Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (wa pili kulia) akiwa na mtoto wake ambaye walinusurika kufa maji na wazee ambao walifika kumpa pole nyumbani kwake Ludewa leo,baada ya kumaliza ziara ya mwambao

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (wa pili kulia) akiwa na mtoto wake ambaye walinusurika kufa maji na wazee ambao walifika kumpa pole nyumbani kwake Ludewa leo,baada ya kumaliza ziara ya mwambao
Mtumbwi uliompakia mbunge Filikunjombe na mwenyekiti wa CCM Ludewa ukivutwa kutoka ziwa nyasa na watoto. Picha na Habari na Mpiganaji Francis Godwin

Wapiga kura wa jimbo la Ludewa mkoani Iringa leo wamejitokeza kwa wingi nyumbani kwa mbunge wao Deo Filikunjombe kwa ajili ya kumpa pole kwa misukosuko aliyoipata kwa kutumbukia katika ziwa nyasa baada ya mtumbwi wake kupinduka jana asubuhi alipokuwa katika ziara ya kuwatembelea wapiga kura wake wa kata za pembezoni mwa ziwa hilo.

Wapiga kura hao wakiongozwa na wazee maarufu wa jimbo hilo walianza kujitokeza nyumbani kwa mbunge huyo eneo la Ludewa mjini baada ya mtandao huu na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti juu ya mbunge huyo kunusurika kifo katika ziwa hilo.

Hata hivyo Mbunge Filikunjombe amewapongeza tena wapiga kura wake kwa moyo wa upendo na kuwapongeza madiwani wa tarafa ya mwambao kwa kujitosa majini kumwokoa na kuwa lengo la ziara hiyo ni ilikuwa ni kwenda kuwakabidhi boti wananchi hao wa pembezoni na gari ya wagonjwa pamoja na vifaa vya michezo kwa vijana kama njia ya kuhamasisha maendeleo ya jimbo hilo.

Pia alisema kuwa eneo hilo ambalo alipata ajali pia limekuwa na historia ya kutokea ajali mbali mbali na kuwa mbali ya mbunge wa zamani kupinduka katika eneo hilo bado viongozi wa CCM wilaya walipata kupinduka eneo hilo ambalo linaongoza kwa kuwa na mawimbi zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2011

    Ankal Ludewa ipo mkoa mpya wa Njombe siyo Iringa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...