NA VERONICA KAZIMOTO NA BITRICE MLYANSI - MAELEZO
Serikali imeamua kuandaa sera ya biofueli ili kukabiliana na changamoto mbalimbali kama vile uharibifu wa mazingira, migongano ya kiardhi, tishio la usalama wa chakula, kupanda kwa bei za vyakula, na mabadiliko ya mifumo ya ikolojia.
Akizungumza wakati wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 35 (sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Mtaalamu wa Kilimo na Mazingira kutoka mradi wa Biofueli Bi, Esther Mfugale amesema kuwa lengo la sera hii ni kusimamia uendelezaji endelevu wa biofueli nchini.
Tayari Wataalamu kutoka mradi wa biofueli nchini wameanza kutoa elimu kwa wananchi ili kuwawezesha kufahamu fursa mbalimbali na changamoto katika uendelezaji endelevu wa biofueli nchini.
“Lengo la elimu hii pia ni kuwapa uwezo wananchi kutoa mawazo na maoni yatakayozingatiwa wakati wa kuandaa sera ya uendelezaji endelevu wa biofueli hivyo sera hiyo itakuwa shirikishi,” amesema Bi Mfugale.
Amefafanua kuwa awamu ya kwanza ya elimu hiyo imeanza kutolewa katika mikoa ya Mwanza, Lindi, Manyara, Arusha pamoja na Singida, lengo likiwa ni kusambaza elimu hii nchi nzima.
Bi, Mfugale ameongeza kuwa elimu hii pia imekuwa ikitolewa kupitia Maonesho mbalimbali kama Wiki ya Utumishi wa Umma, Maonesho ya Sabasaba na Maonesho ya Wakulima-NaneNane.
Ili kufanikisha uendelezaji endelevu wa biofueli, Mradi huu umehusisha waatalamu kutoka katika sekta mbalimbali kama nishati, kilimo, maliasilina na ardhi. Sekta nyingine ni pamoja na mipango na matumizi ya ardhi, usalama wa chakula, maji, viwanda, ajira na mazingira.
Kwa jinsi bei za Petrol zinavyopaa kila siku hamna jinsi ni kujaribu njia mbadala.Nyie akina dada mlioandika hii habari na kutumia hilo neno BIOFUELI-mmekosa kabisa neno zuri la kiswahili??Gabon tutaenda kweli kufundisha kiswahili cha namna hii?BAKITA tusaidieni neno BIOFUEL kwa kiswahili linaandikwaje.
ReplyDeleteDaviv V
tunapoandika kwenye blog kwa kufurahisha wadau ni jambo moja,na tunapoandika habari za kitaalamu ili kufikisha ujumbe kwa jamii ni jambo jingine,sasa hawa waandishi wa habari inaelekea ama hawana eulewa wa lichokusudia kuandika hivyo wanafanya copy and paste ila kwa herufi za kiswahili,ama nao wameamua kuswahilisha msamiati wa kimombo.
ReplyDeletehuwezi kuniambia kwamba mradi wa nishati itokanayo na mimea ujulikanao kama biofuel imekuwa ni shida kuandika hadi wanatuandikia BIOFUELI!!!
pia nimegundu mara nyingi ukisoma habari utakuta kunakujirudia sana kwa haari ilimradi tu ukurasa uwe mrefu kaktika gazeti,hii inaonyesha ufinyu wa uelewa wa baadhi ya hao wandishi,habari sio lazima ijaze ukurasa,chamsingi ni ujumbe ufike tena kiufasaha na ikiwezekana kwa kina bila kumchosha msomaji kwa kurudia kitu kilekile.
wengine fumbukeni macho.