Mtihani wa Uwakala wa Wachezaji wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Septemba 29 mwaka huu. Mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili; maswali kutoka FIFA na kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika saa 4 asubuhi.
Kwa Watanzania wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wafike TFF ili waweze kupewa taratibu za mtihani huo ambao ada yake ni dola 50 za Marekani.
Wahusika wa mtihani huo ni wale wanaotaka uwakala kwa mara ya kwanza. Kwa wale wenye leseni za uwakala wanatakiwa kuziuhisha (renew) kila baada ya miaka mitano.
Mpaka sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA.
Mawakala hao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro, John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Ndugu Wambura,
ReplyDeleteShukran kwa taarifa hii nzuri sana!
Tunaomba pia tupewe anwani ya barua pepe na simu ili tupate mawasiliano na taarifa zaidi kwa sisi Wadau tulio mbali.
Ahsante
Storming