"Posho ndogo mzigo mkubwa tutafika kweli"?, Wasukuma mkokoteni wakiwa bize kusukuma mkokoteni uliosheheni mikungu ya ndizi katika barabara ya Nyerere mjini Dodoma wakielekea katika Soko la Majengo kama walivyonaswa na mpiga picha wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2011

    Bongo tambarare,huyu jamaa anaelimu sawa na baadhi ya wabunge wetu,lakini ni bahati mbaya tu hakuweza kuchaguliwa au hakupata nafasi kwenye ofisi za serikali.
    Hivyo anakuwa na maisha haya ya taabu bila kuwa na chuki na aliowachagua ambao wanalipiwa kila kitu na serikali yake(nyumba,magari,mafuta,ada za shule,nk. nk.).
    Je hakuna viongozi waliokuwa na elimu ya kidato cha nne au chini kwenye serikali yetu?
    Ombi kwa viongozi fikiria ungekuwa wewe katika hali hii ungekuwaje?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2011

    Hee mdau umenikumbusha stori moja mwaka 1997 nilikuwa Mwanza na Canadians wawili ambao ilikuwa mara yao ya kwanza kufika Afrika.

    Wakati tunakwenda kituo cha Utafiti Ukiriguru tulikutana na wasukuma mkokoteni wameujaza mapanki siyo mchezo (kama hao hapo juu walivyojaza ndizi).

    Sasa kilichowashangaza ni kwamba walikuwa wanakokota bila ya viatu (yaani walipiga kelele - pushing the cart without any shoes!!!!). Aah mimi nilijionea ni sawa tu maana nimezoea ile hali.

    Ingetokea wakafika tena miaka 15 baadae wanaona bado watz wanasukuma mkokoteni bila ya viatu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...