFIKAPO BARRACUDA, KISHA MBELE BARABARA YA PILI UNAINGIA KULIA TENA, UTAFIKA NA UKIKWAMA ULIZIA) NA MIPANGO YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU INAFANYWA NA FAMILIA. 

HABARI   ZINASEMA KWAMBA HUENDA DANNY AKASAFIRISHWA SIKU YA JUMATATU ILI KURUHUSU BOSI WAKE AMBAYE YUKO SAFARINI AWEPO NA KUSIMAMIA KILA KINACHOHITAJIKA KWA MSAFARA NA MAZISHI.

JANA JIONI RAIS JAKAYA KIKWETE ALIKUWA MIONGONI MWA WATU WALIOKWENDA KUMWANGALIA MAREHEMU HAPO MUHIMBILI. WANAHABARI WENGI TOKA VYOMBO MBALIMBALI WAMEKUWA WAKIMTEMBELEA MPIGANAJI DANNY, INGAWA KUMUONA ILIKUWA SI RAHISI KWANI ALIKUWA ICU NA KATIKA COMA MUDA WOTE.

DANNY, SISI TULIKUPENDA LAKINI MUNGU KAKUPENDA ZAIDI. TUTAMISS UCHESHI, UNYENYEKEVU NA UCHAPAKAJI KAZI ULIOTUKUKA NA ULIOKUFANYA UVUKE NGAZI ZOTE ZA KIUANDISHI NA KUWA NA CHEO KIKUBWA KATIKA UMRI MDOGO.

MOLA AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI 
ROHO YAKO DANNY MWAKITELEKO
- AMINA








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2011

    jamani danny mwakiteleko!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2011

    R.I.P Danny..tutakukumbuka sana na kukukosa sana kwenye MEDIA.

    David V

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2011

    yeye ametangulia sisi tupo nyuma yake. Mungu amlaze mahala pema peponi. Ameen

    ReplyDelete
  4. nimepokea kwa majonzi habari za DANNY...RIP Danny..tupo safarini,dunia ni mapito..

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2011

    Jamani nadhani sasa ni muda muafaka wa kufanya kampeni dhidi ya madereva na wamiliki wa malori kuwa responsible. Malori barabara ya mandela yameua saaana. Lori linaweza likaharibika lakini wasiweke sign yoyote. Wakati mwingine wala hayaharibiki ila amdereva wanakuwa wababe ikifika usiku wanapark malori barabarani. Hii ni nchi gani jamani ambayo sheria hazifwatwi??? Ina maana wahusika wameshindwa kuyashughulikia haya malori. Na madereva mnaotumia barabara ya mandela kuweni makini jamani, muendeshe kimtego mtego maana ikifika usiku unakuta malori yamezimwa barabarani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2011

    poleni sana wafiwa, sheria za barabarani ni zero wa bongo, watu wengi wanapoteza maisha kwa uzembe wa mtu mmoja, sasa kuna watu wamepoteza ambaye ndie mhimili wa familia!!!!! RIP

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2011

    Poleni wote mliofikwa na msiba huu mzito. Nakumbuka ni miezi michache tu iliyopita nilikutana na marehemu mara ya mwisho pale Sinza. Naungana na wadau waliotangulia katika kulaani matumizi mabaya ya barabara ya Mandela ya madereva wa malori. Ni kweli kabisa malori huwa yanaegeshwa katikati ya barabara hii usiku kwa kisingizio yameharibika. Mara nyingi kunakuwa hakuna ishara yoyote kuwa malori hayo yamesimama barabarani. Pia barabara hii hutumiwa na malori yaliyochakaa ambayo hutumika kubeba makontena na mizigo mingine kwenda eneo la viwanda la Mikocheni nyakati za usiku. Malori haya yasiyokuwa na taa, bima wala leseni za barabarani hutembea usiku tu kwa kuwa hayawezi kwenda zaidi ya mita 10 mchana bila kukamatwa. Kwa kifupi barabara hii ni hatari sana kwa wanaoitumia usiku.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2011

    Mh Zito Kabwe fanyeni kweli wewe ndo tegemeo pigeni kampeni kupunguza ajali hao madereve wanaweza kuwa vyanzo vikubwa vya mapato nchini.Zito tafadhari fanyieni kazi hilo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 23, 2011

    Kuna maeneo ya barabara hii yanayopaswa kuwekwa matuta kupunguza mwendo wa madereva la sivyo watu wataendelea kufa kila siku. Barabara hii ina magari mengi na inapita maeneo wanayoishi watu wengi lakini mwendo wa madereva wengi unatisha.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 23, 2011

    Ndugu na jamaa wote na familia ya Mwakiteleko Poleni sana na nawaombea Mungu awape uvumilivu na kuwatuliza wakati huu wa msiba mkubwa wa ndugu yetu Danny.Naamini Mungu ataendelea kuwafariji na kuwatuliza kwa hali zote zinazowakabili wakati huu.Bwana alitoa na Bwana ametwaa,jina la Bwana na lihimidiwe.

    Amani ya Bwana ikae nanyi nyote. Amin

    Rev. Mwalilino

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 25, 2011

    Kila jambo hupangwa na Mungu,
    Ni ngumu kubeba uchungu wa kuondokewa na mpendwa wetu lakini hatuna jinsi.
    Inshallah Mungu Aiweke Roho yake mahala pema peponi.

    Pole kwa familia, ndugu na jamaa wote.
    Mungu awape subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...