Salamaleoko Mjomba Ankal,
 Naomba niwekee huu msaada tutani katika globu ya jamii ili wadau wanisaidie ushauri.

Bw mdogo wangu ameomba US student visa kwa mara 3 bila mafanikio sababu ikidaiwa na ofisi ya visa ya Ubalozi wa Marekani ni uhalali na uhalisia wa Vyeti vyake vya kidato cha 6 na 4 .

Mara ya kwanza aliwasilisha cheti cha kidato cha 4 na Result slip inayoonyesha matokeo yake ya kidato cha 6 , afisa wa visa akasema anashindwa ku-verify result slip hio .Kwa bahati mbaya alikuwa hajaenda kuchukua cheti cha matokeo ya mitihani wa kidato cha 6 toka shuleni kwake .

Jaribio la 2
Aliwasilisha vyeti vyote viwili lakini afisa wa visa (tofauti na yule wa mwanzo) akasema ana shaka na certificate zote mbili na kama anahitaji ku-reapply arudi na proper verification.

Tuliwaandikia barua baraza la Mitihani (NECTA) kuomba wathibitishe uhalisia wa vyeti vyake . NECTA walijibu kwa kuandikia barua ambayo ilikuwa katika bahasha iliyofungwa na kugongwa muhuri wa CONFIDENTIAL ambayo nayo iliwasilisha wakati naomba visa mara ya 3.

Jaribio la 3
Aliwasilisha barua hio na maombi mapya ya visa , bahati nzuri alipofika getini ile barua ya NECTA ilifunguliwa na kupewa ikiwa wazi hivyo niliweza kusoma kilichoandikwa kabla ya kuiwasilisha kwa afisa wa visa .Barua hio ilithibitisha kuwa vyeti ni halali na halisi .

Afisa wa visa (tofauti na wa kwanza na pili) naye alikataa ombi hilo la visa akitoa sababu kuwa wamecheki katika record na kugundua kuwa shule aliyomalizia kidato cha 6 ilifutiwa mtihani mwaka huo 2006 jambo ambalo si kweli.

Nawasilisha katika blogu ya jamii swala hili kwa ushauri zaidi wa nini kifanyike

osicstz@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2011

    Poleni sana kwa matatizo unajua Marekani wanamatatizo sana ya kutoa Visa mimi naona bora umtafutie chuo kingine huyo kijana akasome. Kusoma si lazima iwe Marekani. kuna nchi nyingine kama Australia wana elimu nzuri tu kama hutaki kijana wetu asomee Tanzania.

    Tatizo hizi nchi sasa hivi zinaogopa wahamiaji. ingekuwa ni Masters bila shaka wasingemuekea kiwingu lakin Bachelor wanajua huyo mzamiaji.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2011

    Ndugu yangu waamerika hawakutaki uende kwao, tafuta shule kwingine. Si lazima kusoma huko. Mtu hataki uingie kwake usinganganie

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2011

    Nadhani si lazima aende USA. Nashauri hebu ajaribu Nchi zingine, lkn pia tumesikiza Upande mmoja tu upande wa USA hatujawasikia, kutoa hukumu ya aina hiyo ni htr

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 07, 2011

    Mdau bora utafute sehemu nyengine mwanao akasome hao wmarekani wameamua tu kukubania kilichobaki ni visingizio tu.Na kwavile washabana mara3 basi uwezekano wakupata tena ni mdogo sana.Kiukweli nikwamba hizo nchi zilizoendelea wanakua wagumu sana kutoa visa hasa student visa kwa watoto wanaotoka nchi maskini km tz.Ushauri wangu kama unapesa bado zipo nchi kibao ambazo elimu yake pia iko juu bora umtafutie nchi nyengine.Hao wamarekani hata hawana formula ktk kutoa visa kaka.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 07, 2011

    Omba nchi nyingine achana na USA.Mimi nipo USA kweli kwa Bachelor kuna kigugumizi sana kwani hizo sababu wanazotoa hazina msingi wowote.Mtazidi kumaliza pesa za kuombea visa bure.Hadi hapo umeishaunguza zaidi ya $500.Lakini pia kama unataka aje USA nenda na ng'ang'a nao kwa kwenda mbele hadi kieleweke labda utafaulu maana kuna wengine wanapata.Kwa masters ingekuwa rahisi tu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 07, 2011

    Hizi nchi kubwa sasa wanasera ya kupunguza wanafunzi kutoka nchi masikini. Wanafunzi wengi kutoka nchi masikini wakifika katika hizi nchi kubwa (tajiri) huwa wanazamia. Pengine mdogo wako ameonekana kuwa ni mmoja wa wazamiaji. Hivyo ubalozi wa Marekani wameamua kumkatalia viza. Lakini wanajaribu kutumia ujanja unaoitwa "Delaying tactics". Kama vile kusema vyeti vyako ni vya udanganyifu, matokeo yamefutwa, upeleke cheti halisi badala ya kikaratasi cha matokeo, cheti cha TB huna, chuo unachokwenda hakitambuliwi, picha hakufata viwango. Tena inawezekana anayetoa maelezo hayo ni Mbongo. Hizo ni mbinu za mfanyakazi hapo kauta anataka kitu kidogo. Kama unataka asome tu basi hizo pesa za kumsomesha marekani robo yake tu inatosha kumsomesha Malaysia

