Kamati ya Rufani ya TFF iliyokaa Julai 23 mwaka huu imesikiliza rufani iliyokatwa na Mwamuzi wa Daraja la Kwanza, Kamwanga Tambwe. Baada ya kuangalia nyaraka zilizotolewa kwenye kamati, kumsikiliza na kumhoji, kamati imefikia uamuzi ufuatao;
Kamati ya Rufani imeona rufani hii haina msingi, na hivyo kutoa adhabu
zifuatazo;
1. Kumfungia Mwamuzi Kamwanga Tambwe kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Oktoba 20, 2009 kulingana na Ibara ya 45 (ii) ya Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikisomwa pamoja na Kanuni za Nidhamu za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Ibara ya 62(ii).
2. Fedha shilingi laki mbili (200,000/-) zilizohusishwa na rushwa katika shauri hili, kufuatana na kifungu 62(iv) cha Kanuni za Nidhamu za FIFA zibaki TFF kwa shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu.
Imesainiwa na Wajumbe wa Kamati ya Rufani;
Prof. G. Mgongo Fimbo

- Mwenyekiti
Dk. Ong’wanuhama Kibuta -
Makamu Mwenyekiti
Lt. Kanali mstaafu Idd Kipingu
- Mjumbe
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Jamal Rwambow - Mjumbe
Henry Tandau
- Mjumbe
Makamu Mwenyekiti
Lt. Kanali mstaafu Idd Kipingu
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Jamal Rwambow - Mjumbe
Henry Tandau
- Mjumbe
Taarifa za nyongeza:
Tambwe na wenzake walifungiwa maisha na Kamati ya Mashindano ya TFF kwa tuhuma za kupokea rushwa kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Majimaji ya Songea na Mtibwa Sugar ya Morogoro iliyochezwa mwaka 2009. Awali walikata rufani Kamati ya Nidhamu ya TFF ambayo iliwapunguzia adhabu hiyo hadi miaka mitatu. Tambwe kwa upande wake hakuridhika na uamuzi huo, hivyo kukata rufani Kamati ya Rufani ya TFF.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Kamati ya Rufaa naipa hongera sana. mambo haya yamezidi katika ligi yetu. Msimu mpya unaanza. sasa muwe makini TFF na waamuzi wenu. maana msimu uliopita ilikuwa inatia mashaka sana, marefa 4 ( wa kati, wa vibendera na wa mezani) wanakuwa ni wale wale katika mechi zaidi ya 6 katika mechi zinazohusisha Simba. wanachofanya wa kati anakuja mezani wa upande huu anakwenda mwingine mpaka ligi inakwisha.na maamuzi yanaonekana dhahiri kuwa yanaionea timu pinzani ya Simba. sasa na upangaji wa marefa nao uwe makini ili kuondoa upangaji wa matokeo. hii hali imekuwa ikifanyika kwa muda mrefu sana. maana kama msimu uliopita marefa walijitahidi sana kubeba timu fulani, lakini kwa kuwa uwezo wa timu hiyo uwanjani ulikuwa chini ikashindikana kuwa mabingwa na hivyo aliyekuwa na uwezo uwanjani akachukua KOMBE. sasa msimu huu tunataka HAKI mwanzo wa ligi hadi mwisho. Angalizo Mjumbe Rwambow usilete Unazi wako kwenye hiyo Kamati. Huaminiki!
ReplyDelete