Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Emmanuel Nchimbi (kulia) akisalimiana na Naibu waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua (katikati) katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma leo.Zhao pamoja na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China. Kulia ni Zhao Haisheng aliyeapambana na ujumbe huo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Utamaduni,Anjela Ngowi akimvalisha kanga naibu waziri wa Utamaduni wa China, Zhao Shaohua wakati naibu waziri huyo alipotembelea mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuonana na viongozi wa Serikali huku waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi (katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni Prof. Helmasi Mwansoko (kulia) wakishuhudia . Zhao pamoja na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.

Naibu waziri wa Utamaduni wa China,Zhao Shaohua akiangalia ngoma ya kabila la kisukuma iliyokuwa inachezwa na kikundi cha ngoma cha Mwinamila cha mjini Dodoma wakati naibu waziri huyo alipowasili mjini Dodoma leo kwa ajili ya kuonana na viongozi wa Serikali . Zhao pamoja na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.
Naibu waziri wa Utamaduni wa China,Zhao Shaohua akiangalia zawadi ya picha ya pundamilia aliyopewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodima. Zhao pamoja na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.
Waziri Mkuu Mizengo Pinga akiangalia zawadi ya chombo cha kuwekea sukari aliyopewa na Naibu waziri wa Utamaduni wa China Zhao Shaohua wakati naibu waziri huyo alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodima. Zhao pamoja na ujumbe wake wako nchini kwa ziara ya kikazi ya siku nne ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano ya kitamaduni baina ya Tanzania na China.Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...