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 07, 2011

    Mi nafikiri uende mwenyewe ubalozini uombe kuongea na counselor, sio mpaka uende na kijana wako. Unaweza kupeleka passport yake tu, muulize if possible kupata sababu zilizofanya mtoto wako akanyimwa visa, watakueleza. Inawezakana kijana wako hakuwa competent, na make sure vitu vyako sio vya kuforge..

    Another issue, kama una chuo unaweza ukalipa hata semester moja ili kuonyesha kwamba u are serious abt this..

    Kama nia yako ni Marekani jaribu until u run out of options..don't be a quitter.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 07, 2011

    Pole sana,lakini sioni kwanini wakatae.Hawa marekani siku hizi hawataki watu kusema ule ukweli na kama ni kwa ajili ya masomo tu basi kuna sehemu nyingi za kusoma.Inategemea pia anataka kusomea nini lakini kama Australia,UK,hata India sio mbaya na bei pia itakuwa ni ya chini.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 07, 2011

    Mbona sehemu nyingine elimu yao ni bora kuliko huko US? Kama shida ni elimu basi aende akasome popote kule, lakini kama shida ni kutafuta maisha hilo nalo ni lingine. Ujue likuepukalo lina heri nawe msiwe mnang'ang'aniza vitu tu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 07, 2011

    Mi ninachojua kwa sasa hali ya uchumi ni mbaya hata walioko nje ya nchi wanabaniwa sana ktk nchi wanazokaa na hawataki mwanafunzi mwenye level ya chini angalau angekuwa na bachelor wangefikiria, but pia hali hii ya uchumi itamfanya hata akifika USA ashindwe kujikimu kimaisha na kuna msemo wa kiswahili unasema likuepukalo lina heri. Panga maisha Tz utafanikiwa tu. poleni

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 08, 2011

    Njia rahisi ya kupata stu_dent vi_sa ni kama hivi:
    1.Tafuta shule yenye bweni na iliyopo nje ya miji mikubwa, kuonyesha kuwa kweli unaenda kusoma na sio kujibabua mitaani.
    2.Lipia ada ya muhula wa kwanza,kuonyesha kuwa unazo pesa za kusoma maana utalipa ukifika anyway na ukikosa watakurudishia hakuna chakachua.
    3.Fanya kama umepata hiyo shule kwa kusearch kwenye internet wewe mwenyewe hata kama una jamaa kakuunganishia na uwe kweli unajua unapokwenda,hii inaonyesha upo makini na www technology na pia huna uhusiano na walioko huko.
    4.Kujiamini,hapa ndio wengi tunashindwa-jaribu kumwangalia usoni(eye contact) afisa wa maombi ya vi_sa wakati wa mahojiano na pia uliza maswali kama unayo hata kama lugha sio nzuri sana maana wanajua kuwa sio lugha yetu.
    5.Hakikisha vyeti na doc. zote ni shihihi na hakuna usanii.
    Hapo wakikunjima ujue Mare_kani sio rizki yako tafuta nchi nyingine

    -

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 08, 2011

    Muombee visa ya Canada halafu tuwasiliane na mimi, nina deal la kumpitisha njia za panya nikaingia nae hapa US na kumkabidhi BOX la kumkaribisha mjini. Baada ya muda atapata ujanja wa kuingia shule hapa Indiana au Illinois au hata kwa jirani zetu Ohio.

    Matari, INDIANAPOLIS

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 08, 2011

    Kaka Matari,
    Nakuona una moyo wa kusaidia. Na mimi ningeomba msaada wako. Nina shida ya mtoto wa ndugu yangu naye afanikishe deal kama hiyo. Kama hutajali na sintakusumbua, naomba tuwasiliane kwa email yangu: ak_abduel@yahoo.com
    Mungu akubariki sana

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 09, 2011

    MMMh Matari Kwa nini unataka kuja kuwatesa watoto wa watu hapa Marekani umpitishe njia za panya halafu akikamatwa si utamruka ft 20 na wala hatakusikia ..wacha kudanganya wenzako... Si shauri mtu yeyote kuinga wa njia zapanya...Vile vile mkumbuke maisha sasa hivi USA co sawa kama miaka mitano iliyopita maisha magumu kazi hakuna wanangalia makaratasi kama hupo kihalali shule nao pia wanaangalia status yako kwa iyo USA kwa SASA NI NOMA! ingia ki halali maisha yatakuwa powa co kwa njia za panya maana utakuwa na wasiwasi sawa na huyo panya!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...